EPA yazaa deni jipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EPA yazaa deni jipya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nat867, Sep 1, 2009.

 1. n

  nat867 Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imeandikwa na Joseph Lugendo, HABARI LEO

  Ingawa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefungwa, lakini matatizo yaliyotokana na uendeshaji wake, yameisababishia benki hiyo hasara kubwa ya Sh bilioni 135 na imeitaka Serikali iilipe.

  Serikali kwa upande wake, imekubali kubeba deni hilo, lakini imekiri kushindwa kulilipa kwa mara moja na badala yake imeamua kuanza kulipa deni hilo taratibu huku ikichajiwa riba ya asilimia 8.5 mpaka mwaka 2028.

  Taarifa za kuaminika zilizolifikia 'HabariLeo' hivi karibuni, zilibainisha kuwa benki hiyo imejikuta na hasara hiyo baada ya kulazimika kuwalipa waliokuwa wakidai fedha zao zilizohifadhiwa katika akaunti hiyo kwa vipindi tofauti vilivyokuwa na viwango tofauti vya ubadilishanaji wa fedha za kigeni kati ya mwaka 1985 na Juni 30, mwaka jana.

  Kukiri kwa Serikali kwamba hasara hiyo italipwa, kumeifanya benki hiyo itarajie kujipatia pato litokanalo na riba hiyo la Sh bilioni 10.8 kwa mwaka, ambayo ni tofauti na malipo ya deni hilo.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, BoT imepeleka taarifa kwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, ikimkumbusha kuwa jukumu la uendeshaji wa EPA iliyokuwa NBC, lilikuwa la Serikali na hivyo hasara yake haistahili kubebwa na benki hiyo.

  BoT imemkumbusha Mkulo kuwa mwaka 1985, benki hiyo ilipewa dhamana ya kusimamia akaunti hiyo kwa niaba ya Serikali na hivyo ikalazimika kuihamishia akaunti hiyo kutoka NBC kwenda BoT. Taarifa hiyo ambayo 'HabariLeo' inayo, iliendelea kueleza kuwa akaunti hiyo wakati ikihamishiwa BoT, ilikuwa na Sh bilioni 6.6 tu.

  Ilibainisha kuwa malipo mbalimbali kwa waliokuwa wakidai kwa fedha za kigeni kutoka katika akaunti hiyo, yaliendelea kufanyika kati ya mwaka 1985 hadi Juni 30, mwaka jana wakati ambao akaunti hiyo ilisimamishwa.

  Taarifa hiyo iliendelea kumbainishia Mkulo kuwa katika kipindi hicho, kulikuwa na tofauti za viwango vya ubadilishanaji fedha za kigeni na za Tanzania. Ilikumbusha pia kwamba kwa kuwa malipo yalitolewa kwa fedha za kigeni kwa wadai ambao walikuwa ni wa kigeni, tofauti za viwango vya kubadilishana fedha za kati ya mwaka 1985 na mwaka jana, ziliisababishia benki hiyo hasara ya Sh bilioni 135.

  HabariLeo ilizungumza na Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, ambaye alifafanua kuwa deni hilo limetokana na ucheleweshaji wa malipo ya wadai ambao walipaswa kulipwa kwa fedha za kigeni na mabadiliko ya viwango vya kubadilisha fedha hizo za kigeni.

  Profesa Ndulu alifafanua, kwamba wafanyabiashara wa Tanzania katika miaka ya 1980 walilipa fedha za ndani NBC iliyokuwa ya Serikali na kuruhusiwa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, ambapo NBC ilipaswa kutafuta fedha za kigeni na kulipa waliowauzia Watanzania bidhaa.

  Alibainisha kuwa wakati huo fedha hizo za kigeni zilikuwa zikipatikana BoT na katika benki ya NBC pekee ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Serikali. Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, kutokana na upatikanaji mdogo wa fedha hizo za kigeni, malipo kwa waliowauzia Watanzania bidhaa, yalicheleweshwa huku kiwango cha kubadilisha fedha kikipanda kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu.

  “Kwa mfano, BoT ilipochukua EPA, ilichukua fedha zilizohifadhiwa kwa kiwango cha ubadilishanaji wa Sh 7.14 kwa dola, lakini wakati wa kulipa deni, ililipa kwa kiwango cha Sh 1,000 kwa dola na Serikali ikasema itafidia tofauti,” alisema Ndulu.

  Alibainisha kuwa tofauti ya Sh 7.14 waliyoichukua kutoka NBC na kujikuta ikilipa Sh 1,000 kwa waliokuwa wakiidai NBC, ndiyo hasara waliyoipata. Alisisitiza iwapo Serikali ingekataa kulipa deni hilo, Sh bilioni 69 zilizorejeshwa na wafanyabiashara waliodanganya kuwa sehemu ya wadai, wasingeziruhusu zitumike kwenye kilimo na badala yake wangezitumia kufidia sehemu ya hasara hiyo.
  ............................................

  :confused:My comment: waliofanya kuwepo ucheleweshaji ulipwaji wa deni hilo lazima utakuta bado wanadunda na vyeo vikubwa.... kazi kwelikweli:confused:
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wizi mtupu
   
 3. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hii EPA tangu watu waitolee macho,kila mara tunaletewa habari tofauti tofauti halafu za kutuchanganya,na kuchanganya mpaka inafikia hatua mtu haelewi wakati anapaswa kuelewa/kueleweshwa.
  Hii kitu ina usanii ndani yake tena wa kufa mtu/watu;mbaya zaidi inafikia hatua hadi matumizi yake yabadilishwa,hatimaye kila kiongozi anaongelea anavyojua yeye na ukifanya majumuisho hakuna kauli moja hadi hivi sasa!!??
   
Loading...