Emmanuel Mbasha aachiliwa huru kesi ya ubakaji

Emmanuel Mbasha aachiliwa huru kesi ya ubakaji

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
attachment.php


Mahakama ya Ilala, Dar imemwachia huru Emmanuel Mbasha leo Jumatatu Septemba 21, 2015 baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la ubakaji dhidi yake.

Itakumbukwa mwaka 2014 Emmanuel Mbasha ambae ni mwimbaji wa injili na mfanyabiashara alifunguliwa mashataka mawili mahakama ya Ilala kwa makosa mawili ikiwemo la ubakaji. Katika shitaka la kwanza Mei 23, mwaka 2014 eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, ilidaiwa kinyume cha sheria alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka 2014 eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake.
 

Attachments

  • MBASHA.jpg
    MBASHA.jpg
    19.5 KB · Views: 30,914
Sasa ni wakati wake wa kupiga pesa kupitia wanasiasa. Yaani asipopiga 500M muda huu uliobaki, fursa nyingine itabidi aisubiri 2020
 
Sasa ni wakati wa kupiga 500m toka ccm,tumia akili ya kuzaliwa wajinga ndiyo waliwao
 
mbasha kama anaakili huu ndo muda wa kupiga hela ya ccm!
 
  • Thanks
Reactions: aye
ugomvi wa panzi furaha kwa kunguru
 
Hivi na yule mtoto wa Flora ilishadhibitishwa ni nani baba yake? Maana kuna tetesi zilizagaa kwamba Flora aliondoka kwa Imma akiwa na kichanga kwa tumbo..
 
Hongera kijana. Ila kama uko tayari kununuliwa tutakusikia ukipepeta mdomo soon.
 
Mbona Wataifilisi CCM, Mwisho Wa Siku Lowassa Ni Rais..Mahakani Siasa Ila Makanisani Hairuhusiwi...

Acha hizo..haifai kabisa ndugu yangu.

Sijui umekula maharage ya wapi wewe, sijui nikupe sinia la malimao wewe, sijui nikuletee mshenga akupashe wewe...

Ile kesi ilikuwa na ushahidi hafifu sana.
Flora na mdogo wake walichemsha vibaya sana kwenye comment za magazeti achilia mbali mahakamani

Bwana Ryaro usitake kuishusha hadhi mahakama kwa kitu ambacho ilishaonekana wazi kuwa ni kesi ya kuchonga..
Ililenga kuficha aibu za wanene....walijihami kwa kesi ikawabumburukia usoni.
 
Back
Top Bottom