Enzi zetu zilikuwa bomba sana

Enzi zetu zilikuwa bomba sana

suri

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2012
Posts
404
Reaction score
260
SIJUI KAMA SIKU HIZI YAPO..!? ILIKUWEPO SANA
ENZI ZETU
1. Kung'olewa jino kwa uzi
2. Ubwabwa kupikwa J'pili tu
3. Kidonda kuweka mchanga
4. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
5. Kunyolewa na mkasi
6. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
7. Kwenda kuangalia sinema za Ukimwi na Lishe sokoni
9. Kurewind kanda kwa peni
10. Ndala kuchemshwa ili zisiishe
11. Kucheza umeshikilia kaptula sababu mpira umekatika
12. Kuchonga penseli na meno
13. Kukata ndala, ati ni kifutio
14. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele
ndefu.
15. Kutosinzia kama wamepika wali home..
16. Kucheza kibaba na mama kujipikilisha
Unakumbuka???
 

Attachments

  • 1410025489621.jpg
    1410025489621.jpg
    57.9 KB · Views: 463
namba 10 kiboko,hiyo picha balaa kupika na kifuu maana chenyewe tu kinatoa nishati ya joto na kuisha,
sie tulikua tunawinda ndege na kwenda vua samaki tunakuja pika pika tunang'ata
 
namba 10 kiboko,hiyo picha balaa kupika na kifuu maana chenyewe tu kinatoa nishati ya joto na kuisha,
sie tulikua tunawinda ndege na kwenda vua samaki tunakuja pika pika tunang'ata

Unapikia kifuu at the same time na chenyewe kinashika moto
 
mi namba 12 mpaka leo mtoto akikosa kichongeo meno yanawajbika
 
Umesahau kuoga mapema kwennda kwa jiran kuangalia kidedea, kipindi cha tausi, Fukuto, mambo hayo na kipind cha onyango
 
11: Kukenua meno mstarini ili kukagua wasio piga mswaki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom