Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Habari Wana JF..
Imekuwa kawaida kwa watanzania tulio wengi kukatishana tamaa juu ya matumizi ya lugha za kigeni hususani kiingereza.
Aidha,ni mara kadhaa nimeona mtu uki-post kitu kwa kiingereza na kikawa na makosa ya kiunadishi ama kisemantikia au hata kisintakisia basi watu lao ni moja tu;
"Si ungeandika tu kwa kiswahili".
Hata hivyo,binafsi kama mdau wa somo la kiingereza naamini lugha ina skills nne ili mtu uonekane anaimudu.
1.kuandika
2.kusoma
3.kuskiliza na
4.kuongea
Skills zote hizi unaweza kujifunza,na tendo la kujifunza ni endelevu;haliishi.Na ili ujifunze vizuri, inahimizwa kuongea hadharani(kufanya mazoezi mara kwa mara) na hata kuandika pia ili kujijengea ujasiri wa kuongea.
Ikiwezekana watu(wanaojua) wakukosowe pale unapotokea kutengeneza makosa.naamini mwl. mzuri hamzomei mwanafunzi anaethubutu kujifunza badala yake anamtia moyo.
Lakini sisi tumekuwa tukikatishana tamaa na matokeo yake watu wanaogopa kuandika au hata kuendesha mijadala ya kujijengea ujasri wa kuongea lugha hii.
Kama ni makosa hata kwa kiswahili tunayo pia tena mengi tu.
Ndiyo maana sio kila mtu anauwezo wa kuandika vizuri hata kwa kiswahili tu.kumbe tuache tabia ya kukatishana tamaa,badala yake tutiane moyo .
kukodimiksi na kukodiswichi inaruhusiwa kiuandishi na kimaongezi pia, inategemea na aina ya hadhira.
Hali Hii inapelekea Tanzania kuwa taifa lenye uwezo mdogo sana kwenye lugha hii; ambayo binafsi naamini ni miongoni mwa lugha muhimu kutokana na sababu za kiuchumi,kisayansi,kisiasa na hata kiutamaduni nk.
Hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania haijaumbwa yenyewe jangwani au kisiwani bali ina muingiliano na mataifa mengine...