Escrow account ni uhujumu uchumi kwa Sethi, Rugemalira lakini siyo kwa SIMBA TRUST?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
186,748
2,000
Kushtakiwa kwa Sethi na Rugemalira huku baadhi ya wamiliki wa IPTL kama Simba Trust hawaguswi ni majibu mepesi kwa maswali magumu

Escrow account tunaambiwa ilikuwa na $250 mill lakini zilizolipwa ni $122.1 mill zilizobakia jumla ya 127.9 mill ni nani walilipwa na kwa maelekezo ya nani?

Hivi kutoa na kupokea rushwa si ni jinai tu sasa inakuwaje "baadhi" tu ya waliotoa rushwa washughulikiwe lakini waliopokea rushwa walindwe? Selective justice hupelekea kesi kufutwa kwa ubaguzi na " misjoinder of the accused."

Waliopokea rushwa hawawezi kuwa mashahidi bali watuhumiwa.

Hata kama SIMBA TRUST na wale waliohongwa wakifunguliwa kesi tofauti na hii ya akina Sethi na Rugemalira ni kuzidhoofisha kesi hizo zote kwa sababu tukio, muda na makosa ni yale yale

Naona ni reality TV ndiyo inaendelea
 
demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,234
2,000
Imeamrishwa Mikataba ya madini tu ikajadiliwe Bungeni ila sio mikataba mingine.

Ufisadi unahukumiwa nusu tu ila mingine kapuni.

Kila kitu nusu nusu....

TiGo walilitambua hili wakaja na Kampeni ya
Jaza Ujazwe.

Hatuwezi kumjaza raisi Magufuli upendo mpaka ajaze maamuzi yake na watendani wake.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
5,226
2,000
Tatizo kesi za ufisadi huwaga zinacreat attention kubwa mwisho wa siku inatoka hukumu ya kijinga, yaani haina tofauti na watu walioalikwa ktk sherehe alafu wanafanyiwa surprise ya kunawisha mikono na mafuta ya kula, vichwani mwao wanajua labda Kuna vinono kumbe MAFENESI.Ila naipongeza serikali kwa 50%, 50% nyingine na baki nayo manake yasijekuwa yale ya MRAMBA na YONA na naona yale yale ya Kagoda, yanajirudia.
 
Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
4,999
2,000
Kushtakiwa kwa Sethi na Rugemalira huku baadhi ya wamiliki wa IPTL kama Simba Trust hawaguswi ni majibu mepesi kwa maswali magumu

Escrow account tunaambiwa ilikuwa na $250 mill lakini zilizolipwa ni $122.1 mill zilizobakia jumla ya 127.9 mill ni nani walilipwa na kwa maelekezo ya nani?

Hivi kutoa na kupokea rushwa si jinai tu sasa inakuwaje waliotoa rushwa washughulikiwe lakini waliotoa rushwa walindwe?

Waliopokea rushwa hawawezi kuwa mashahidi bali watuhumiwa.

Hata kama SIMBA TRUST na wale waliohongwa wakifunguliwa kesi tofauti na hii ya akina Sethi na Rugemalira ni kuzidhoofisha kesi hizo zote kwa sababu tukio, muda na makosa ni yale yale

Naona ni reality TV ndiyo inaendelea
Acheni kiherehere. Mlijua kama Seth na Ruge wangefikishwa mahakamani jana?
Kinachowafanya muamini huko kwingine Ngosha hatafika ni nini?
 
mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,213
2,000
JPM anajua kweli kucheza na akili za watanzania, sasa amehamisha mziki wa makinikia umesahaulika now tunaimba IPTL...wale kina Masamaki imekuwa zilipendwa watu wengi hawapendi mambo yaliyopita, atapigiwa makofi kwelikweli kwa kuminya majipu ila kuayatumbua hathubutu..
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
186,748
2,000
Tatizo kesi za ufisadi huwaga zinacreat attention kubwa mwisho wa siku inatoka hukumu ya kijinga, yaani haina tofauti na watu walioalikwa ktk sherehe alafu wanafanyiwa surprise ya kunawisha mikono na mafuta ya kula, vichwani mwao wanajua labda Kuna vinono kumbe MAFENESI.Ila naipongeza serikali kwa 50%, 50% nyingine na baki nayo manake yasijekuwa yale ya MRAMBA na YONA na naona yale yale ya Kagoda, yanajirudia.
Haki ni kwa wote siyo kwa baadhi tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom