franckkimm
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 440
- 852
Rais wa klabu ya Yanga Eng. Hersi Said kupitia kipindi cha Jahazi kinachorushwa na radio Clouds hapo jana alieleza namna klabu ya Yanga inavyojiandaa kupokea wawekezaji baada ya mabadiliko ya kikatiba kukamilika kwa asilimia 100
Eng. Hersi Said amesema kuwa kwa mujibu wa mabadiliko ya katiba na uendeshaji wa klabu ya Yanga, Rais wa klabu ndiye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya klabu tofauti na klabu zingine kama Simba ambazo mwenyekiti wa klabu ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi.
“Bodi ya wakurugenzi ina watu tisa [9] Young Africans inapeleka watu watano, kwahiyo uwepo wa Yanga ni mkubwa zaidi kuliko mwekezaji”.
“Rais wa Yanga ndiye mwenyekiti wa bodi, Mangungu ndugu yangu akiingia pale yeye ni mjumbe”.
” Mwekezaji ananunua asilimia 49 lakini analipa mara moja, na atamiliki hizo hisa bila kikomo, iwe ni mmoja au wawili, atakayenunua hisa moja itakuwa ni ya kwake milele mpaka atakapoiuza”.
“Mwanachama wa Yanga atalipia ada yake kila mwaka, kwa muda mrefu mwanachama atakuwa na mchango mkubwa kuliko mwekezaji”.
“Mwanachama amekuwa na mchango wa kuipa nguvu hii timu toka 1935 kuhakikisha kwamba anakwenda uwanjani ananunua jezi”. Eng. Hersi alisema.
Kwa upande mwingine pia Eng. Hersi aliweka wazi namna ambavyo klabu inatengeneza mfumo ambao mwekezaji atakuta muundo bora wa utawala.
“Tunajenga mfumo ambao mwekezaji akija anakuta muundo bora wa utawala, kimapato”.
“Malengo yetu ni kuhakikisha kuwa na timu imara kiuchumi ili yule anayekuja awe na uhakika wa kile anachowekeza kwenye timu”.
“Hivyo tumezingatia sana usalama wa biashara kwa kila ambaye ana nia ya kuwekeza kwenye Klabu yetu”.
“Ili kulinda maslahi ya wawekezaji tumehakikisha kuwa lazima tuwe na Makubaliano ya kimkataba”.
“Vile vile tumelinda maslahi ya Klabu kwa kuhakikisha kuwa kinachopelekwa kwenye kampuni ni nembo na biashara ya timu”.
“Mali zote za Yanga zinabaki kuwa mali ya Yanga na sio mali ya kampuni. Kampuni mpya ya Yanga haitaimiliki Yanga, bali Yanga ndio itamiliki kampuni. Mwekezaji hana haki na mali za klabu kama vile uwanja na majengo".
Source:CloudsFm ( jahazi )
Sent using Jamii Forums mobile app