Enyi wanaaume!! ndoa na ngumi wapi na wapi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enyi wanaaume!! ndoa na ngumi wapi na wapi??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kiteitei, Oct 30, 2011.

 1. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,253
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  aaaaaghrr!! niko na ka hangover ka jana, nimejipumzisha nikiwaza na kuwazua jinsi ya kureplace pesa niliyotumia jana bila mpangilio maalumu, mlangoni ngo ngo ngo, nauliza nani, naitwa jina......., ni mimi mama ....., natoka nje namkuta mke wa jirani yangu, uso umemvimba kichwani kavaaa kofia kuubwa,namuuliza kulikoni, nikahisi kapigwa nondo (niko mkoa ule almaarufu kwa nondo), naye akaniulza kwani jana hukuyasikia? nikajibu hapana... basii mdada wa watu kaanza kumwaga ya moyoni jinsi alivyopewa kichapo na mumewe wanayeishi naye miaka miwili sasa wakiwa na mtoto mmoja! mdada wa watu ameshaichukulia hali hii kama ni kawaida na ndio maisha yake ya kila siku!nimejaribu kumuhoji sababu eti kosa ni kuwa alikuwa anafua usiku! kama siku mbili hivi maji yalikuwa yamekatika!,namuuliza vipi hali hii umeshawahi kujadiliana au kulifikisha hata kwa wakubwa zenu! kajibu..yaani kwao wote wako hivyo, katikati ya maongezi anakuja mke mwenzie(mke wa shemeji yake) naye kavimba kama katiwa hamira..yeye anadai kapewa kibano juzi!!nawauliza washawahi kulifikisha mbele ya sheria, wote wanadai hapana na wanaogopa, wote wana mambo yanayofanana, jirani yangu alipewa mimba mwaka juzi akiwa form four na hakumaliza shule ikabidi aolewe, mzazi wake mmoja alishafariki na aliyebaki hana uwezo, mwenzie naye hakumaliza o level,wazazi wake wote wamefariki na hana ndugu mwenye uwezo,wote hawana kazi;hivyo waanajiona kama hawana msaada ila kilichobaki ni kuvumilia tu kipigo, nina incident nyingine inaendana na hii nikiwa dar last week.. why why sie wanaume tunawageuza ma punching bags hawa viumbe! kila mtu ana makosa but sidhani kama kipigo ndio suluhisho,niwashaurije hawa, ahh ngoja kwanza nitoke nikatafute supu washaniharibia siku hawa.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  ndio mapenzi hayo. Nalog off
   
 3. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ngumi NO. Labda kama ni DOA au NDOANO na sio NDOA
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,119
  Trophy Points: 280
  Bwana ana pengo, jichoni ana mshono, ngeo mwili mzima, unatarajia nini? Dudubaya
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  napita tu
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni aina mojawapo ya kuonyesha real love kwa baadhi ya makabila.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mapenzi ya mbwa hayo...mpaka wang'atane ndo wapeane vitu!
  Waacheni wa-enjoy mapenzi yao.
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmh! jamani mapenzi gani hayo yakupigana ndio akujue kua wewe mwanamme au sababu unamletea ugali? wanaume namna hii ukiwakuta nje na vimada wanapigwa makofi na hawasema kwamkewe ndio anajitia mwanamme,hawajua kama mwanamke hapigwi kwa fimbo wala ngumi,anapigwa kwa ulimi...
   
 9. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  we nawe usirudi tena humu kila wakati unalog off maana nakitafuta ile mbaya,
   
 10. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wengine bila kipigo siku haiendi
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  hao wanawake wanakosa uthubutu! Ugali unawaponza!
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kumbe utamaduni wa kuwatandika wanawake bado upo! Kweli Beijing haijafanya kazi kabisa!
  Wanaume wengine wasipopiga jogoo hawiki. atamtandika mwanamke weeeeee mpaka asikie mwanamke analia ndiyo anapata hamu ya kufanya mapenzi! Mkoa wa baba wa taifa unaongoza kwa hii practice!
   
 13. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Nipo mkuu. Nalog off
   
 14. T

  Tewe JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60

  Hahahaaaa!!!!! unafa kuwa mtafiti wa mambo ya mapenzi
   
 15. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mboga bila chumvi si mboga!
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Hii ya leo kali...mbwa kumbe hakuna access mpaka wang'atane kwanza!
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ndoa bila kipigo inawezekana
   
 18. k

  kisukari JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  ki ukweli m.me anaepiga ni mbaya mno.inasikitisha,na kama hao,hawana mtaji wowote ule,inabidi waishi nao hivyo hivyo.bora na wao,wanachukue lessons za siri siri,akikupiga kibao,na wewe unarusha ngumi ya nguvu.lakini hayo hayatokuwa maisha mazuri
   
 19. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wanaopigwa wasipopigwa wanaongea haooo!! Ooohoooo, nendeni mitaa ya bugarika mwanza utasikia kila siku usiku mtu anaangua kilio, ikifika asubuhi watu wanacheka na ngeo. Si tulishazoea hizo kesi. Dirishani kwangu ni mwenyekiti wa mtaa wangu, kila saa 9 hadi 10 usiku utasikia kesi zikisikilizwa namimi najaribu kuchungulia kunani, huwa nawaona tu! nikikutana nao mitaani nacheka na kuwapa pole.
  Ndo life style na tamaduni za kiafrica!! Sema mzungu anataka tumuige kila kitu! which is impossible.
   
 20. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Binafsi nalaani mapigo baina ya wanandoa, siyo wanaume tu kuwapiga wake zao, hata wanawake kuwapiga waume zao. Muda si mrefu uliopita kule Ruvuma wanaume wengi sana wamepoteza maisha kupitia mikono ya wake zao. Wanandoa wanaokusanya michango yetu mingi wakati wa maandalizi ya harusi zao hatutarajii wapigane kwa sababu yoyote ile. Fimbo ni maalum kwa watoto, watu ambao akili yao haijakomaa kuweza kuelekezwa na kufuata lililo jema, sasa mwanamke au mwanaume mtu mzima anapopigwa maana yake ni kwamba abadilike au hawezi kuelekezwa au ni kumaliza hasira za mpigaji?

  Wanandoa kama wana hasira wapelekane kitandani wakamalizane pale kwenye 6''X6'' hiyo ndiyo halali yao. Mambo ya kupigana ni ya kishamba mno na ni dalili ya kuishiwa hoja na hatimaye kauamua kutumia nguvu.
   
Loading...