EPA hadi Kortini - Kwa nini twashangilia majani na si matunda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EPA hadi Kortini - Kwa nini twashangilia majani na si matunda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Dec 17, 2008.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wanabaraza wenzangu , nimekaa na kutafakuri kwa kina. Nimesoma na kusikiliza wengi humu jamvini. Sasa naomba kuuliza wote wale wanaoshangilia kukamatwa kwa mafisadi, nipeni sababu za msingi za kunifanya name ninyanyue sauti , kalamu na hata key board kuanza kushangilia kufikishwa kwa mafisadi mahakamani. Kwani tumesahahu wahenga wa kale walisema, atushangilii mimba , mpaka mtoto amezaliwa. Vilele atushangilii embe kutoa majani au maua kuashilia mavuno ya embe dodo, kwa kawaida tunashangilia wakati wa mavuno.

  Si unajua tena isije ikawa tukabaki vinywa wazi na yale yale ya ‘mbaazi kukosa maua na kusingizia jua’.

  Narudia tena swali mbona tunashangilia sana majani badala ya matunda? Enzi ya Sokoine tulishangilia kwa sababu justice was seen to be done ….Naomba kuelemishwa.
   
 2. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Yawezekana matunda yakaja bila majani kwanza? Yawezekana twashangalia majani kwa kuwa hata hayo tu yalikuwa hayaoti?

  Yawezekana kama matunda hayatakuja, tutaanzia hatua hiyo hiyo ya kwenye majani kutafuta namna ya kutatua tatizo, kama ni mbegu au hali ya hewa? Yawezekana mafanikio hayawezi kuja kwa hatua moja kubwa kwa mkupuo?

  Tukigundua matunda hayaji, bado tutaendelea kufanya la kufanya ili yaje.
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Una point nzuri na ndio maana watu wengine wanasubiri mwisho wa siku itakuwaje ,itajua kuwa ni kaole ama vp.

  Ila ni hatua iliyotakiwa kupitiwa kwa hawa jamaa kufika kwa pilato.
   
 4. t

  techno New Member

  #4
  Dec 17, 2008
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukurani ya serikali za kiafrika ni mateke. Kwanza utumikie taifa miaka 40 ya maisha yako, ukinunua gari wananchi wanapiga kelele HATA HAWAJALI UMETUMIKIA NCHI KWA MUDA GANI, ukipita barabarani unazomewa kuwa wewe unaiba bila hata ushahidi wa kutosha, ukistaafu unaambiwa uripoti mahakamani kuwa umeitia hasara serikali yako halafu wananchi wanashangilia bila hata ushahidi ama uamuzi wa mahakama.

  Je kwa mtindo huu, nani atatumikia taifa kwa moyo wote? Pili waheshimiwa na mafisadi wa EPA waliorudisha pesa waliyoibIa serikali majina yao HAYATAJWI. KUMBE MWIZI AKIIBA AKARUSHA ALICHOIBA SI MWIZI TENA. Watanzania tuamkeni usingizini. KIKWETE ANAFANYA KIINI MACHO. Mramba, Yona na Mgonja wameitia serikali hasara na wamefikishwa mahakamani. ZHAKIA MEGHJI aliye saini check ya BILIONI 31 akampa ulaji Balali yuko huru na hakuna mashtaka juu yake. Jee? Kati ya Zakhia na (Mramba, Yona na Mgonja) nani katia Hasara kubwa serikali? AU BILIONI 31 NI NDOGO KULIKO BILIONI 11?
  Lowasa na Richmond boys, wako huru na hakuna Mashitaka juu yao. Wametia serikali hasara ya bilioni 170. Wako huru na kukamilisha kiini macho, waliopoteza bilioni 11 wako mahakamani. CCM haikO mahakamani pia lakini watanzania wanashangilia ati mafisadi wako ndani. MTAAMKA KESHO kujua kuwa hiki ni kiini macho.

  Kikwete anawajua marafiki zake waliorudisha billioni 70 za EPA na majina yao hataki yatajwe kwa sababu ni jamaa zake na anakula nao. NA YEYE AKIMALIZA MUDA WAKE TUMFIKISHE MAHAKAMANI. MAJAJI WETU NAO wanatutia aibu. Kesi ya watu watatu ya bilioni 11 dhamana yake ni ya watu watatu. Cha ajabu mtu mmoja anatakiwa atoe nusu ya hiyo pesa kana kwamba nashtakiwa pekee KWENYE KESI TOFAUTI. AU NDIYO KUKOMOANA?

  WATANZANIA TUAMKENI. KIKWETE NI MMOJA WA EPA PIA. MAFISADI WAKO WAPIIIIIIIIIIIIIIIIII.?
   
 5. M

  Mkengeufu Member

  #5
  Dec 17, 2008
  Joined: Dec 16, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Techno ume-hit target mwana! mie nilishaona kuna mchezo fulani unachezwa ili kuwafumba macho (ya akili) walio wengi. Mie pia najiuliza, kashfa ya EPA na hasara ma mabilioni inayotajwa haijatokea kwenye enzi ya JK, imetokea kabla yake, iweje aliwateua wahusika kuwa kwenye cabinet yake? Ni kweli hakujua kuwa they are not clean? i can swear he knew very well-being one of mawaziri waliotumikia kwa muda mrefu! but he still went ahead and appointed them in his cabinet.
  What is happening now (it looks like) ni jitihada za kutuliza kelele za wapinzani.....ninahisi hukumu ya Mramba, Yona na sasa Mgonja zinajulikana tayari, zinasubiri kusomwa tu!!!

  Wakuu hebu nipeni mawazo yenu: Hivi huyu jamaa(JK) kajiandaaje endapo timu ya mafisadi aliowafikisha kwa pilato wataamua "kumwaga mtama"?
   
 6. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tunashangilia kwasababu tumeona some light at the end of the tunnel. Sio mpaka tuone tundu lote, but there is a glimpse of hope. Hope is good. Hope keeps you alive. And we always hope for the best.
   
 7. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  sema jingine
   
 8. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mbalamwezi, asante kwa hiyo tafakuri. Lakini si unajua mti huo waweze kupopoa majani kabla ya matunda ...sijui itakuwaje...na docket za case Tanzania zilivyokaa kiajabu ajabu minimum procesing yaweza kuchukua muda sana mpaka kujua kama matunda yatapatikana.
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  QUOTE=Mbalamwezi;343246]Yawezekana matunda yakaja bila majani kwanza? Yawezekana twashangalia majani kwa kuwa hata hayo tu yalikuwa hayaoti?

  Yawezekana kama matunda hayatakuja, tutaanzia hatua hiyo hiyo ya kwenye majani kutafuta namna ya kutatua tatizo, kama ni mbegu au hali ya hewa? Yawezekana mafanikio hayawezi kuja kwa hatua moja kubwa kwa mkupuo?

  Tukigundua matunda hayaji, bado tutaendelea kufanya la kufanya ili yaje.[/QUOTE]

  Mkuu Mbalamwezi, asante kwa hiyo tafakuri. Lakini si unajua mti huo waweze kupopoa majani kabla ya matunda ...sijui itakuwaje...na docket za case Tanzania zilivyokaa kiajabu ajabu minimum procesing yaweza kuchukua muda sana mpaka kujua kama matunda yatapatikana.
   
 10. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  waenga walisema ukitaka kujua tabia ya mtu, tizama watu wanaomzunguka....nothing to add!
   
Loading...