Endapo Mashtaka ya Erick Kabendera ni ya Kutengeneza basi gharika inakuja

Terrible Teen

JF-Expert Member
May 1, 2017
936
2,645
Ndugu wana JF. Mwandishi wa habari ndugu Erick Kabendera leo Novemba 07 alifikishwa tena Mahakamani kwa ajili ya kesi yake kutajwa. Kama ilivyo ada kwa mfumo wetu mbovu wa utoaji haki ni kwamba kesi imehairishwa sababu upelelezi haujakamilika na pia Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo ameteuliwa kuwa Jaji.

Nikirudi kwenye msingi wa uzi huu, tangu mwanzo kumekuwa na viashiria kuwa mashtaka ya Erick ni ya kubambikiwa hasa kutokana na mazingira ya kukamatwa kwake ambapo wenye mamlaka walikuwa wakibadili sababu kila wakati hadi walipompiga kesi isiyokuwa na dhamana.

Aidha, Erick Kabendera hivi majuzi aliwaagiza mawakili wake kumuomba msamaha mtu yeyote ambaye atakuwa amekwazika sababu ya shughuli zake za uandishi wa habari. Ni dhahiri kuwa mashtaka ya Erick yametokana na kazi yake na ukosoaji kupitia kazi zake.

Maono yangu ni kuwa, Mwenye Mamlaka aliyesababisha Erick afunguliwe mashatka haya amuachie huru ndugu huyu mapema iwezekanvyo kabla ya mwaka kuisha. Vinginevyo anajua nini kilimpata wiki mbili zilizopita. Anajua kuwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema alimfanyia alichofanya ili kumkumbusha kuwa naye ni binadamu na ameumbwa kwa nyama. Anajua kuwa kwa zaidi ya masaa 6 haukuwa na fahamu.

Mwisho , nimeona mateso anayopitia Erick leo. Kuna kila dalili anapata ulemavu wa kudumu. Mama yake ni mgonjwa sana. Ila kuna mtu kwa chuki tu anayafanya haya. Jumapili anakaa siti ya mbele kanisani. Namauonya kuwa mwaka huu hautapita kabla Mungu hajafanya uamuzi wake wa moja kwa moja. Mawakili wa Serikali , nawaonya pia mwaka huu hautaisha kabla ya Mungu kuliiinua Taifa lake dhidi ya uonevu.
 
Watu wanaojielewa huwa hawatoi vitisho vya kipuuzi namna hii....kumbuka huyu unaemtetea leo hii alikuwa anatumika na watu wabaya wasiolitakia mema Taifa hili...na kumbuka Kuwa ni Mungu ndiye aliyekuwa upande wetu akasaidia kuwezesha Kabendera kuwa ndani Leo hii...maana huyu tungemuachia aendelee na upuuzi wa kutumia kalamu Leo labda mamia na maelfu ya Watanzania wangekuwa wameisha umia na kupoteza maisha but kama kweli Maandiko yake alikuwa Hatumiki na hao Wapuuzi wasiolitakia mema Taifa hili GOD stand for him na kama alikuwa anatumia let him Suffer
 
Tunaomba japo maandishi ambayo aliandika na yalihatarisha amani..
 
Kama alikuwa anajua mama yake mgonjwa ama ana wategemezi asingepeleka pua yake kwenye "mambo ya watu".

Kufa kupo tu hata kwa watakatifu kwa hiyo wala siyo sababu ya watu kutokuwashughulikia wanaoleta u-much know!

USHAURI:Kama huwezi ku-pay the price of what you're doing,then fanya kitu kingine!

Gandhi aliwahi kusema,"ukiamua kuwa mkosoaji,utakuwa umejichagulia aina ya kifo utakachokufa "
 
Huyo alitumika na Mabeberu kuharibu Amani ya Nchi

Sasa wanasiasa wameacha anateseka peke yake
Hapa tuna la kujifunza sisi Wananchi

Huyo anayetumia madaraka yake kumtesa Kabendera, ajue madaraka yana mwisho na hana support ya yoyote kwenye utesaji wake. Tunamkubali Kabendera kuliko yeye na hata kwenye uchaguzi tumemdhihirishia hilo.
 
Watu wanaojielewa huwa hawatoi vitisho vya kipuuzi namna hii....kumbuka huyu unaemtetea leo hii alikuwa anatumika na watu wabaya wasiolitakia mema Taifa hili...na kumbuka Kuwa ni Mungu ndiye aliyekuwa upande wetu akasaidia kuwezesha Kabendera kuwa ndani Leo hii...maana huyu tungemuachia aendelee na upuuzi wa kutumia kalamu Leo labda mamia na maelfu ya Watanzania wangekuwa wameisha umia na kupoteza maisha but kama kweli Maandiko yake alikuwa Hatumiki na hao Wapuuzi wasiolitakia mema Taifa hili GOD stand for him na kama alikuwa anatumia let him Suffer
Embu ficha ujinga wako wee mataga hata kama kusaka uteuzi si kwa kujitoa ubinadamu kiasi hichi embu eleza hata kitu kimoja alichokua anatumiwa huyu Erick tatizo mnakaririshwa lumumba mnakuja kuharisha humu ni wapi erick aliandika habari ambayo ilisababisha watu tupigane au kuhatarisha amani? Kichwa kikubwa bila akili ni hasara kwa miguu
 
Tunamkubali Kabendera kuliko yeye na hata kwenye uchaguzi tumemdhihirishia hilo.

Huu ugoro ungewalisha watoto wako uliowatelekeza sweeden baada ya kutimuliwa kwa kufanya mambo haramu

Kabla kikundi cha watu wachache hamjafanya vurugu ni bora mtafute kabisa sehemu ya kukimbilia

Uliza maalim seif alivyowadanganya mahzib walivyonyooshwa

Don't try this
 
Bado unapiga propaganda mfu? Ni hivi,jiwe hakubaliki na hilo tumemdhihirishia kwenye uchaguzi huu. Kilichobakia ni yeye kutumia tu madaraka kunajisi box la kura.
 
Terrible Teen,

Muache tu huyo jamaa akabiliane na matokeo ya kuisaliti nchi. Wee unatumwa na mabeberu kuiandika nchi yako vibaya unakubali. Kweli ndiyo utu huo. Ndiyo maana mpaka leo akili yangu haiamni kama huyu jamaa ni raia kamili wa nchi hii. Yale maandiko yalikuwa ni ya mtu mwenye hila na njama.

Pia acha kumpangia Mungu kazi. Labda kama unasema miungu mingine. Wee ni nani mpaka umpangie Mungu kuwa mwezi wa 12 kuna sijui issue gani.
 
Terrible Teen,
Sijajua tatizo ni nini,watuhumiwa siku ya kwanza wakienda mahakamani wanakuwa wapo fiti lakini ikipita muda wanaanza kuchechemea sijajua nini kinawakumba......Nimeona Aveva na kaburu wanachechemea kabisa wanabuluza miguu.
 
Huyo anayetumia madaraka yake kumtesa Kabendera, ajue madaraka yana mwisho na hana support ya yoyote kwenye utesaji wake. Tunamkubali Kabendera kuliko yeye na hata kwenye uchaguzi tumemdhihirishia hilo.
Uchaguzi gan mmefanya mkashinda?

Wakati CCM imeshashinda hata kabla ya pambano

Uliza Hai kwa Mbowe
 
Hatuna cha kukusaidia......

Kama mambo uliyoyafanya kwa kalamu yako kwa kuagizwa na kupewa ujira na mabeberu basi mamilioni ya watanzania wangeangamia kwa kuuana wenyewe
 
Back
Top Bottom