Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 948
- 1,092
Habari vijana Tanzania.
Laiti vijana wa Tanzania tungekuwa na upendo na uaminifu mkubwa tungesaidiana kwa mengi sana mfano mitaji, kazi za kujishkiza na biashara kwa ujumla.
Kuna mikoa hapa Tanzania ina fursa nyingi sana na masoko yapo ya kutosha tatizo ni uaminifu kwa vijana waliowengi.
Fursa zipo mikoani lakini ni nani utamwamini na nani atakuwa na upendo wa hiyo fursa mfanye wote kwa kusaidiana. Mfano upo Dar es Salaam viatu, T-shirt za V, madela na viatu bei poa na unajua fika vinasoko Mwanza au Arusha. Pangekuwa na watu au vijana wa aminifu unamtumia mzigo anakuuzia then anajilipa mwenyewe commission maisha yanaenda.
Mfano2, Dodoma kuna soko kubwa la viazi vitamu na mtu yupo Ushirombo au Geita au Katavi kama pangekuwa na watu waaminifu unapakia mzigo watu wanaupokea then wanafanya maisha.
Ipo mifano mingi sana.
Jaribuni kusoma na kufatilia historia ya kampuni ya DHL Logistics Company walitengeneza uaminifu wakafanikiwa sana.
NB
MTAJI WA BIASHARA VIJANA NI UAMINIFU WAKO AMUA LEO UPATE MAISHA BORA NA MAZURI. WATU WEMA BADO WAPO HAWAJAISHA HAPA DUNIANI.