Endometritis inasababishwa na nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Endometritis inasababishwa na nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by tunyi, Jun 18, 2012.

 1. t

  tunyi Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mke wangu alichunguzwa akaambiwa ana Endometritis akapewa sylate tabs 1x1 kwa siku 5 na cifran CT 1x2 kwa siku kumi ila tatizo halijaisha.

  Mke wangu alikuwa akiona damu siku 3 ya 4 anakauka ila sasa anaona damu zaidi ya siku 7 kuna namna ya kumsaidia mzunguko wake urudikama ilivyokuwa awali yaani awe anaona siku zake siku 3 ya 4 awe amekauka?

  Je, Endometritis inasababishwa na nini?
   
 2. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lengo langu la kufungua JF Doctor leo ilikuwa niulize juu ya tatizo hili na ufumbuzi wake,please
  wataalam tupatieni msaada juu ya hili.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280

  Subirini Dr. Riwa na wengine wanakuja....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. kukucd

  kukucd JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2014
  Joined: Sep 5, 2013
  Messages: 265
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Help please jf doctors!!!kuhusu hili tatizo
   
 5. ram

  ram JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2014
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,209
  Likes Received: 909
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. ram

  ram JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2014
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,209
  Likes Received: 909
  Trophy Points: 280
  Ngoja nimwite na watu8, njoo please tuna shida huku
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2014
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Mbona kama hii habari ni ya muda mrefu kidogo, maana naona ilianzishwa hapa jamvini mwaka 2012...!!!
   
 8. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2014
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Ni nini hii kitu?
  Endometritis ni hali ya kututumuka (kuvimba) au kuwashwa kwa kuta ya nje ya mji wa mimba iitwayo endometrium.

  Chanzo ni nini?
  Chanzo cha endometrisis huwa ni infection inayokuwa imetokea kwenye miji wa mimba. Infection hii huweza kuletwa na:

  • Gonorea
  • Mchanganyiko wa bakteria waliopo ukeni
  • Kifua kikuu
  • Chlamydia.
  Pia unaweza mwanamke yupo hatarini kukutwa na endometrisis kama atapa miscarriage au wakati wa kujifungua mtoto.

  Pia mwanamke aliyekuwa na muda mrefu wa labor au operesheni ya uzazi (c-section) pia yupo hatarini kupata maambukizi.

  Dalili zake je?
  • Kutokwa na damu ukeni kusikokuwa na mpangilio.
  • Kutokwa na majimaji ukeni ambayo si ya kawaida.
  • Maumivu kwenye nyonga au chini kidogo ya tumbo.
  • Homa na kutojisikia vizuri kwa ujumla.
  • Wakati mwingine kukosa choo au kutoa choo kwa shida uwapo faragha.

  Matibabu yake yapoje?
  Endometrisis huwa inatibiwa kwa kutumia antibiotics na kwa wenye complications nyinginezo zenye kuambatana na endometrisis hupewa tiba kulingana na comlication husika.

  Kama una mtu ambaye unashirikiana naye tendo la ndoa ni vyema naye akapewa tiba kama tu daktari atang'amua kuwa una STI.

  Athari zake je?
  Ni vyema kupata tiba mapema inavyowezekana kwani uathirika wa muda mrefu huweza kupelekea complications zaidi kama ugumba, pelvic peritonitis n.k
   
 9. ram

  ram JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2014
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,209
  Likes Received: 909
  Trophy Points: 280
  Imeibuliwa upya, binafsi nimefaidika coz sikuwahi kuiona hii thread kabla, ahsante kwa majibu

   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mkuu wewe unatakiwa umtibie mke wako hutakiwi kujuwa mke wako hayo maradhi ingelikuwa hivyo Daktari angelikwambia kila kitu sasa mimi sio Daktari ila ninakwambia mke wako ana matatizo ya uvimb ndani ya mfuko wa uzazi (Endometritis) usije kumuambia mke wako utamstua roho yake Soma hapa kwa kiingereza kama unajuwa.

  Endometritis refers to inflammation of the endometrium,[SUP][1][/SUP] the inner lining of the uterus. Pathologists have traditionally classified endometritis as either acute or chronic: acute endometritis is characterized by the presence

  of microabscesses or neutrophils within the endometrial glands, while chronic endometritis is distinguished by variable numbers of plasma cells within the endometrial stroma. The most common cause of endometritis is

  infection
  . Symptoms include lower abdominal pain, fever and abnormal vaginal bleeding or discharge. Caesarean section, prolonged rupture of membranes and long labor with multiple vaginal examinations are important risk

  factors[SUP][citation needed][/SUP]. Treatment is usually with broad-spectrum antibiotics.

  The term "endomyometritis" is sometimes used to specify inflammation of the endometrium and themyometrium.[SUP][2]

  Tumia dawa za Hospitali ikishindikana nione mimi ninayo dawa kwa gharama lakini ukinitaka kuwasiliana na mimi bonyeza hapa.[/SUP]
  Mawasiliano[SUP]
  [/SUP]
  [SUP][​IMG][/SUP]
   
Loading...