Enzi za kupimana uwezo zimekwisha??

Enzi za kupimana uwezo zimekwisha??

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,789
Reaction score
7,174
Wana JF Umuhofia kwenu,

Nimeona nililete kwenu hili, siku za nyuma kizazi cha JK, wakina dada walisumbua sana kutupima uwezo kama hakupendi au kabla ya kumpata awe amekupukutisha kila kitu. Lakini mambo kwa sasa yamebadilika, zamani ukimpenda mwanamke siku ya kwanza ni lazima akuijie na watu wawili au mmoja au akuambie mkutane hoteli fulani wakati akijua kuwa ni bei ghali.

Siku hizi baada ya UKATA wanawake wamebadilika hawatuangalii tena kwa kutumia miwani nusu, bali wanakuwa makini kutupeleka sehemu ya kawaida. Pia yupo tayari kushea maongezi hata yeye akachangia kinywaji.

Sababu za kujirekebisha mpaka sasa hazijulikani au ni kwa sababu sasa hivi wanataka kuolewa au wameona mbali kwamba enzi za kuzalishwa na wakurugenzi, wabunge, hata mawaziri wakarisishwa nyumba na gari umekwisha, au wameona mengi jinsi walioachwa kwenye mataa wamekuwa wengi baada ya vibopa kurejea kwenye familia zao na kuachana na michepuko.

Au ni kwa sababu wamechoka kupalamia wazee huku wakiisha muda wao wanakufa mapema wanakuwa wajane, au wamechoshwa na watoto wao kulia kuonyeshwa baba na akionyeshwa tayari ni mzee asiye na sura ya furaha.

Inabidi nimpongeze sana Magufuli ameleta furaha kwa vijana, siku hizi wanasikilizwa, hata vijana waliozaliwa na vibabu sasa hivi hawatakuwepo tena maana walikuwa wanapata tabu akitokea sherehe za kumaliza shule mtoto anashindwa kuoonyesha wenzie kuwa huyu ni baba yake kutokana na mikunjo na hanging valey zilizojaa usoni.
 
KUNA SIKU NILIWEKA HAPA UZI WANGU NIKASEMA HIVI :
"manzi wangu hanipigi kabisa mzinga inakuaje "

MABOYA WAKACHOOONGA....

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
 
KUNA SIKU NILIWEKA HAPA UZI WANGU NIKASEMA HIVI :
"manzi wangu hanipigi kabisa mzinga inakuaje "

MABOYA WAKACHOOONGA....

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
Alafu sijui kwanini hutaki kumtambulisha kwasisi mashemela wake
 
Mi Polis katoka Arusha kunfuta huku Chato,,, huku kipindi kile cha Masemina mengi,,,,Nilikuwa nalipia nauli ya Chato Geita na haji na kuomba zingine,,,Lakini Leo anasema yupo tayari kwa chochote,,, Hata nikisema aache kakazi ka Upolisi,,Jamani Nimeshangaaaaa,, basi mi nimemwambia Miradi yangu naendesha mwenyewe,,,So aendelee tu na kazi,,Alikuwa hajawahi hata niambia Neno''Nakupenda'' but siku hizi mpaka na kifurushi nanunuliwa,,,Wawe wanaachaga,,, mbwembwe!
 
Mada ina umuri wahusika, wengine tunawaza upande wa pili, ada ni bei gani kwa mwaka kwa watoto 3
 
Back
Top Bottom