Employer kupekua NSSF ya mwajiriwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Employer kupekua NSSF ya mwajiriwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nikupateje, Feb 12, 2010.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kumeanza kujitokeza mtindo ambapo NSSF wanatuma statement zao kwa waajiri (employer) ili kuwasambazia waajiriwa wao. Yaani kama mtu anafanya kazi kwenye KAMPUNI B basi NSSF ni kama vile wameshakubaliana na KAMPUNI B kwani NSSF wana list ya majina ya staff wa hiyo KAMPUNI B na hivyo wanatuma kila mwezi statement zinazoonyesha balance yako ya NSSF.

  Sijaelewa ni kwa lengo gani japo inaelekea kwamba ni kumrahisishia mchangiaji ambaye ni mwajiriwa kujua balance yake.

  Lakini je pamoja na hayo mwajiri ana haki gani ya kujua balance ya mwajiriwa wake? Kwani mwajiriwa ndiye beneficiary wa NSSF na wala si employee.

  Pili ni kwamba naamini kuwa NSSF balance au amount ni confidential information. Je, Administration au Human Resource officers wa employer si tayari wanakuwa wameshajua balance yako ya NSSF?

  Naomba kusaidiwa ufafanuzi na kujua sheria inayozungumzia hilo.
   
 2. Mnhenwa Ndege

  Mnhenwa Ndege JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Vipi baba mbona sikuelewi, sasa balance yako ya NSSF itakuwaje confidencial kwa mwajiri wako wakati yeye ndiye anayepeleka hiyo michango huko NSSF. Na kama mwajiri wako ana rekodi nzuri anaweza kujua balance yako hata bila ya kuletewa hiyo statement.

  Mimi hucheki balance yangu ya NSSF kutoka kwa mwajiri wangu maana record za NSSF huwa ziko nyuma. Hili sio swala la nyeti bana. Siri siri za nini kwani wewe ni fisadi?
   
 3. K

  Kisanduku Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 90
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Mkuu, hebu nipe somo, mwajiri wangu wa sasa kinachomhusu ni ile michango anayo-submit kipindi chote ninachoajiriwa naye.

  Je, michango yangu kabla sijaariwa naye yaani nilipoajiriwa na taasisi zingine huko nyuma yeye inamhusu nini?

  Tukumbuke kwamba ukipenda hata wewe bnafsi unaweza kuongoezea kiasi chako kama unvyo-deposit kwenye bank kama kweli umeamua kuwekeza huko NSSF. Je kama ulifanya hivi na hivi vinamhusuje huyu mwajiri wa sasa yaani kwa nini yeye awe exposed kwavyo?
   
 4. Abraham

  Abraham Senior Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Basically, that's absurd! Member wa NSSF (Mwajiriwa) ndio anatakiwa afuatilie NSSF ili kuconfirm kwamba contribution zake zinapelekwa na Mwajiri. Hivyo kumtumia mwajiri statement ni upuuzi mtupu ambao hauleti tija!

  NAtoa wito kwa NSSF kuacha mara moja
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,970
  Likes Received: 294
  Trophy Points: 180
  Balance yako si lazima iwe imetoka kwa mwajiri wako wa sasa tu, inawezekana hiyo kampuni ikawa ni ya tatu, nne au zaidi so balance yako haitakuwa inahusiana na mwajiri wa sasa. So it can be cinfidential. Actually hiyo defined contribution scheme ni kati yako na NSSF na si mwajiri ingawa mwajiri ndo anayechangia. So NSSF wanatakiwa wakutaarifu kwanza ndipo waweze kutoa hizo info.

  Mbona mwajiri ndo anakupelekea hela benki lakini benki haiwezi tuma statement yako kwa mwajiri wako?
   
 6. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mwajiri ndiye anayepeleka michango ya kila mwezi ya Mumishi hivyo ni muhimu kujua kama akiba imewekwa vizuri.Na hapa si swala kujua tu kuna mambo ya reconciliation.

  Au una ugomvi na HR wako??
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,934
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mimi nina utaratibu kila mwisho wa mwaka naomba statement yangu ya NSSF na ninaletewa chini ya dk 10 na hao watu wa HR, sasa mkuu hapo sidhani kuna siri tena kati ya NSSF na wewe/mimi coz wale hr pale kuna mtu ambaye anashughulikia hii issue ya NSSF, na kwa maana hiyo mwajiri wako lazima ajue coz siku NSSF wakikupunja kama mwajiri wako hajui alipeleka kiasi gani kule atakutetea vipi mkuu? huoni kwamba yeye anapaswa kujua kwa sababu ninapofanyia kazi mimi nachangia lets say kilo na nusu na mwajiri wangu anachangia kiasi hicho hicho kwa mwezi, KWA NINI ASIJUE?
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 3,141
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nijuavyo na kwa uelewa wangu NSSF contribution ya mfanyakazi siyo siri hata siku moja kwa mwajiri wako kwa kuwa yeye mwajiri kwa mjibu wa sheria anatakiwa kuhakikisha anachangia na kujua michango yako kuwa inapelekwa kwenye hilo shirika.
  Mwajiri ndiyo mwenye jukumu la kukamilisha utaratibu wote wa (withdraw) pale mfanyakazi anapokuwa anataka kuchukuwa michango yake pale anapokuwa amesitisha ajira iwe aidha kufa,kuresign au kuachishwa, pia ni jukumu pia la mwajiri kumpa takwimu mfanyakazi kuwa michango yake kuwa imepelekwa NSSF.

  Inwezekana wewe unaugomvi labda na huyo mwajiri wako au unaugomvi na huyo anayeshughulikia contibutions za wafanyakazi hapo kazini kwenu ila hakuna ubaya hata siku moja.

  na hata ukienda nssf kudai michango yako watakurudisha kwa mwajiri kujaza baadhi ya form sasa unachoficha nini hela ni zako na hawezi hata siku moja kwenda kuzidai tena unatakiwa kushukuru kwa kuwa mwajiri wako ana mpango mzuri kufuatilia na accounts zenu zipo updated.

  Ulizia yanayotoke Mtibwa na kwingineko wafanyakazi wanakatwa michango yao ila hailejeshwi NSSF.

  tafadhali angalia hiyo attachment halafu uniambie unachoficha nini?
   

  Attached Files:

 9. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kuwa Mwajiri ndie anaepeleka michango yote ya waajiriwa wake, account ya NSSF ni ya mwajiriwa binafsi. Hivyo hakuna mtu mwingine yeyote mwenye mamlaka ya kujua siri ya account hiyo.

  Kama kuna tatizo katika akiba inayowekwa kila mwezi, mwajiriwa anao wajibu wa kuchukua statement yake, na kuuliza kwa mwajiri kuhusu tatizo ambalo ameliona katika account yake, na si vinginevyo. Hili ni jukumu pekee la mwajiriwa kulalamika na kufuatilia kwa kuwa yeye ndie mfaidikaji pekee wa account hiyo, na pia ana kila information ya kumsaidia kujua kama akiba iliyowekwa si sahihi kupitia pay slip, offer letter, na formula zilizopo za jinsi ya kukokotoa akiba za NSSF.

  Kama kweli NSSF wanafanya hivyo, wanafanya kwa makosa makubwa. Waache mara moja kutoa siri za account za watu. Wanachotakiwa ni kutuma statement kwa mwenye account pekee.
   
 10. H

  HUBERT MLIGO Member

  #10
  Feb 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  "
   
 11. Mrbwire

  Mrbwire Senior Member

  #11
  Feb 12, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 198
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sioni kama kuna tatizo km employer wako atajua balance yako. Lakini pia ni kweli kuwa atajua balance yako kabla hujaenda kwake, in other words kama ulimwambia ulikuwa unapokea 4M. huko ulikotoka wkt kumbe ilikuwa ni laki sita basi issue itakuwa wazi.... Labda km you are facing that problem then useme ili wachangiaji wajue namna ya kusaidia.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...