Epuka sana kukopesha mtu pesa

Epuka sana kukopesha mtu pesa

Mpeleke Kwa mjumbe au Polisi adhalilike hapo mtaani kuwa kumbe anaishi Kwa ubabaishaji mjini.

Wanasema Gari alonayo n.k kumbe anavipata Kwa ubabaishaji na kukopa bila kulipa madeni ya watu kwa wakati.

Mwache adhalilike ni funzo pia!
 
Aisee. Mdaiwa afungwi.
Katika maisha yako ya utafutaji epuka sana kumkopesha mtu pesa kwa lengo la kurudishiwa pesa yako ya awali.

Kumbuka kuwa pesa unayompa mtu kwa mkopo sio yako tena.

Aliwahi kuniambia baba yangu"mtu akikuomba umkopeshe pesa mpe nusu ya pesa alio omba kama sadaka mbele ya Mungu, Ila usije weka matarajio yeyote kwa pesa uliomkopesha mtu.

Mfano
Rafiki akikuomba umkopeshe elfu Kumi, basi wewe kiroho Safi mpe elfu tano ili kumuwezesha katika jambo husika.

Sio ndugu
Sio rafiki
Wala nini.

Usikopeshe Ila wezesha.

Wapo wengi sana walirudishwa nyuma kwa kukopesha pesa kwa watu.

Asante
Kwa hiyo mtu akiomba mkpo milioni tano mpe miliono mbili na nusu kama sadaka... huyo babaako alikuingiza mkenge...
 
Ila hao matajiri wanakopeshana pesa pia.

Binafsi naona, tukopeshane tu pesa kwa sababu wengine tunakuwa tumetingwa na hatuna namna.

Binafsi naona ni bora kuwa na marafiki na ndugu wachache wenye tija, kuliko kuwa na marafiki na ndugu wengi wasio na tija.

Yaani nikiwa na shida usiponikopesha pesa wakati unazo, basi nakata mawasiliano na wewe kwa sababu hauna faida kwangu. Ukiugua siji kukuona, ukipata msiba siji, pesa zako zikusaidie!

Unaweza kuwa na pesa, ila unahitaji msaada wa wafu pia, mf, nguvu kazi ukiwa unashida.

Tukopeshane, kwa sababu tunategemeana. Mtu mmoja akikudhulumu isiwe kigezo cha kuacha kukopesha wengine waaminifu.
Hopeless
 
Kinachofuata ni kupoteza urafiki/udugu na pesa zako pia. Mtu akitaka kukukopa ni bora umuelekeze kwenye taasisi za fedha akakopeshwe huko.
Wengine hawaendi kwenye taasisi za mikopo kwa sababu wanakwepa uwajibikaji.
 
Umesema hawafungwi ?

Wanafungwa vizuri.

Ukiiweka kesi vizuri anafungwa.

Usiweke kesi ya madai weka iwe kesi ya utapeli, ulaghai, wizi wa kuaminiwa haponi mtu hapo hata dhamana ni Kwa mbinde!
Wizi wa kuaminiwa ndio upoje mkuu ?
 
Kila mtu ana hela humu....duu sometimes unakuwa huna hela,..michongo yote imebuma...sa itabidi tukwepane tu..
 
Uko sahihi.
Ila, suala la kukopesha haliendani na ulichoandika.
Ukiopesha unastahili kurudishiwa bila kujali uwezo wako.
Vinahusiana......kukopa ni njia mojawapo ya kusaidiana na wewe kulipwa ni haki yako.....shida inakuwa kwa sisi ambao tunakopeshana kibinadamu na sio kimikataba......kinachotusukuma ni ubinadamu zaidi.....na hayo ambayo huleta majuto ikiangukia kwenye mikono ya watu wasiokuwa waaminifu
 
Wizi wa kuaminiwa ndio upoje mkuu ?



Pale ambapo unampa mtu pesa au mali/kitu kwa kumwamini kwa muda ili baada ya muda akurejeshee lakini badala yake hakurudishii anachukichia nacho/nayo.

Au kumpa mtu pesa (mfano advice payment) ya bidhaa au huduma fulani halafu asikupatie hiyo bidhaa au huduma mlokubaliana.

Huo ni aina ya wizi.
 
Ila hao matajiri wanakopeshana pesa pia.

Binafsi naona, tukopeshane tu pesa kwa sababu wengine tunakuwa tumetingwa na hatuna namna.

Binafsi naona ni bora kuwa na marafiki na ndugu wachache wenye tija, kuliko kuwa na marafiki na ndugu wengi wasio na tija.

Yaani nikiwa na shida usiponikopesha pesa wakati unazo, basi nakata mawasiliano na wewe kwa sababu hauna faida kwangu. Ukiugua siji kukuona, ukipata msiba siji, pesa zako zikusaidie!

Unaweza kuwa na pesa, ila unahitaji msaada wa wafu pia, mf, nguvu kazi ukiwa unashida.

Tukopeshane, kwa sababu tunategemeana. Mtu mmoja akikudhulumu isiwe kigezo cha kuacha kukopesha wengine waaminifu.
😂😂Mbona kama umepanic?
 
Hii kweli kabisa,

Juzi nimeingia kwenye mtego, nimemkopesha mdada aise, Sijui atanilipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nna rafiki zangu watatu rafiki zangu sana na ni wanaume... Hawajawahi kuniazima ela hata siku moja Ila Mimi huwa nawaazima lakini nawarudishia... Mmoja kati yao nilimuazima wakati narudisha akakataa kuipokea basi mpaka Leo Sina ujasiri wakumuazima Tena...
Ila Hawa wengine kama kawa
 
kopesha kwa faida ila isiwe ndugu ama rafiki,hao watu watakulostisha!
 
Kuna mmoja huyo nimemwambia ulikolalia ndiko nilikoamkia!

Nimemwambia usizani nitakufungulia kesi ya madai ili unilipe unavyotaka wewe!

Nimemwambia itajulikana nani amezaliwa Muhimbili na nani alifanya kuja mjini!
 
Back
Top Bottom