Epidemic ya Blogs na Websites Bongo …Nyingi Lakini Ubora ni Zero | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Epidemic ya Blogs na Websites Bongo …Nyingi Lakini Ubora ni Zero

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gem08, Jun 15, 2012.

 1. g

  gem08 Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je, Ni uhaba wa wataalam au ndiyo mazoea ya kupenda vya bure au rushwa!!?
  Tembelea website na blog za Bongo, ziwe za serikali, mashirika makubwa au za watu binafsi utashuhudia mwenyewe ninachokieleza hapa. Page hazina mpangilio (page alignment and inconsistency), hazivutii (matumizi mabaya ya typography, rangi na picha), vigumu kupata unachokitafuta (usability issues), maelezo yasiyoeleweka (no useful content and lack of clarity) na mengine mengi.
  Mfano mzuri ni website ya serikali iliyopewa msukumo mkubwa wa rais wa Marekani Barak Obama iitwayo www.opengov.go.tz. Madhumuni yake yalikuwa kuwashirikisha wananchi katika masuala na shughuli za serikali ili kuhamasisha uwazi (promote transparency). Kama hilo ndio lengo lake, si lazima uwe na degree kufahamu kwamba pamoja na mambo mengine kilichohitajika kwenye website kama hii ni maelezo sahihi (useful content); user interaction kama emails na forms; na muonekano (look) ambavyo vitamshawishi mwananchi kushiriki (encourage public engagement). Kinachonishangaza ni upungufu wa ubora wa website hii kwa vitu basic kabisa ambavyo hata mwanafunzi (junior web developer) angeweza kufanya.
  Orodha ya mifano ya website zenye mapungufu ni ndefu ila ona hizi chache ambazo ungetegemea ziwe angalau afadhali.

  Pamoja na websites, nao wapenda kublog wameongezeka hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la blog na hali hii haioneshi dalili ya kupungua. Hata hivyo ubora wa blog hizo ni wa kusikitisha. Kwa lugha rahisi kabisa ni kwamba ‘zimelipuliwa’ hakuna ujuzi. Wanablog wengi wanatumia free google hosting (yaani .blogspot). Elements zimebandikwa kila upande kwenye page hivyo msomaji anabaki ku-guess wapi pa kwenda. Nyingine hata maandishi hayaonekani.
  Hivi majuzi tu nikiwa kwenye jamii forum kuna msomaji mmoja alikuwa anauliza wasomaji wengine ni wapi anapoweza kupata .com domain ya bure. Mwingine anaulizia internet ya bure. Ni swala la kushangaza kuona jinsi tunavyoitaka teknolojia bure bila kujali ubora.
  Katika kulichambua swala hili nimeona kuna sababu kuu zifuatatzo:

  1. hali ngumu ya kimaisha; (2) kupenda vya bure; (3) rushwa; na (4) upungufu wa wataalam.
  Binafsi nakubaliana kwamba hali ya mtanzania wa kawaida ni ngumu si ajabu ubora wa vitu ni mdogo. Hata hivyo iweje hata makampuni na serikalini bado hakuna ubora? Tatizo ni kwamba tumejenga mazoea ya kupenda vya bure na kutokujali ndiyo sababu inayopelekea hata tunapopata nafasi za uongozi iwe serikalini au kampuni binafsi bado tunajikuta kuchagua urahisi (cheap) na kusahau ubora (sacrifice quality)!
  Swala la rushwa na ubinafsi linachukua nafasi kubwa. Katika uchunguzi wangu nilishtuka baada ya kusikia kiasi cha fedha kilichotumika kutengeneza website ya kampuni moja kulinganisha na ubora wa website hiyo. Ni dhahiri kwamba bajeti iliyoidhinishwa haikutumika ipasavyo. Aidha kampuni ililipa bei ya juu kwa mtu au kampuni iliyotengeneza website hiyo au kuna mtu kabakiza chenji.
  Kuhusu swala la upungufu wa wataalamu sikubaliani nalo. Japokuwa tuko nyuma, kuna vijana wengi wa kitanzania wenye ujuzi na wanaoweza kufanya kazi nzuri. Tuchukulie mfano mzuri wa ‘michuzi’ blog iliyopata mafanikio makubwa. Mmiliki wa blog hii japokuwa anatumia free google service, ni dhahiri anatumia wataalamu wa tecknolojia kumtengenezea blog inayopendeza na kukidhi matakwa ya mtumiaji wakati yeye akitumia muda wake kuweka bidii kwenye fani yake ya ‘uandishi na upigaji picha’ (yaani content). Sio ajabu kwanini anafanikiwa sana.
  Mifano mingine ni hizi website zifuatazo ambazo naamini zimetengenezwa na watanzania:

  Ukweli ni kwamba kuna matatizo ya kiuchumi, cultural na hata uongozi mbaya katika ngazi mbalimbali. Ukichukulia kwamba dunia ya sasa ni ya Internet, matatizo haya yanarudisha nyuma mafanikio ya nchi. Kwa kuwa hakuna physical contact kati ya msomaji na mwandishi, website ni kama kioo cha mwandishi. Hakuna mtu mwenye akili zake anayeweza kuamini kazi yako au kukuchukulia serious kama website yako imelipuliwa.
  Kila mtu ana ujuzi wake. Ni unprofessional kutaka kufanya kila kitu peke yako. Wakati mwingine inabidi kutoa kidogo ili upate zaidi. Si lazima ulipe malaki, kuna watu wenye ujuzi watakaokufanyia kazi nzuri kwa bei nafuu..shop around utawapata.
  Mwisho ni kwa wajuzi na wataalam wa teknolojia. Kumbukeni teknolojia inabadilika kila siku hivyo tuna kila sababu ya kuendelea kujifunza mambo mapya constantly. Baadhi ya software tools nzuri kuzijua kwa maswala ya internet ni :
  For Developers: PHP, Python, Ruby, Javascript, Wordpress, Joomla, CSS, ajax, JQuery, etc.
  For Designers: Graphics - Photoshop, Gimp, CSS, etc.
  Kwa ushauri namna ya kuboresha website au blog wasiliana nasi:
  goody@goodytechnology.co.uk
   
 2. i

  isotope JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kweli hakuna cha bure, nimefurahia hiyo elimu uliyoitoa hapo juu free of charge kabla sijaona hilo tangazo la biashara mwishoni, namaanisha contact!
   
 3. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 784
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 80
  nimekubali strategy yako. Una-identify weakness zilizopo halafu unaitumia kama key success factor.....create opportunity out of crisis.
   
 4. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  somo limeeleweka!
   
 5. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pamoja mkuu,naombeni ushauri kwenye hii blog yangu
  GSHAYO
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu kishatoa email mwisho kazi ni kwako..
   
 7. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa upande wangu naona imetulia spendi blog zenye mazaga zaga mengiiiiiiiiiiiii hii naona ipo poa,muhimu si uzuri wa gari muhimu uimara wake,mada zilizopo humu ni nzuri sana na kila mmoja yupo huru kutoa hoja,au kuchangia.
   
 8. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  asante mkuu na karibu kwa maoni na ushauri kwenye cBox yetu
   
 9. g

  gem08 Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dio website yako ni nzuri ina-meet minimum standard. Main content area ambayo iko center-aligned imekaa kiprofessional na naweza kuongea kwa confidence kabisa kwamba hii sehemu imefanywa na mtu anayejua kazi yake. Matumizi ya rangi ni mazuri (graysh backgroundfor the wrapper which i really like, black font color in a white background which compelements each other very well). Hakuna vitu vingi visivyo na maana which is a good thing.

  Tatizo liko kwenye elements on the left. Hizo widget ziko sawa ila image ni ndogo kuliko saizi ya box. Hii inasababisha nafasi kubaki upande wa kulia especially kwenye matangazo. Images haziko sharp enough na zimelipuliwa. Ukichunguza utagundua hata file size for images ni kubwa which increases loading time.
  Pia just a word of caution, wasomaji wengi wata-ignore elements on the left (hizo zenye matangazo na facebook plugins). Unapokuwa na content muhimu ambazo ungetaka kila msomaji azione hakikisha ziko katikati ya page au upande wa kulia.

  Overall website yako ina sifa zinazotakiwa. Could be better but nikifungua website hii kama msomaji kwa mara ya kwanza nina kila sababu ya kuendelea kusoma articals zilizopo maana it keeps me there unless nina visa na wewe.

  All the best
   
Loading...