England yaishutumu Urusi kwa udukuzi Duniani

England yaishutumu Urusi kwa udukuzi Duniani

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,355
Reaction score
16,408
Uingereza yaishutumu Urusi kwa udukuzi

Maafisa wa Uingereza wamesema kuwa idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi, GRU inahusika na mfululizo wa mashambulizi mapya ya mitandaoni duniani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Jeremy Hunt amesema leo kuwa idara ya GRU inahusika kwa mashambulizi hatari dhidi ya taasisi za kisiasa, biashara, vyombo vya habari pamoja na michezo. Shirika linalohusika na mitandao nchini Uingereza limehitimisha kwamba wadukuzi wanaohusika na mashambulizi kadhaa wamegunduliwa kama wafanyakazi wa GRU. Shirika hilo limesema mashambulizi mapya manne yanahusishwa na GRU pamoja na mashambulizi mengine ya awali. Kwa mujibu wa shirika hilo, mashambulizi dhidi ya shirika la kudhibiti dawa za kuongeza nguvu michezoni, mfumo wa usafiri wa Ukraine, kampeni za uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2016 na mengine bila shaka ni kazi ya GRU.
@kokuyo Frank wanjiru Tujitegemee Struggleman Hammaz Aretasludovick Malcomlumumba

Dw
 
Hata hivyo Uingereza hana nguvu dhidi ya kamanda Putin
 
Ndio maana mrusi humdanganyi chochote maana anakuwa ameshakufuatilia vya kutosha na taarifa zako anazo za kutosha
Na wenyewe wanajua propaganda kuhusu Urussi hazimtishi Mrusi....ila ni kwa ajili ya kutuburuza sisi wa ulimwengu wa tatu...tusioujua mchezo kiundani...

Rejea lile tukio la yule jasusi aliechomwa sindano ya sumu uingereza.....pamoja na mbwembwe zote za Mwingereza na mwenzake USA....Mrusi alijibu tu sihusiki ......Kama vipi tuunde timu ya wachunguzi toka pande zote mbili iliyo huru .....Mpaka leo Mwingereza kimya.

Hawa wamagharibi wanatuhadaa sana wanadunia...
 
Pia naona anaifuatilia sana Ukraine
Pia shirika la kudhibiti dawa za kuongeza nguvu michezoni bila shaka kuna taarifa anazihitaji za siri zilizofichwa
 
Back
Top Bottom