Enyi Waume Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 Asubuhi!-Bado Nampenda!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,626
Wanabodi,

Kama umejaaliwa kipaji cha kupenda kwa dhati, sio vibaya kuwafundisha na wengine kupenda kwa dhati hivyo kuimarisha ndoa despite all the odds!, hii maana yake hakuna ndoa isiyo na matatizo hata madogo madogo!.

Hivi ninavyoandika hapa, sijalala usiku kucha nikimsubiri wife ambaye ndio kwanza ameingia home akitokea tamasha la Fiesta!.

Najiuliza iweje wife unirudie asubuhi kweupe?!. The simple answer ni kuwa alipaki gari ndani, akataka kuondoka mapema tuu, tangu saa mida ya saa za 7 usiku akashindwa, kisa, alipigwa pini!, hivyo akawa hana jinsi, na baada ya pini kuisha, kuwapitisha mashosti makao ndio hivyo mara kweupe kumekucha!.

Kiukweli kama unapenda kwa dhati, huna sababu ya kuwa na mashaka yoyote ndio kwanza unazidi kufurahi kuwa japo amechelewa, lakini amerudi salama!.

Mwanzo mimi na wife tulikuwa na hobbies zinazofanana, kujirusha kwa sana mwishoni mwa wiki. Laani baada ya kujiunga jf, nikajikuta nimekuwa addicted na KF, hobby yangu kubwa kwa sasa ni jf, hivyo humruhusu wife kuendelea kujirusha na time zake kurudi huwa ni kati ya saa 7, 8 mwisho 9!.

Wiki nzima hii, aliipania sana Fiesta, aliishanunua tiketi zake 3 ya kwake na za ma shostito wake wawili. Wakati anaaga nikamshauri apaki mbali gari, na kwa vile fiesta ya mwaka jana, alipaki mbali, baada ya fiesta ile tuu kwenda alipopaki gari, alikombwa kila kitu, kuanzia simu, pochi, iliyokuwa na kila kitu!, huku watu wakiangalia!. This time ni mimi nikamshauri asivae jewels zozote, abebe pesa tuu ya kutumia, na wala asiondoke na simu!.

Tangu ilipotimu saa 7 usiku nikaanza kusubiria kumfungulia, subiri, subiri na wewe!, saba...nane...tisa ...kumi!. Ni;osikia adhana, nikajua kumekucha!, wasiwasi ukanianza!, nini kimempata?!, simu hana!. Humu jf nako thread iliyokuwa inanikeep busy imefungwa!.
Nikaanza kukasirika na wasiwasi labda kuna jambo baya limetokea!. Sikuwa na jinsi zaidi ya kusubiri tuu, huku nikisali na kuomba kimoyo moyo!.

Hivyo wife ameenda Fiesta bila simu, na ndipo ilipotinga 12 kasoro dakika chache ndipo akatinga home!. Ile kumuona tuu kuwa ni mzima na hana tatizo lolote, nikafurahi na sikumuwazia baya lolote!. Kuaminiana pasipo shaka ni jambo muhimu sana katika mahusiano!.

Huu ni utekelezaji wa mafundisho ya Biblia Takatifu sikumbuki mstari bali imeandikwa "Enyi Wanaume, Wapendeni wake zenu!".

Saa hizi ninapoposti hii, usingizi umegoma jumla huku mwenzangu kajilalia fofofo!.

Ukipenda kwa dhati, unapenda tuu kwa yote!.

Pasco.

Background Story!
Mimi nimeoa nikiwa kijana sana, na nilimuoa my school mate na classmate school sweetheart, na baada tuu ya ndoa tukahamia UK kutafuta maisha, utumwa wa box ukanishinda, nikalazimisha kurudi bongo, baadae tukaenda US, by that time tuna watoto 2, kule mwenzagu ndio alipata scholarship ya miaka 4, mimi ndie niwe house boy, house husband na baby sitter wa watoto wetu wawili!. Kwa vile mimi bongo nilikuwa na kazi yangu, tukakubaliana mimi nirudi na watoto, niendelee na kazi, yeye asome, akimaliza atarejea bongo!. Japo nilimtembelea kila miaka 2, nilimpomtembelea mara ya pili ambapo ndio anamaliza shule, yalinikuta yaliyokukuta!, mwenzagu aligoma kurudi bongo!, nilirudi mwenyewe bongo na kusubiri for 7 good years kuwa atarudi, atarudi, hakurudi!.

Katika kusubiri huko, ubinadamu nao lazima uendelee, (sisi sio malaika), hivyo nililazimika kuwa na "rafiki" tena nakumbuka kuna wakati wakuu wangu wa Jumuiya Ndogo Ndogo, walinilalalimikia, "wewe una ndoa ya Kikatoliki", kwa nini "rafiki" umlete home?!. Nilijibu ni kweli ndoa ipo ila ni kwenye makaratasi tuu, "huyu ni rafiki zaidi ya rafiki"!, kwanza ile kukubali tuu, kuwalea wale watoto wangu wawili wa mwanzo, na kukatokea wawili wengine hapa katikati!, nikajiaminisha wanawake wenye upendo wa hivyo, ni wale tuu walioshushwa kutoka mbinguni!.

Katika kuendeleza "ubinaadamu", shetani naye akaleta majaribu mengine!, nilipata a very bad motor accident, nikawa hospitalized, muhimbili, South Africa na India for six months, wife aligoma kuja, nikawa taken care na huyu "rafiki". Kutokana na lots and lots of anaesthesia nilipata "pseudo invalidity" but she stood by me all this time. Hospitali za wenzetu, mgonjwa unalazwa na anaekuangalia, kila chumba cha private ward kina kitanda na jirani kuna kiti-kitanda, mchana kiti, usiku kitanda!. Huyu "rafiki" alilala kwenye kiti-kitanda for all this time, mpaka niliporuhusiwa!.

Baada ya kurejea home, ndipo wife akataka kurudi!, nadhani baada ya kushauriwa na ndugu zake, na nimerudi kwenye wheelchair, hivyo wakadhani nitakuwa confirmed to wheelchair!. Nilisema no!, japo nilimpenda kupitiliza, kumruhusu wife kurudi, kutakuwa sio kumtendea haki huyu "rafiki" aliyeteseka na mimi all this time!. Nilikubali yale ya mwanzo yaishe, yakaisha, nikafuata taratibu, nikamuoa rasmi "rafiki" na nikamuahidi, chochote atakachotaka within my powers, atapata, kwa pendo letu ni more than everything, tutatenganishwa na kifo tuu!, nothing else!. Hivyo hii incident ya fiesta!, ni kitu kidogo sana!, ukilinganisha na mapito tuliopitia!.
This is a true story.
Pasco
 
Wanabodi,

Kama umejaaliwa kipaji cha kupenda kwa dhati, sio vibaya kuwafundisha na wengine kupenda kwa dhati hivyo kuimarisha ndoa despite all the odds!.

Hivi ninavyoandika hapa, sijalala usiku kucha nikimsubiri wife ambaye ndia kwanza ameingia home akitokea Fiesta!.

Nauliza iweje unirudie asubuhi kweupe?!, simple aswer ni kuwa alipaki gari ndani, akataka kuondoka tangu saa 7 usiku akashindwa, alipigwa pini!.

Huko sio kupenda aisee, ila subiri wenyewe waamke!
 
Mh. Huo ni moyo wa Chuma, mwenzio hata nguo vipimo nampima mwenyewe hakuna
Ruhusa kupimwa na fundi cherehani(nguo) Mwanamke haaminiwi hivyo ndugu ingawa
najua huo ni ujanja wa kutaka kupata ushauri wa kumporomoshea kipigo mkeo Pole
sana mkuu, najua saa hizi umefura kwelikweli.
 
Pole kwa kupenda kiasi hicho. Kumbe watu wa aina yako bado wapo?

Tumeambiwa tuwapende wake zetu ila tuishi nao kwa akili, mke anirudie sa12 asubuhi, anatoka wapi...? Anyway, kwa vile wote mna/mlikuwa na hobby ya kutoka wikiendi labda ndio maana umemuelewa.
 
Msipende kuhukumu moja kwa moja kuwa ni kicheche kuna watu wana hobby ya namna hiyo lakini hata huo ukicheche hana Pasco hongera kwa kumpenda mkeo na endelea kumpenda ila mpe mipaka kwa kuwa yeye ni mama wa familia na kama mmejaliwa watoto anatakiwa atoe taswira nzuri katika makuzi ya watoto siyo kwa namna aifanyayo yeye.
 
Last edited by a moderator:
Hahaahaa nimecheka sana,

Sijui ni mtazamo wangu tu ama?

Mkuu kimsingi mnatakiwa mbadilike sana na haraka katika ndoa yenu,

Athari za matendo ya mkeo ni kubwa sana, vivyo hivyo athari za matendo yako kuwa bize na jf bila kuwa bize na mkeo ni kubwa sana,

Muombe sana Mungu wako awabadilishe tabia zenu
 
hapo lazima kile kitu cha vinunduvinundu cha banana cha mdhamini wa fiesta kilihusika!eti bby wako asiombe hata simu kwa rafiki yke akubeep au namba yako haijui?wanakugongea wewe

...umeongea kwa akili kuliko watu wooote hapo juu, eti hata kuomba cm ya shost zake ampe taarifa mme hakuna, yan hata m2 yoyote pale fiesta eti hamna.... Mm kwa akili yangu ya kitoto toto nahis pasco aliwah kutenda jambo baya kwa mke au m2 mwingine au alikuwa mtenda maovu sanaaa ikafikia stage akaapa kutoyatenda/mtendea tena na kuamua kuwa mpole kama alivyo sasa....ninachokiona unachokifanya sio upendo tena bali ni kumpoteza huyo mkeo, ww na watoto wenu kama mnao! Haiwezekan mtt afanye makosa, achele kurud hom, anywe pombe, hajal hom na ww unamwangalia kisa upendo vivyo hivyo kwa mkeo....usiharibu wanaume wenzako hapa kupoteza ndoa zao kwa upendo ambao hata hiyo biblia unayoisema haujaandikwa.
 
Back
Top Bottom