English - vijana changamkeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

English - vijana changamkeni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MJIMPYA, Jun 16, 2012.

 1. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ni ukweli kuwa sasa english imekuwa lugha ya dunia,
  ni bahati mbaya tumejifariji na kiswahili na kushindwa kuwapa watoto wetu helimu nzuri hasa uwezo wa kuongea english kwa ujasiri kama kiswahili.

  Nimefuatilia mtandaoni nikakuta China na maendeleo yao yote wanatenga fedha nyingi sana kuhakikisha watu wao wanajua english sawasawa, kuna vyuo vikuu vingi tu China vinatoa elimu kwa english na wamefungua milango kujichanganya na mataifa mengine ili kuhakikisha english inapewa kipaumbele.
  Nchi kubwa kama Germany, Uholanzi n.k watu wao pamoja na kujua lugha zao wanajitaidi kujua na kuongea English, Italy nao hivyo hivo.
  Uswiss nao wanazidi kujikita kwenye english pamoja na kuwa nchi tajiri na lugha zao za kitaifa.
  Rwanda nao wameanza kiingereza juzijuzi ila wanahakikisha watu wanakiongea vizuri

  Inasikitisha kuona nchi yetu ambapo English ni lugha ya taifa watu hawawezi kuongea kwa ujasiri hata wasomi wetu. Leo nimemwona Dr. Nchimbi mazishi ya Saitot akisoma hotuba ya english kwa hofu sana.
  Yule mama wa Mbeya kwenye uchaguzi wa wabunge EA alipoona english aliingiwa na hofu akaamua kujito. Na wabunge wetu wengi ikitolewa agizo kuwa sasa tutumie english bungeni, wengi watakuwa mabubu.

  Tuache kujifariji English haikwepeki sasa, nawashauri vijana hakikisheni unajua english ya kuongea kwa ujasiri, jipe mazoezi, kubali kukosea ili ujifunze.
  Tunakoelekea soko linazidi kubana, ukiweza kuongea vizuri english kwa ujasiri ni mtaji wako mkubwa

  Nawatakia heri na narudia tena English ni muhimu sana kwa sasa na wakati ulio mbele yetu, hakikisha unaweza kuongea english kwa ujasiri.

  Nimeandika kwa kiswahili ili wengi waweze kusoma make wengine akiona makala ya kiingereza hata hasomi.
   
 2. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Mtoa labda nianze kwa kukuuliza baada ya wewe kufahamu/kujua English ni muhimu we umechukua hatua gani? au wewe mwenzetu unajua English? HILI SUALA SI LA KUIACHIA SERIKALI na ninakuhakikishia hata siku 1 serikali hii hitatenga senti hata 1 kuleta mwalimu wa KIINGEREZA kama wanavyofanya SAUDI ARABIA,RWANDA, EGYPT......watu tumekuwa wabinafsi kuanzia pale UDSM/TATAKI watu wamekalia kujishibisha wenyewe (hasa Dr. Aldin Mutembei-Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili(UDSM) ati anapigia pande lugha ya kujifunzia iwe kiswahili toka chekechea mpaka chuo kikuu. ANATUTAKIA MEMA VIJANA WA TANZANIA kwenye karne hii ya ushindani? au anasema hivyo ili aandike vitabu auze, na machapisho ya kupanda cheo tu? Angalia aibu ya Dkt. Nchimbi kwenye mazishi ya SAITOTI hapo alikuwa anasoma jasho linamtoka mpaka kwenye ulimi, angekuwa anapiga kavu si ndo angedondoka? Bora hata angeenda Mheshimiwa Samwel Sitta (Rais ajaye wa Tanzania 2015-2020 na 2020-2025).
   
 3. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,302
  Likes Received: 8,397
  Trophy Points: 280
  this is one of the reason why most kenyans with all their internal problems underrate tanzanians-kizungu.
   
 4. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kiukweli Kiswahili kiko nyuma sana kimisamiati hasa katika suala la masoma hasa kwa wanafunzi wa masomo ya science litakua tatizo kubwa Mno. Me nashauri bora kiingereza kifundishwe kuanzia ngazi yachekechea ili kumuwezesha mwanafunzi kuwa na uelewa zaidi pale atakapo endelea juu, Nimeshuhudia wanafunzi wengi wa kidato cha kwanza wanapata shida kunasa kiingereza kwasababu hawana msingi nacho toka awali. Kama kiingereza kikitumika kama lugha ya kufundishia kuanzuia mwanzo wa elimu ya watanzania Tuya pata wanafunzi wenye uwezo na uelewa wa mambo mengi. HATA SERIKALI IPINDISHAJE MAELEZO KIINGELEZA ITABAKI KUA LUGHA STAILI KUFUNDISHIA NA HAIEPUKIKI.
   
 5. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Hiviiii..basi ulaya wote wangekua wasomi
  vox populi,vox dei
   
 6. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Sijakupata mkuu
   
 7. A

  ADK JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,159
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Tuongee yote lkn ukwel utabaki kuwa waliotumia lugha zao wametuacha sana angalia india ,china ,japan n.k
   
 8. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  MJIMPYA

  Thank you very much for putting weight to my mission of being here on JF. I've been learning through mistakes which are vividly progressive. People are not yet aware of the fact that they can make effective use of time and other resources they spend here online to gain life skills. Most do concentrate into gossiping and blackmailing. Lets change...whether you like or hate, English is there to stay as the key to global doors of opportunities and prosperity.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Well said.Tutazunguka hapa na pale. Tutasema hili na lile lakini ukweli utabaki hapo kwenye blue.
  Hivi fikiria wewe ni contractor mdogo tu, unapata kazi ya kujenga mradi flani. Ukiangalia Document zote zimandaliwa kwa Kiingeleza na serikali injua hiyo. Sasa iether uajili mtu wa kufasili hicho kilicho andikwa au ujifunze lugha hiyo ili upunguze gharama. Lakini pia katika soko la kimataifa Lugha ya Kiinngereza inachukua nafasi kubwa. Na ndo maana wapo wachina ambao kazi yao kubwa ni kutafsri lugha zilizopo kwenye makablasha ya kazi. Labda ndo maana serikali yao inweka jitihada za kuhakikisha watu wake wanajua hiyo Lugha kwa ufasaha.

  Kila siku bungeni wanapiga kelele matumizi ya kiswahili lakini angalia utekelezaji wake, ni kingereza tu kinachotawala kwenye makablasha yao. Angalia sera na sheria zinazotungwa, zipo kwa Kiingereza. Hata mswaada wa marekebisho ya katiba ulitungwa kwa Kiingereza na kufasiliwa kwa kiswahili. Hii inamaana kwamba kukitokea utata wowote lugha lugha lugha mama itatumika kiingereza.
  Sisemi tuache kabisa Kiswahili, la hasha tukijue sana na kwa undani lakini pia tujifunze kiingereza kama tunavyojifunza Kiswahili. Hiyo ndio lugha ya Jangwani. Vinginevyo mtu ambaye hataki kujua ajiandae kula majani ya chini kama mbuzi huku twiga akibaki na uwezo wa kula majani katika miti anayotaka hata ile ya chini inayofikiwa na mbuzi pia.
  Wale wanaomba kazi kubwa kubwa za miradi mikubwa mikubwa watakuwa mashahidi Lugha inayotumika kuandaa makablasha ni Kiinereza tu.
  Wala serikali haina ubavu wa kuagiza ziandaliwe kwa Kiswahili maana wafadhli wenyewe kama Benki ya Dunia na wengine wanataka sharti la kwanza Lugha ya kazi iwe Kiingereza. Sasa unadhani kwa kujua Kiswahili tu itatufanye tupate hizo kazi au tupate kwa kuajili wale wanao jua ili watusaidie. Kama ndivyo kwanini tusiweke msisitizo wa kujua wenyewe.

  Nachukia sana wanasiasa wanaopotosha umma eti tutumie Kiswahili tu, na mitahala yetu iwe ya kiswahili wakati wanajua fika kuwa watoto wao wapo English medium School. Na hao ndo wanashika nafasi nzuri kwa sabubu tu ya uwezo wa kujieleza vizuri kwa kiingereza na si kwamba wana akili sana kuliko wale wanaojua kiswahili.

  Nenda kwenye bodi yoyote ya proffesional yoyote utakuta report zao zipo kwa Kiingereza. Angalia utaratibu wao wa kujisajili huko, wanahitaji nini? Viandaliwe kwa lugha gani? Kwanini wakati Lugha ya Taifa ni Kiswahili!!
   
 10. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Like two weeks we had to recruit drivers for the new project (its a gov inst.), only those who could speek good english made it through. Imagine this is happening in a Gov inst. and ironically at this very cadre!
   
 11. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ndg ok hata kama unadhani lugha zao zimewasaidia fine, tunachosema sisi bado uchumi wetu ni mdogo na lazima tutumie siraha zote ili tuweze kutoka, ndo maana tunasema vijana wajue english hata wale wa chini kabisa. Tunategemea wawekezaji na ajira zao, so lazima tujue english la sivyo kazi hata za mahotelini tutaendelea kunyimwa english hatujui!
   
Loading...