Epuka makosa yaliyotendwa na " Yahoo"

Epuka makosa yaliyotendwa na " Yahoo"

Nakubaliana Na wewe mkuu. Ubunifu, marketing strategies n.k inqchangia Sana.

Pia CEO anachangia Sana. CEO wa Nokia aliiangusha Sana wakati angekubali ushauri Nokia itumie Android badala ya windows ingekuwa mbali sana. Kuanguka kwa Nokia inasikitisha Sana.

Hata baada ya kununuliwa na Microsoft mwaka 2014 na kuendelea kutumia windows bado hawakufanya vizuri. Microsoft walitaka kuitumia Nokia kama karata yao ya kuingia kwenye soko la simu janja. Move iliyo-fail vibaya mpaka Microsoft walipoamua kuiuza Nokia tena majuzi.

Nadhani Nokia, Microsoft, walichelewa sana ku-adopt changes za kiteknolojia wakakuta Samsung, Apple, na Google wameshalishikilia soko la smart phone.
 
Mada ni nzuri Ila umejichanganya kuingiza maswala ya mahusiano. Ungebaki hukohuko kwenye fursa za kibiashara ingeleta maana zaid
 
inamaana google ikiuzwa inaweza kuilisha tz kwa miaka 10?
 
Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.
Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.
Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni "ndogo"
Lakini Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG] ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya "mbwa" (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG] ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio "Boss" anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990's lakini kwa sasa imebaki "Skrepa". Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.
Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata "department" ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG] nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Vivyo hivyo katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani.
Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG] nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na "Offer" walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa bei ya kuku za kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe "too much". Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama "Yahoo"… una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini "natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana". Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea kama Yahoo. Hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25, wakati wewe una 40.

Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonize. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua form one?? Lakini leo wanaitana mababy?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio issue. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la "akina bibi wanaolea wajukuu zao"

Lakini hupati "husband material". Unawapata "maplay boy" wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza "umemaliza eddah" wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng'o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la "Jihadhari mbwa mkali" lililokuwa getini anaweka tangazo jipya "tunauza barafu" Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga "plasta" nyumba yenu.
My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata.

Usiringe Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Usifanye makosa ya "Yahoo".!
Well done [emoji8]
 
USIFANYE MAKOSA YA YAHOO.!

By Malisa GJ,

Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana).

Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.

Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.

Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni "ndogo"

Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:

Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG] ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya "mbwa" (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG] ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio "boss" anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990's lakini kwa sasa imebaki "skrepa". Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.

Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata "department" ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG] nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo halafu kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG] nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi mwisho utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na "Offer" walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa sawa na bei ya kuku wa kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe "too much". Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama "Yahoo"... una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini "natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana". Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea. Unagundua hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unaamua kuretreat kama Yahoo walivyoretreat kwa Google. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25.

Muda huo wewe unakaribia 40, lakini unaona isiwe tabu. Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonizer. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua "njuka" wa form one?? Lakini leo anamuita Wema baby?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio "issue" sana. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la "akina bibi wanaolea wajukuu zao"

Lakini hupati "husband material". Unawapata "maplay boy" wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza "umemaliza eddah" wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng'o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la "Jihadhari mbwa mkali" lililokuwa getini anaweka tangazo jipya "tunauza barafu" Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga "plasta" nyumba yenu.

My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata. Usiringe. Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Saidia wengine unapopata nafasi ya kufanya hivyo. Usilipize baya kwa baya. Lakini pia, Usifanye makosa ya "Yahoo".!

Malisa G.. (copy and paste)
 
Kufananisha biashara hasa katika nyanja za Teknolojia maisha yetu ya leo ni kujidanganya.

Mbona hajailaumu google kutaka inunuliwe na Yahoo wakati walikuwa na fursa ya kukua?

Vipi Watsapp wangekuwa na tamaa ya kuuzwa mapema wangezipata Usd. Bilioni 16!!
 
Mwaka 1998 "Google" walitaka
kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo"
kwa dola Milioni 1 (sawa na
Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo
wakakataa. Yani Yahoo wakakataa
kuinunua Google.

mkuu 98 unajua thaman ya sh yetu ilikuwa sh ngap au umepigia kwa sasa
 
kistaarabu ukichukua kazi ya mtu inapaswa ku mwa aknowledge jamaa mhusika kwa kutumia akili yake kuandika alichoandika. wewe ume copy na kuja kupaste na watu wengine wanaweza fikiri ni yako. si vizuri huu ni wizi kama wizi mwingine wowote ule.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom