Epuka makosa yaliyotendwa na " Yahoo"

Epuka makosa yaliyotendwa na " Yahoo"

The Bourne

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
1,077
Reaction score
1,322
Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.
Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.
Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni "ndogo"
Lakini Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG] ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya "mbwa" (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG] ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio "Boss" anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990's lakini kwa sasa imebaki "Skrepa". Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.
Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata "department" ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG] nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Vivyo hivyo katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani.
Usifanye makosa ya Yahoo.!

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG] nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na "Offer" walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa bei ya kuku za kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe "too much". Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama "Yahoo"… una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini "natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana". Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea kama Yahoo. Hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25, wakati wewe una 40.

Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonize. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua form one?? Lakini leo wanaitana mababy?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio issue. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la "akina bibi wanaolea wajukuu zao"

Lakini hupati "husband material". Unawapata "maplay boy" wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza "umemaliza eddah" wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng'o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la "Jihadhari mbwa mkali" lililokuwa getini anaweka tangazo jipya "tunauza barafu" Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga "plasta" nyumba yenu.
My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata.

Usiringe Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Usifanye makosa ya "Yahoo".!
 
Daah. Uzi bora kabisa wa kufungia mwaka. Nanii nakuomba ukishasoma Uzi huu, uje piemu!
 
Ni kuhusu THAMANI, nakumbuka miaka mitatu iliyopita nilihamia nyumba moja Mbezi beach, katika nyumba ile ni mimi tu niliyekuwa sina kipato cha uhakika. Nilikuwa nikitukanwa sana nilipochelewa kulipia bills zinazokuja, tena natukanwa na vijana wenzangu, hawakujua lilikuwa ni swala la muda tu, ilifikia kipindi nikashindwa kulipia kile chumba ikabid nirud nyumban kwanza, Mungu akanibariki nikapata kufungua biashara yangu nikaanza kuifanya ipasavyo mwaka jana, mwaka huu mwezi wa sita mwenye nyumba akanipigia simu akanambia kuna chumba na sebule kama naweza nirud, nikamjibu naweza. Nikarudi, kila mtu alishangaa kuniona nimerudi tena na sasa hivi nina THAMANI mbele ya macho yao.
 
safi kwa ilivyorelate real life situation life event kwa kutumia mfano wa yahoo
 
Ngoja niende church kupunguza dhambi nitakuja kusoma baadae
 
Hahahahahahahajahahah..
Kuna mzee mmoja ana makontena yake,kuna kipindi wachina walimwambia awauzie kila moja kwa zaidi ya milion 15 akakataa ,sasa imefika zama hizi za bwana yule vyuma vimekaza ,sasa anatamani kuaaza hata chini ya milion 10.
 
Mada haina ukweli kuuza kitu kwa sasa wakati bado unakihitaji na kinakuiingizia faida ni kukosa ubunifu ni vema yahooo walivyokataa mwanzoni wakiamini watapambana sokoni kufeli kwaoo kwa baadae ni kukosa ubunifu wa kutosha ila wangeweza kutokuuuza kwa bei zote hizo na bado wangeweza kutengeneza fedha zaidi ya hizo
 
Yani yahoo Na internet explorer kuporomoka bado siamini kabisa. Miaka ya tisini Hadi mid 2000 hizi mbili zilidominate Sana. Yahoo ilikuwa the most visited homepage in the world kwenye internet.

Pia marketing strategies Na ambitious employee s ndio uipaisha kampuni Na bahati vilevile.

Ila Cha ajabu Japan bado yahoo inapendwa Sana kutumiwa Kama sech engine kuliko Google.
 
Mada haina ukweli kuuza kitu kwa sasa wakati bado unakihitaji na kinakuiingizia faida ni kukosa ubunifu ni vema yahooo walivyokataa mwanzoni wakiamini watapambana sokoni kufeli kwaoo kwa baadae ni kukosa ubunifu wa kutosha ila wangeweza kutokuuuza kwa bei zote hizo na bado wangeweza kutengeneza fedha zaidi ya hizo
Nakubaliana Na wewe mkuu. Ubunifu, marketing strategies n.k inqchangia Sana.

Pia CEO anachangia Sana. CEO wa Nokia aliiangusha Sana wakati angekubali ushauri Nokia itumie Android badala ya windows ingekuwa mbali sana. Kuanguka kwa Nokia inasikitisha Sana.
 
Kutangulia siyo kufika mkuu,malengo nayo yananafasi. Muda mzuri sana wa binti kumreme ndiyo huo huo wa kuwa shule. Anaweza kuolewa hata na billionaire,lakini vipi hiyo 40 ikifika,bado atamtaka?nasikia huwa hawazeeki kabisa wanaume.
Cc Mengi
Mugabe.
 
Hii makala ilibidi iwepo kwenye gazeti, kina dada waisome kwa wingi, mm niliwahi kukataliwa kisa sina gari, kwa sasa nina magari 5, yy kaolewa na jamaa hana hata baiskeli. Maisha ni fumbo!
Kuna demu bongo alinidump. Sasa hivi nabeba boks halafu naposti picha zangu fb Na six-packs Yani compliments za kutosha.
 
Ukweli mchungu...
Asante mkuu kwa kutukumbusha ngoja nipunguze maringo kabla jua halijazama [emoji23]
 
Kumbuka, kuna stori nyiiingi sana za a failed investment.
Kumbuka, katika scenario hizo mia moja, kuna moja tu ambayo ili-work.
Namaanisha kuwa kuna kampuni nyingi zilifanya hicho ambacho yahoo haikufanya, yet wali-fail miserably.
Haimaanishi yahoo wangechukua, google ingefika hapo.
Kuna 99℅ of businesses failing every month.

Simply put, kuna lots of variables.
Sucess inatokea pale opportunity ikigongana na skill au potential inapoonekana.
Hivyo basi, its vague and relative.

Kamwe usi-invest based on past circumstances. Just study.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom