Engine nzuri za Toyota chini ya 2000 cc

fmlyimo

JF-Expert Member
May 4, 2012
324
198
Naombeni ushauri kujua ni engine gani za Toyota chini ya cc2000 ambazo hazisumbui na spear zake ninapatikana kwa wingi na kwa bei rahisi? Wengine wanasema ni 5E kama za Toyata Raumu na wengine wanasema 4E kama za Toyota Starlet au Corolla. Pia nimesikia 7A kama za Spacio na 3S kama za Rav4 za zamani. Nipo njia panda, msaada please!!!
 
ungesema ww unataka kuifunga katika gari gani? maana kunakuModify magari km ya Volkswagon, Corolla nk sasa ukitaja hiyo Body uliyonayo wataalam watajitokeza kukuelekeza na kukupa ushauri wa Gearbox iwe manual au AT
 
Hapana, sihitaji kumodify, ninachotaka kujua kama mtu unataka kununua gari, kwenye swala la engine ipi ni bora zaidi. Kwani unaweza kukuta gari aina moja lakini lina engine tofauti. Mfano Raum ina 5E, pia zipo Raum za kuanzia 2003 zina engine za VVTi. Hivyo nimeona bora ulizie aina ya Engine kuliko kuulizia aina za magari. Pia, je huu mfumo wa VVTi ni nzuri? Je vipi kuhusu upatikanaji wa spear?
 
Mkuu chukua 5A hii hata kwenye ulaji wa mafuta ni nzuri,inapatikana kwenye carina TI na corolla.
 
Naombeni ushauri kujua ni engine gani za Toyota chini ya cc2000 ambazo hazisumbui na spear zake ninapatikana kwa wingi na kwa bei rahisi? Wengine wanasema ni 5E kama za Toyata Raumu na wengine wanasema 4E kama za Toyota Starlet au Corolla. Pia nimesikia 7A kama za Spacio na 3S kama za Rav4 za zamani. Nipo njia panda, msaada please!!!
Hapa mkuu kuna tatizo ambalo lazima uwe makini nalo...

1. engine za corolla AE90 - AE 110 ni 5A na zimezoeleka kwamba hazili mafuta hizi kama ilivyo 2E na 4E takribani ni 1500cc.
2. 3S iko kama 4s tofauti ni ndogo sana hizi takriban ni 1800

baada ya kuwa umetambua hayo ningelipenda ujue kwamba engine tajwa hapo juu ni outdated na muda si mrefu ujao hata upatikanaji wa spare genuine itakuwa mashaka.

Hivyo basi chukua 7A ambayo hata ulaji wake wa mafuta ni mdogo na kasi ya gari ni kubwa zaidi kuliko hizo zilizotangulia.

Vinginevyo chukua Totoya Stalert au Spacio. ka matumizi madogo ya mafuta. hizi ni cc1200 - 1350 inategemea na wewe mwenyewe unapenda ipi.
 
Hapa mkuu kuna tatizo ambalo lazima uwe makini nalo...

1. engine za corolla AE90 - AE 110 ni 5A na zimezoeleka kwamba hazili mafuta hizi kama ilivyo 2E na 4E takribani ni 1500cc....

Nimekusoma mkuu, asante kwa mchango wako. Umeongelea kuhusu 5A za Corolla na 4E za Starlet ambazo umesema zimepitwa na wakati. Vipi kuhusu 5E? je nayo imepitwa na wakati? Nimeipenda sana Raum kwani naona ipo juu na CC zake ni ndogo ukilinganisha na Spacio. Lakini naona kuna zenye 5E na 1NZ. Je, ipi imetulia? Pia naona Spacio mpya nazo zina 1NZ. Je, hizi engine za 1NZ ni nzuri au presha tupu?
 
3s ni jiwe

Kweli mkuu. Naona inasukuma mpaka Noah. Je, kuna 3S yenye 1500cc au 1800 cc? Na kama ipo, je ipo kwenye gari gani? Nasikia haya ma-CC makubwa (kuanzia 2000cc) yanaumiza sana kwenye foleni zetu za Dar.
 
Nimekusoma mkuu, asante kwa mchango wako. Umeongelea kuhusu 5A za Corolla na 4E za Starlet ambazo umesema zimepitwa na wakati. Vipi kuhusu 5E? je nayo imepitwa na wakati? Nimeipenda sana Raum kwani naona ipo juu na CC zake ni ndogo ukilinganisha na Spacio. Lakini naona kuna zenye 5E na 1NZ. Je, ipi imetulia? Pia naona Spacio mpya nazo zina 1NZ. Je, hizi engine za 1NZ ni nzuri au presha tupu?
mkuu 5Endio kama 7A ila sasa kwenye 1NZ tatizo ni mafundi wetu na vema usichukue yenye supercharger ili kuepuka baadhi ya usumbufu.. kama wanavyoteseka na engine za VVTI ndivyo wanavyoteseka kwenye hizi mashine zote mpya zinazotumia mfumo wa umeme!!! Wanatulazimisha turudi kwenye Pijo na zi One - O - Nine!!

Ila kama una ubavu nunua gari hilo jipya kabisa na si hizi zi-recondition au used ili ulitumie kwa muda mrefu, hata siku likianza kuroga mafundi watakuwa wameshapata ujuzi! Vinginevyo cheza patapotea
 
mkuu 5Endio kama 7A ila sasa kwenye 1NZ tatizo ni mafundi wetu na vema usichukue yenye supercharger ili kuepuka baadhi ya usumbufu.. kama wanavyoteseka na engine za VVTI ndivyo wanavyoteseka kwenye hizi mashine zote mpya zinazotumia mfumo wa umeme!!! Wanatulazimisha turudi kwenye Pijo na zi One - O - Nine!! Ila kama una ubavu nunua gari hilo jipya kabisa na si hizi zi-recondition au used ili ulitumie kwa muda mrefu, hata siku likianza kuroga mafundi watakuwa wameshapata ujuzi! Vinginevyo cheza patapotea

Mkuu, asante sana. Mimi nafikiri nitaelekea kwenye 5E Kwani nataka cc1500 kwani naona 7A (1800cc) ni kubwa sana kwangu. Hahahaa, umenikumbusha mbali sana enzi Pijo na 109. Mambo ya carburators hayo. Tatizo mafundi wetu hawapendi kurudi darasani na kujifunza mifumo mipya.
 
Poa Kiongozi, nakutakia kila la kheri.:welcome:
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom