Enyi wanaaume!! ndoa na ngumi wapi na wapi??

Binafsi nalaani mapigo baina ya wanandoa, siyo wanaume tu kuwapiga wake zao, hata wanawake kuwapiga waume zao. Muda si mrefu uliopita kule Ruvuma wanaume wengi sana wamepoteza maisha kupitia mikono ya wake zao. Wanandoa wanaokusanya michango yetu mingi wakati wa maandalizi ya harusi zao hatutarajii wapigane kwa sababu yoyote ile. Fimbo ni maalum kwa watoto, watu ambao akili yao haijakomaa kuweza kuelekezwa na kufuata lililo jema, sasa mwanamke au mwanaume mtu mzima anapopigwa maana yake ni kwamba abadilike au hawezi kuelekezwa au ni kumaliza hasira za mpigaji?

Wanandoa kama wana hasira wapelekane kitandani wakamalizane pale kwenye 6''X6'' hiyo ndiyo halali yao. Mambo ya kupigana ni ya kishamba mno na ni dalili ya kuishiwa hoja na hatimaye kauamua kutumia nguvu.


Na ndivo walivyo wala hawana sababu ya msingi na hawakubali makosa yao!! Hao wapigwaji nao wana kazi aisee, mi hujanifanyia kitu cha hivo nikakuchekea chekea!!! Hivi hawaonagi hata stuli humo ndani na wao wakawatwanga nazo??
 
Mkuu inakuwaje hao wake za watu wanakuja kukuhadisia wewe mambo yao ya ndani ya ndoa zao? Hayo mambo yanahasiwaga saluni...
 
Back
Top Bottom