Epa, vyombo vya habari na kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Epa, vyombo vya habari na kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Iga, Aug 28, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KWA umoja wao vyombo vya habari Tanzania baada ya kuwa co-opted na wajanjuzi wa Chama twawala waliwaona wagombea ukuu wa chama hicho kuwa ni malaika.

  Miaka miwili na nusu baadaye leo Alhamisi 28 Agosti 2008 vyombo vyote vinamkamia mkuu kutokana na suala la EPA!

  Hata hivyo, mie ninaona jamaa hawa wanashughulikia dalili za ugonjwa na sio chanzo cha gonjwa lenyewe.

  Nina maana kwamba ukiangalia toka huko nyuma iwe suala la NOLAN na miradi ya ajabu; suala la rada mbovu; suala la Benki Kuu; suala la Richmond na masuala mengi mengi tu ya ~ISSUE- za tenda kuna mzizi ambao tunapaswa kuuangalia ili masuala kama haya yasiwe yanajirudia rudia.#

  Kama hamjalijua angalau nishavizindua vyombo vya habari vya nje. Suala lenyewe jamani ni kwa namna gani vyama vyetu vya kisiasa vinajiendesha, vinapata pesa wapi, toka kwa nani, kwa sababu gani, kwa njia gani na kwa malengo yepi.

  Kama vyama vyetu vya siasa vitaendelea kuchota toka hazina au toka Social Security or Pension funds or Health Insurance funds -kila anayechota atadaia ilikuwa ni kwa ajili ya shughuli za chama.

  Hebu basi acheni nyie waandishi kuwa bendera fuata upepo. Fuatilieni au anzisheni ajenda zenye msisimko wa kitaifa na zinazokusuia kubadili nchi kwa kuwa na uongozi mzuri badala ya uongozi mbovu.

  MWANZO wa yote mkumbuke kuwa nyie kama vyombo vya habari mna uwezo mkubwa wa kuwa na mfululizo wa makala na vipindi vinavyoweza kushinikiza serikali kuanzisha mchakato wa KATIBA MPYA. Maana tupende tusipende viraka ndivyo vilivyotufikisha hapa tulipo. Ingawa Kenya walikuwa nyuma sana kwenye masuala ya demokrasia tusishangae baada ya miaka michache wakawa mbele yetu. Na kama tumejifunza kutoka Kenya na kwingineko Afrika muda ukifika wa kuwa na KATIBA MPYA hakuna namna ya kuahirisha mambo. Mkiwaachia hawa jamaa kuahirisha mambo, mwaka njoo, mwaka nenda, hatima yake yote ni kuwa na matatizo sampuli hii yanayojirudia tena na tena.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Vyombo vyahabari vyenyewe vimekuwa so corrupt kiasi kwamba haviaminiki tena!They do their work for the interests of the few and to please other people!
  Shida hapa inakuja pale ambapo wamiliki wa vyombo vya habari wao wenyewe wana manipulate hivi vyombo for their own sake aand interests!Walioko CCM wataisupport na upinzani watafanya hivyo hivyo sasa sijui tutapate strong criticism ila nitaunga mkono upinzani na baadhi ya wabunge wa chama tawala ambao kweli sasa naona wametoka shimoni na wamedhamiria kuuvalia njuga ufisadi kuutokomeza!
  Amen!
   
 3. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2008
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  in brief, kila kingaacho lazima kipoerwe (Chachage). Ulaji upo sana kwenye tenda na miradi yote ya kifisadi. It is highly logical that these are areas most favourable to cater for the insatious desires of the likes of kleptomaniacs, wanaodokoa mboga ya nyumbani ikiwa jikoni etc......
  For example, kuna mambo megine ya ajabu MKATABA wa TRA na ile kampuni ya NECOR....phew!!!! Vogogo wagawana tu revenue za contractor
   
Loading...