Engineers from dit,must are mostly professionally than udsm?

Engineers from dit,must are mostly professionally than udsm?

udsm wanatoa Bachelor of Science in engineering, wakati DIT ni bachelor of engineering. udsm ni designers, dit ni watendaji technicians. huwezi kuwalinganisha maana kazi zao ni tofauti.

UDSM wanafundishwa kutumia formwork wakati DIT wanafundishwa kutengeneza formwork. Msanifu na fundi mchundo ni watu 2 tofauti
 
Alie vizur kimatendo ndie anaehitajika......hayatohitajika madaftar katika ufanisi ila ni matendo tu......so DIT is the best for everything
 
Engineer mzuri anaweza kutoka mahala popote pale ama chuo chochote kile..
UDSM ni wazuri katika maswala ya IT na Electrical
DIT ni wazuri Mechanical na Civil and Building
Must ni wazuri kwenye Archtecture
NIT ni wazuri kwenye Automobile
St. Joseph ni wazuri kwenye IT

all in all juhudi binafsi ya mtu ndio inaweza kumfanya bora zaidi na sio chuo
 
Engineer mzuri anaweza kutoka mahala popote pale ama chuo chochote kile..
UDSM ni wazuri katika maswala ya IT na Electrical
DIT ni wazuri Mechanical na Civil and Building
Must ni wazuri kwenye Archtecture
NIT ni wazuri kwenye Automobile
St. Joseph ni wazuri kwenye IT

all in all juhudi binafsi ya mtu ndio inaweza kumfanya bora zaidi na sio chuo

MUST ni wazuri kwenye architecture??..unapajua ardhi wewe au umrkariri..ulizia top architect wa hapa mjini kina lazaro,dr mosha nk wametokea wap na ulizia best young architect wa east africa mshindi wake ametoka wap?ulizia caleb kimaro kamaliza ardhi mwaka 2011 amefanya nini katika hilo shindano la vyuo vyote vya east africa..ardhi usipime pale ni noma
 
Ok nimekupata. Una mengine ya kusema?

MUST ni wazuri kwenye architecture??..unapajua ardhi wewe au umrkariri..ulizia top architect wa hapa mjini kina lazaro,dr mosha nk wametokea wap na ulizia best young architect wa east africa mshindi wake ametoka wap?ulizia caleb kimaro kamaliza ardhi mwaka 2011 amefanya nini katika hilo shindano la vyuo vyote vya east africa..ardhi usipime pale ni noma
 
Huu ni mfano mmoja mzuri wa tofauti ya product hizo mbili alizouliza mwanzisha uzi. BSc. Inaandaa Researchers, inventors, analysts na wafananao na hao ambao msingi wake mkubwa ni ANALYSIS. Baadaye huja kuwa Managers, Policy makers, Think tank n.k wa taifa lolote. BEng. inaandaa direct supervisor kwenye maeneo ya uzalishaji, ujenzi n.k ambazo msingi wake mkubwa ni hands-on knowledge. Udhaifu mmoja wa kundi la kwanza ni kuwa huwa ni ngumu sana ku-cross kufanya kazi za wale wa kundi la pili wakati hawa wa kundi la pili wakipata mafunzo kidogo tu ya ziada na wakichanganya na sharpness na analytical mind ya kuzaliwa huweza ku-fit vizuri kabisa kwenye kundi la kwanza. mfano ni watu kama Prof Luhanga, Prof Mwandosya n.k Udhaifu wa kundi la pili ni ukosefu wa uwezo wa kuinvolve analysis kwenye problem solving ambao hupelekea kuwa wazuri tu kwenye low to mid-levels za technology na kupwaya kwenye viwango vya juu zaidi. Nina mifano ya watanzania wengi product za BSc wanaoexcel kwenye Technology Giants ulimwenguni huko mbele lakini hawa wengine huishia humuhumu ndani tu. Udhaifu wa post hii ni mfano wa tu wa kiwango cha analysis....no offence intended
Acheni mambo nyie! UDSM wako vizuri kwenye madaftari lakini kiutendaji ni---niii mlenda ! DIT wako vizuri sana kwenye utendaji than UDSM! UDSM ukiwaambia 4X4 wanajua ni 16 lakini ukiwaambia jinsi 16 ilivyopatikana patachimbika ilan DIT watakuambia ni 16 na jinsi hiyo 16 ilivyopatikana ! nimefanya field na watu wa degree wa UDSM kipindi mm nikiwa Diploma DIT at the same field lakini UDSM ikaonekana kama walikuwa mzigo sana! UDSM ni jina tu limewazidi ukubwa lakini wengi wao ni akina ACHIBA!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nimesoma FTC mbeya tech, BEng. DIT, Masters UDSM acheni kudanganyana DIT jina linawabeba hamna kitu wamejaa kelele
 
Kunguni utawajua tu..DIT jina linawabeba?acha ujinga...DIT ya ukwel!
 
Inanikumbusha debate za O level zamani!!!!!!! - Mother is better than Father!
 
Inanikumbusha debate za O level zamani!!!!!!! - Mother is better than Father!
 
Tehe tehe Hamis77, eti wa UD ndiyo wanawasimamia wa DIT&MUST! Ni upogo wa hali ya juu. Nakumbuka enzi zile nikisoma pale DIT nilifaulu vizur O-Level kule Tech school, ila form6 haikuwa first choice nilipenda kusomea ujuzi siyo kukariri tena physics(sisi kule tech sec tukiita Engineering Science) ambayo ni full calculations. Kwa mfano kwa mitaala ya wakati ule, topic kama angular motion, projectile motion, magnetomotive forces(mmf-siyo ile emf ya physics) na mashines tulizisoma secondary, wakati wenzetu wa shule zisizo za ufundi walizikuta kidato cha tano. Kwa hiyo watu wengi tuliotoka tech sec schools mimi nikiwemo na wenzangu wengi tu kutoka Moshi Tech, Tanga Tech, Ifunda,Iyunga na Musoma Tech, tena wengi ni division I za points7 hadi div II. za points 18 tulikutana pale DIT tena ni PCM wote. So baadae wengi walibaki DIT kuchukua ADE na sasa ni BEng ambayo nami nilichukua hiyo na pia kusajiliwa kama Prof Eng na ERB. Bahati ni kwamba wale tuliotoka tech sec school tumekutana kwny game hata za structural design na kwa kweli tunategemeana sana tofauti na story hizi ambazo ni za wanafunz. Watu kama Prof Luhanga, Mwandyosya na hata Mshoro ni product za mwanzo za Dar Tech, bila kusahau Dr Nkwera wa NACTE, ni zao la Mtwara Tech then DIT
 
namkumbuka prof majani wa uclas(rip) kwamba kuna watu wanafundishwa kuwa punda ( watendaji) na wengine wanafundishwa kufikiri! Kauli nyingine tamu ilitolewa kwenye mahafali ya dit sikumbuki mwaka, na prof mayunga nnkhunya (rip) nesi hawezi ku claim udokta kisa anashinda na kuwajua vzr wagonjwa!
 
Back
Top Bottom