Erolink yamtunishia misuli Waziri Kabaka

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
419
Habari wana-JF

Mtakumbuka mwezi uliopita mnamo 27.01.2014 na kuendelea kulikuwa na mjadala mkali ulioshika hatamu kwenye vyombo vya habari, ambapo waziri wa kazi na ajira Mhe. Gaudensia Kabaka alitoa tamko la serikali na kuzitaka kampuni zinazofanya udalali wa kuajiri ikiwemo Erolink kusitisha zoezi hilo mara moja, na kuwahamishia wafanyakazi hao kwenye kampuni husika wanakofanyia kazi kabla au kufikia tar. 28.02.2014

Vile vile alitoa wito kwa makampuni hayo kujisajili kwa Kamishna wa ajira ili waweze kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za kazi tofauti na awali.

Sasa jana tar. 27.02.2014 ikiwa imebaki siku moja kabla ya tarehe iliyotajwa na waziri kuwa ndiyo deadline, Erolink imewatumia wafanyakazi wake wanaofanya kazi customer care ya pale Vodacom sijui tuite ni taarifa, waraka mfupi au barua (nachelea kuiita barua maana haijakidhi vigezo vya kuitwa barua maana haina muhuri wa ofisi pamoja na kasoro kibao). Katika maelezo ya 'barua' hiyo waliyotumiwa Erolink inasema kuwa ime-decline wito wa Kamishna wa ajira inayowataka wajisajili kama Private Employment Promotion Agency kwa sababu Erolink haijawahi kusajiliwa kama Private Employment Promotion Agency.

Naomba niweke maelezo ya hiyo barua hapa;

RE: THE MINISTER OF LABOUR AND EMPLOYMENT’S DECREE AS PUBLISHED ON THE 27[SUP]TH[/SUP] JANUARY 2014
Reference is made to the Minister’s Decree ordering all Private Employment Promotion Agencies to cease operating as outsourcers of services.

We would like to inform the staff that Erolink has never been registered as Private Employment Promotion Agency by the Commissioner for Labour, and although we are grateful to the Commissioner for his invitation to us to register as a Private Employment Promotion Agency under section 20 of the National Employment Promotion Service Act Cap.243 R.E 2002, we have decided to respectfully decline the said invitation and concentrate on our core business of outsourcing services to clients

Yours sincerely
….<signature>….
Management

Nawasilisha.
 
Serikali ilidai haikukurupuka let's wait and see!! ila kwa habari ninazozipata kutoka kwa wafanyakazi walio chini ya hao jamaa hatuwezi kuvumilia kuona vijana wetu wanyanyasike, watumikishwe kama watumwa ndani ya nchi yao tena chini ya serikali huru na sikivu!! Erolink najua mnajua kuwa mnawaonea watoto wa maskini wasio na pakuenda lakini mjue watanzania wanajua nini mnachofanya ipo siku!
 
Habari wana-JF

Mtakumbuka mwezi uliopita mnamo 27.01.2014 na kuendelea kulikuwa na mjadala mkali ulioshika hatamu kwenye vyombo vya habari, ambapo waziri wa kazi na ajira Mhe. Gaudensia Kabaka alitoa tamko la serikali na kuzitaka kampuni zinazofanya udalali wa kuajiri ikiwemo Erolink kusitisha zoezi hilo mara moja, na kuwahamishia wafanyakazi hao kwenye kampuni husika wanakofanyia kazi kabla au kufikia tar. 28.02.2014

Vile vile alitoa wito kwa makampuni hayo kujisajili kwa Kamishna wa ajira ili waweze kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za kazi tofauti na awali.

Sasa jana tar. 27.02.2014 ikiwa imebaki siku moja kabla ya tarehe iliyotajwa na waziri kuwa ndiyo deadline, Erolink imewatumia wafanyakazi wake wanaofanya kazi customer care ya pale Vodacom sijui tuite ni taarifa, waraka mfupi au barua (nachelea kuiita barua maana haijakidhi vigezo vya kuitwa barua maana haina muhuri wa ofisi pamoja na kasoro kibao). Katika maelezo ya 'barua' hiyo waliyotumiwa Erolink inasema kuwa ime-decline wito wa Kamishna wa ajira inayowataka wajisajili kama Private Employment Promotion Agency kwa sababu Erolink haijawahi kusajiliwa kama Private Employment Promotion Agency.

Naomba niweke maelezo ya hiyo barua hapa;

RE: THE MINISTER OF LABOUR AND EMPLOYMENT’S DECREE AS PUBLISHED ON THE 27[SUP]TH[/SUP] JANUARY 2014
Reference is made to the Minister’s Decree ordering all Private Employment Promotion Agencies to cease operating as outsourcers of services.

We would like to inform the staff that Erolink has never been registered as Private Employment Promotion Agency by the Commissioner for Labour, and although we are grateful to the Commissioner for his invitation to us to register as a Private Employment Promotion Agency under section 20 of the National Employment Promotion Service Act Cap.243 R.E 2002, we have decided to respectfully decline the said invitation and concentrate on our core business of outsourcing services to clients

Yours sincerely
….<signature>….
Management

Nawasilisha.

Kifungu cha sheria kimetajwa.., unaambiwa ufanye according to the said Act wewe unasema unadecline..???!!, ni kama mimi nikutwe naiba .., niambiwe acha kuiba kulingana na sheria namba flani.., halafu niseme na decline tena respectfully..???! bullsh*t..!!!! hivi kwani kufuata sheria ni ombi au wajibu..??!!
 
Au ndio tuanze kuamini zile tetesi za magazeti kuwa hii kampuni ina mkono wa vigogo fulani wa serikali na vile vile mkurugenzi wa hii kampuni (Elvis Rodgers) baba yake aliwahi kuwa MD wa bank fulani hapa nchini so kuna invisible hands hapa.
 
Kifungu cha sheria kimetajwa.., unaambiwa ufanye according to the said Act wewe unasema unadecline..???!!, ni kama mimi nikutwe naiba .., niambiwe acha kuiba kulingana na sheria namba flani.., halafu niseme na decline tena respectfully..???! bullsh*t..!!!! hivi kwani kufuata sheria ni ombi au wajibu..??!!

Hapo hapo ndipo pananichanganya, unadecline to comply with the said law....tena respectifully!!!
 
Hao erolink ni matajiri lkn still vilaki sita vya watoto wa maskini wanavitolea macho....km alivosema mdau hpa juu hyo mkurugenzi wa erolink babake alikuwa MD wa bot it seems mtoto wa kishua hajawahi ku experience shida so anayafanya anaona sawa tu...aende tandale some watu wanavyosomesha watoto wao kwa shida
 
Ni kwa nini hizo kampuni zilizopewa huduma ya outsource wasitii maagizo ya serikali kwa kuingia nao mkataba wafanyakazi wenyewe direct? hivi serikali hii inauwezo wa kusimamia jambo lipi na likaheshiwa?
 
jana waliitisha kikao cha gafla na wafanyakazi kitu ambacho walichozungumza eti " wamewaajiri wafanyakazi then wakawauzia vodacom" inamanaa erolink inaziilisha kuwa inafanya biashara ya utumwa!!!
 
Like 5 kwako mkuu dj1000
 
Last edited by a moderator:
Sio Erolink tu, makampuni yote ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta wana mikataba na tukampuni uchwara twa kutumikisha. Halliburton, Shrumberger, Erricson, Statoil na menginewe.

Haya maagizo na maneno ya kwenye khanga vimeachana padogo sana
!
 
Jaman kuna hii inaitwa Ison ipo customer care ya airtel na Tigo yaan wenyewe ndo hawana hata mpango wakucomply na leo wanapamba tigo customer care wanasherehekea kutimiza miaka 2!!!
 
Wanalipa watoto wa watu 270000/= yaan ni waonevu sana wahindi hawa yaan watu wanaonewa nchini mwao,serikali nayo iamke jmn
 
Erolink na recruiment agency nyingine wakae wakijua hta km wata skip time hii hawana muda kwny industry hii ajira coz dhulma hues haidum hta cku moja
 
Serikali inabidi iliangalie hili, hawa watu walininyonya hadi nikaamua kuacha kazi maana unafanyakazi Usiku na mchana ( shift) lakini salary 270K maisha yenyewe yamepanda na Rene Meza (M.D. VODACOM ) Anafahamu kwani yeye alipokuja ndo alishusha mishahara zaid.Kiukweli inaudhunisha sana nikikumbuka hayo maisha ambayo watoto wa watanzania wenzetu wanafanyiwa ndani ya nchi huru.
 
Duh! Ila hii gvnt yangu cjui nitaiamini lini na kwa lipi asee.... yan tamko linatolewa af jamaa wanapiga kazi kama kawaida tena bila uoga wwte. Watu waliamin tar 28 ni ijumaa bac j'3 ndo yaliyokua yakisemwa na kujinadi kwny media na hawa viongozi wetu yangetimizwa bt hola. Cjui ndo niamini matamko hutolewa ili watu wapate chance za kupiga pesa kwa kuunda kamati za uchunguzi au kuwatisha upande wa pili ili pesa iongee...!!(rushwa). Kwa hili tunahitaji serikali iliyomakini na c kugeuzwa vyanzo vya mapato kwa baadhi ya viongozi wetu na hayo mashirika.
 
Habari wana-JF

Mtakumbuka mwezi uliopita mnamo 27.01.2014 na kuendelea kulikuwa na mjadala mkali ulioshika hatamu kwenye vyombo vya habari, ambapo waziri wa kazi na ajira Mhe. Gaudensia Kabaka alitoa tamko la serikali na kuzitaka kampuni zinazofanya udalali wa kuajiri ikiwemo Erolink kusitisha zoezi hilo mara moja, na kuwahamishia wafanyakazi hao kwenye kampuni husika wanakofanyia kazi kabla au kufikia tar. 28.02.2014

Vile vile alitoa wito kwa makampuni hayo kujisajili kwa Kamishna wa ajira ili waweze kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za kazi tofauti na awali.

Sasa jana tar. 27.02.2014 ikiwa imebaki siku moja kabla ya tarehe iliyotajwa na waziri kuwa ndiyo deadline, Erolink imewatumia wafanyakazi wake wanaofanya kazi customer care ya pale Vodacom sijui tuite ni taarifa, waraka mfupi au barua (nachelea kuiita barua maana haijakidhi vigezo vya kuitwa barua maana haina muhuri wa ofisi pamoja na kasoro kibao). Katika maelezo ya 'barua' hiyo waliyotumiwa Erolink inasema kuwa ime-decline wito wa Kamishna wa ajira inayowataka wajisajili kama Private Employment Promotion Agency kwa sababu Erolink haijawahi kusajiliwa kama Private Employment Promotion Agency.

Naomba niweke maelezo ya hiyo barua hapa;

RE: THE MINISTER OF LABOUR AND EMPLOYMENT’S DECREE AS PUBLISHED ON THE 27[SUP]TH[/SUP] JANUARY 2014
Reference is made to the Minister’s Decree ordering all Private Employment Promotion Agencies to cease operating as outsourcers of services.

We would like to inform the staff that Erolink has never been registered as Private Employment Promotion Agency by the Commissioner for Labour, and although we are grateful to the Commissioner for his invitation to us to register as a Private Employment Promotion Agency under section 20 of the National Employment Promotion Service Act Cap.243 R.E 2002, we have decided to respectfully decline the said invitation and concentrate on our core business of outsourcing services to clients

Yours sincerely
….<signature>….
Management

Nawasilisha.

Me nipo hapa ison bpo call centre ya Tigo hapa lugoda makao makuu ya Tigo ya zamani. Kazi nimeichoka ila kuiacha siwezi kulingana na maisha kuwa magumu. Ninachofanya kusave energy yangu isitumike kwa kulipwa kidogo ni kukata simu za wateja wao wote tukose. Kama Tigo wanafanya biashara na wanataka faida why wanaadeal na outsourcing agency mean hata Tigo hawapo serious na kazi zao.
 
Ha ha haaaa, nimeipenda style yako kaka, halafu ili usionekane umekata usitumie mouse maana mshale wa mouse utaonekana unavyokata. Unatumia combination fulan fulan ya button za kwenye keyboard (kulingana na system unayotumia) hii kitu ipo hii.
 
masikini watanzania tunakuwa watumwa kwenye nchi yetu wenyewe
 
anaekaa na kuamini kuwa agizo la waziri litatekelezeka ni kichaa, mwenzake alisema jengo pacha na lililoanguka livunjwe nn kimefanyika hadi leo?
 
Back
Top Bottom