Enzi za Mwinyi zimeanza kurejea magari ya serikali yamepaki hayana mafuta! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi za Mwinyi zimeanza kurejea magari ya serikali yamepaki hayana mafuta!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dumelambegu, Nov 4, 2011.

 1. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wazee,
  Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka takribani 15 ofisi za serikali zimeanza kukosa hata karatasi za kufanyia printing za barua na documents mbalimbali. Kuna mdau mmoja yupo wizara ya maji anasema magari ya wakurugenzi yamepaki miezi kadhaa kutokana na kukosa hela ya kununua mafuta. Mengine yanadaiwa na DT Dobie, Toyota (T) Ltd, n.k. malipo ya matengenezo tangu mwaka jana. Madereva wanaenda ofisini kupiga stori na kusibiri mishahara mwisho wa mwezi. Watumishi wengi wanaenda likizo bila malipo. Mdau aliendelea kunihabarisha kwamba hata programu ya kitaifa ya maji ni kama imesimama na wafadhili wakiwemo wajerumani, waholanzi, benki ya dunia, n.k. wamepanga kujiondoa kwenye programu.

  Kama habari hizi ni za kweli, basi kikwete nchi imemshinda na kwa dalili hizi tunarudi kulekule alikotutoa mzee mkapa wakati serikali ilikuwa haina fedha hata za kununua karatasi kwa matumizi ya ofisi. Cha ajabu wakati mambo hayo yakiw mabaya hivyo serikalini, wafanyabiashara wakubwa wanaendelea kuporomosha majengo marefu mijini.
   
 2. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Dume,
  Ni kweli kabisa hali ni mbaya kupita maelezo. Binafsi sijawahi kushuhudia hali hii tangu niajiriwe serikalini. Imefika wakati mkurugenzi wetu mmoja anatumia hela yake mfukoni kununua karatasi za kuprintia documents za serikali. Nadhani muda si mrefu nchi itacollapse.
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kingcobra, unataka nchi icollapse mara ngapi!!! Ukweli ni kuwa sasa tunaelekea kwenye kiza kizito. Wengi wetu hatuoni mbele.
   
 4. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60

  Mpaka tutakapokubali kupumuliwa kisogoni!
   
 5. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Halafu hili sharti limetolewa katika wakati mugumu wa nchi yetu na zingine zinazoendela! Nafikiri wameyaona mazingira kuwa yanaruhusu kutoa sharti lolote. Kwa ugumu wa maisha, wasiokuwa wavumilivu lazima wapumuliwe kisogoni mkuu.
   
 6. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kama wamekosa za mtihani kidato cha 2 watapata za mafuta wapo busy na maadhimisho
   
 7. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Hivi za maadhimisho zinatoka wapi? au zinatoka pia mifukoni mwa wakurugenzi, mawaziri na watu binafsi kwenye wizara na idara za serikali?

  Kwa hali hii hii nchi iko mahali pasipo salama hata kidogo na kibaya zaidi ni kuwa hakuna juhudi za uhakika zinazochukuliwa na watawala wa nchi hii zaidi ya kupanda ndege kila siku
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  Wametumia pesa Igunga wakakodi chopa wakagawa pesa kama embe mtini,kuna askari jamaa yangu aliniambia palikuwa na pesa haijawahi kutokea...mbali ya hilo pesa iliyobaki wakanunua jengo USA na zingine wamewapa wezi wa Dowans,sasa pesa itoke wapi tena?
   
 9. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama mambo hayo kweli yanafanyika, basi nchi hii haina 'rais' bali ina 'rahisi'.
   
 10. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  mambo mengi yanakuja..magari yatazimika barabarani bila kusaau kujikausha kuhusu mishahara ya watu.hakika hali itakua mbaya sana.
   
 11. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  brah brah tu! hamna kazi kila siku kulalama hapa, kwani aliyemchagua jk sio nyie? unafiki mtupu. na bado mtalia sana, mwaka wa kwanza tu huo bado minne. watz sisi mdomo sana ila waoga kama kobe. hivi unakumbuka muswada wa ugaidi ulivyopita fasta fasta? ngoja siku si nyingi na muswada wa haki sawa kuruhusu mashoga utapita tu. ngoja hela ziishe. kwani govt si ni bunge? na bunge si ni ccm? ha ha ha haa! majuhaland !
   
 12. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Habari hizi umezichukua kutoka pale viwanja vya biafra, au pale viwanja vya jangwani tujuze chanzo.
   
 13. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180

  kwani mkuu ulitaka wafanyabiashara wafanye nini na unadhani inawahusu hii kitu ya govt kufilisika? Au una ajenda ya siri gani mpaka kufikia kusema hilo?
   
 14. i

  ibange JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tatizo unakariri hujui hata chanzo ni nini. Yeye anasema anafanya serikalini na anayaona sasa chanzo ni yeye unataka chanzo gani tena? Au unadhani chanzo lazima kiwe gazeti?

  Ukweli nchi ipo rehani. Jk alikuta hela za Mkapa akaziponda bila kufanya kazi. Yeye kusafiri tu sasa matokeo ni hayo
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Maadhimisho pia ni kitendawili kwani hata huo uwanja wenyewe wa kuadhimishia miaka 50 ya Uhuru....uwanja wa kihistoria ...ujenzi wake unasua ......na kuna uwezekano mkubwa usikamilike ndani ya muda kwa ajili ya sherehe hizo....ukata.
   
 16. i

  iMind JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Msiwe na wasi wasi wakuu, fedha zipo na maisha yataendelea kama kawaida kama kila mtu ataacha kulalamika na kutimiza wajibu wake.
   
 17. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Alichoambiwa mkuu Dume ni kweli kabisa, hali ya serikali ni mbaya hasa hii Wizara ya Maji,kwani mimi mwenyewe ni muathirika wa miradi hii ya maji,ofc yetu tulifanya kazi ya facilitation, katika baadhi ya wilaya ya mikoa ya kusini toka mwaka 2008/9 ila hadi sasa sehemu kubwa ya malipo hatujapewa..na ukiuulizia unaambiwa WB walishatoa hizo hela,zilipokwenda hatujui..wacha WAJITOE tu..
   
 18. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama hali ndiyo hii kwanini wasiondokane na upuuzi huu wa sherehe ya miaka miaka 50 ya Uhuru
  wa Tanzania bara? Afterall 9/12/1964 hakukuwa na nchi inayoitwa Tanzania bara, hivyo hawajui
  hata wanasherehekea uhuru wa nchi gani? (SIC)
   
 19. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Please read 9/12/1961 not otherwise!
   
 20. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa uswahili wa RAHISI wetu itakuwa vigumu kuacha maadhimisho. Si unajua watu wa pwani wanavyopenda minuso?!
   
Loading...