Enzi za Mzee MM mwanakijiji-Tujikumbushe !!!

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
875
545
::Madikteta wote duniani hufanana::

Kutoka Maktaba (JF by Mzee Mwanakijiji
11 Feb 2011 ) #UKUTA

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

By Mzee Mwanakijij
Platinum JF Member
Feb 11, 2011
Source JF

My Take : Nini kilimsibu MM mwanakijiji .. Maana huyu wa siku hizi ni tofauti kabisa na yule wa kabla 2012?
 
Attachments

  • IMG_8359.JPG
    IMG_8359.JPG
    4.4 KB · Views: 4

Uzee sasa amesha choka
 
R.I.P Chacha Wangwe hiki kiti hapo pichani kilikuponza. Mwanzoni ulibabaishwa na jina la chama (chama cha demokrasia na maendeleo) ukajua utakuta demokrasia imetamalaki achilia mbali maendeleo, lkn badala yake ikawa kinyume na matarajio yako na ya wengine waliokuwa na mawazo kama yako. Udikteta haukuishia kwako ukaendelea hadi kwa wenzako kina zito waliofahamu kama vile ww ulivyofahamu, bado yule waziri mkuu mstaafu alieambiwa asionje sumu kwa ulimi nk. Toka hapo hakuna mtu kutoka chama husika mwenye uwezo wa kuhoji swala la kiti hicho, na kama yupo ajitokeze tumuone. Huu ndio udikteta tunao usema.

images (25).jpeg
 
Siku hizi Mzee Mwanakijiji ni msukule wa lumumba. Busy kutafuta TEUZI kama mwenzie Pascal Mayalla tangu 2016 lakini hadi hii leo HAJAFANIKIWA 😂😂😂
::Madikteta wote duniani hufanana::

Kutoka Maktaba (JF by Mzee Mwanakijiji
11 Feb 2011 ) #UKUTA

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

By Mzee Mwanakijij
Platinum JF Member
Feb 11, 2011
Source JF

My Take : Nini kilimsibu MM mwanakijiji .. Maana huyu wa siku hizi ni tofauti kabisa na yule wa kabla 2012?
 
Siku hizi Mzee Mwanakijiji ni msukule wa lumumba. Busy kutafuta TEUZI kama mwenzie Pascal Mayalla tangu 2016 lakini hadi hii leo HAJAFANIKIWA 😂😂😂
Kuna wakati aliwekwa kwenye list ya MADC kwa msaada wa Dr Slaa , Mizengo Pinda na Dr Mwakyembe , lakini kuna mnoko mmoja akafukua nyuzi zake za JF ikabidi wamuondoe , wakasema ngoja wamuangalie kwanza kama amerudi kweli au geresha , nadhani ndio maana akaongeza juhudi
 
😂😂😂😂😂😂 Duh! Ama kweli ng’ombe wa mnyonge hazai na akizaa ndama anakufa 😜😜
Noma sana mkuu , unajua Huyu jamaa hakuwa mfuasi wa Chadema , alikuwa mfuasi binafsi wa Dr Slaa ( sitataja sababu Ili kuheshimu maadili ya JF) , kwahiyo baada ya Dr Slaa kununuliwa na ccm kupitia kwa dalali Mwakyembe (kumbuka zile video zilizovuja za kempiski) , ikabidi MM naye ajiunge naye , aliweka uzi humu jf kuhusiana na hilo nadhani bado upo
 
::Madikteta wote duniani hufanana::

Kutoka Maktaba (JF by Mzee Mwanakijiji
11 Feb 2011 ) #UKUTA

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

By Mzee Mwanakijij
Platinum JF Member
Feb 11, 2011
Source JF

My Take : Nini kilimsibu MM mwanakijiji .. Maana huyu wa siku hizi ni tofauti kabisa na yule wa kabla 2012?
Mwendazake ameharibu watu wengi sana
 
No permanent situation.

Muda wake kwenye anga hizo uliisha.
Inaweza ni kwa sababu fulani..ila ikumbukwe hakuna kifo kisichokuwa na sababu.
 
Mwendazake ameharibu watu wengi sana
Chahali hata wewe huwa unachukia sana kukosolewa au mtu kuwa kinyume na maoni yako. Uzuri wako ni kuwa huwa unajaribu kusimamia haki na kukosoa hata pale unayempenda anapovurunda. Hujiondoi ufahamu kama huyu Mwanakikiji au Kigogo. Hawa wawili wapo tayari kutetea ujinga unaofanywa na serikali ili kuwakomoa wale waliokosana nao. Magufuli alifanya fyongo na ukatili mwingi sana lakini Mwanakijiji hakusema chochote kwa sababu tu ''alikosewa'' na aliokuwa anawa-support. Kigogo naye sasa hivi anajifanya kulamba miguu ya watawala kwa sababu tu ''alikosewa'' na aliokuwa anawa-support
 
Uko sawa kabisa Mkuu kule Twitter Republic kapiga block watu wengi sana kisa kumkosoa.
Chahali hata wewe huwa unachukia sana kukosolewa au mtu kuwa kinyume na maoni yako. Uzuri wako ni kuwa huwa unajaribu kusimamia haki na kukosoa hata pale unayempenda anapovurunda. Hujiondoi ufahamu kama huyu Mwanakikiji au Kigogo. Hawa wawili wapo tayari ujinga unaofanywa na serikali ili kuwakomoa wale waliokosana nao. Magufuli alifanya fyongo na ukatili mwingi sana lakini Mwanakijiji hakusema chochote kwa sababu tu ''alikosewa'' na aliokuwa anawa-support. Kigogo naye sasa hivi anajifanya kulamba miguu ya watawala kwa sababu tu ''alikosewa'' na aliokuwa anawa-support
 
Uzee sasa amesha choka
Hapana, nakataa, si uzee. Nadhani tuko wengi tunaomzidi Mzee Mwanakijiji umri. Misimamo yetu toka miaka ya nyuma haijayumba hata siku moja. Toka siku najiunga rasmi JF mwaka 2008 nilisema wazi bila kumung'unya maneno kuwa naamini adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na haijalishi ni nani yuko madarakani, CCM ni ile ile.

Wengine hatukuipenda CCM toka inaasisiwa mwaka 1977 ilipokuwa chama pekee nchini na hatujawahi kuipenda CCM kabla na baada ya ujio wa vyama vingi. Wengine kwa sababu ya huo msimamo wetu tumejikuta tukihusishwa na mara NCCR Mageuzi na mara Chadema. Wanaofanya hivyo wanaamini kutoipenda CCM ni sawa na uhaini.

Hadi leo nasema na narudia, Tanzania haitafanikiwa ikiendelea kukikumbatia hiki chama chakavu ambacho leo hii tofauti yake na mkoloni ni rangi tu. Hivi sasa imefikia hatua ambayo hata vyombo vya dola navyo huwaona wapinzani wa CCM kama wahaini. IGP Sirro anaongoza kitengo cha CCM kilichojivika koti la Jeshi la Polisi, period!

Hapana mgen, Mzee Mwanakijiji hasumbuliwi na uzee, kasalimu amri na kuamua kuungana nao. Sababu zake za ufanya hivyo anazijua yeye mwenyewe, ni siri yake. Alithubutu kumwita Kikwete dikteta, lakini tulipompata dikteta wa kweli kweli, hakuweza kustahimili...huo nao ni ubinadamu! When the going gets tough, only the tough keep going.
 
Sifa zote hapo zimeangukia kwa mwendazake na mamaaa. Siku hizi pesa za serikali zikitoka kwenda kwenye miradi wanaojiramba husema mama katoa kana kwamba ni mali yake. Sioni tofauti ya huyu mama na mwendazake. Tofauti ni jinsia tu.
 
Back
Top Bottom