Employee's disciplinary codes and permissible penalties | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Employee's disciplinary codes and permissible penalties

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by NewDawnTz, Jul 25, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wandugu habari.

  Kwanza niseme mimi ni mwajiri anaechipukia na ninatengeneza sera yangu ya usimamizi wa rasilimali watu.

  Ninaomba nisaidiwe kufahamu, je baada ya kutungwa kwa sheria mpya ya Kazi ya mwaka 2004 (The Employment and Labour Relations Act, 2004) je inamaanisha (kama nitakuwa nimeielewa second schedule ya sheria hii kwa lile neno "whole repealed") kuwa ile sheria ya Kazi ya mwaka 1964 (Security of Employment Act CAP 574 of 1964) haitumiki tena?

  If so, swali langu la msingi ni kuwa, sheria ile ilitoa muongozo wa hatua za kinidhamu (code of disciplinary) kwenye second schedule yake pamoja na permissible penalties ambazo zilikuwa zikisaidia sana kwenye maamuzi ya adhabu za mfanyakazi. Kwa hii sheria ya sasa ya mwaka 2004 hizi code of discipline hazipo sasa sijajua je kuna kifungu chochote kinachotoa muongozo kama ule wa second schedule ya 1964 au ndio kila mwajiri atakavyojiamulia kivyake?

  Au ndio sawa na ile iliyoonyeshwa kwenye section 99 ya sheria ya 2004 kuwa Waziri atatoa CODE OF GOOD PRACTICE na kuzibandika kwenye gazeti la serikali, je ndiyo mbadala wa zile code of discipline au ni vitu viwili tofauti? Kama ni kile kile kitu kimoja, je zimeshachapishwa kwenye gazeti la serikali? and if so, je naweza kupata msaada wa kuzipata?

  Nawasilisha na ahsanteni sana
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 180
  Nenda TUCTA au Tanzania Employers Association au muone labour lawyer yeyote. Nadhani utapata majibu ya maswali yako huko.
   
 3. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hii ya sasa ina mabadiliko makubwa sana. Lakini makubwa zaidi ni waliondoa ule mtindo wa kujaza fomu za onyo etc. Sasa hivi utaratibu ni kama imethibitika yale yaliyoonyeshwa katika sheria hiyo kama yametokea na kufuatwa muajiri anafukuza bila hata fomu. Na katika hayo yaliyotajwa ni pamoja na kama anakuona humfai tena kwa labda elimu yako haiendani na mabadiliko yaliyofanywa katika sector hiyo mf. kuna machines za teknologia mpya ambayo wewe elimu yako hairuhusu. Na mambo mengi yameainishwa humu. Na kuna taratibu zake za kufuatwa. Kwa kifupi hii Act mpya imesaidia kiasi fulani kuondoa migogoro ambayo ilikua inalea uvivu kazini na muajiri akapewa nguvu zaidi ya kumfukuza mtu. Pia imeanzisha reconcilliation and arbitration boards ambazo zimewekea muda maalumu kushughulikia migogoro ya kazi ikishindikana ipelekwe labour court. Na pia imeruhusu migomo kazini ambayo zamani ilikatazwa.
  Hivyo basi kuna labour rules ambazo ndio hizo zinatoa maelekezo ya kila kitu katika mambo ya kuachisha mtu kazi ambayo ukiisoma au ukipata mtu anaejua sheria atakuelezea zaidi. Jaribu kwenda Open University wana kitengo cha legal aid watakufahamisha zaidi.
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ruge unajaribu kusema nini hapa? unadhani hawa wanapatikana kila mahali kwenye nchi hii au ofisi zote zipo walippo? Nimeuliza hapa kwa kuwa nafahamu kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kisheria na ambao wanaweza kusaidia eneo hili.

  BTW ahsante kwa mchango wako
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 6. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
   
Loading...