Emirates yanunua ndege 40

Salute kwako mkuu izzo.Very impressive analysis.
 
Donor country huku kandege ketu kako lockerup za Canada,kanadaiwa
mbona tunaweza isipokua hatujaamua tu cc ni "donor county" kwa tariifa yako
 
Sasa ni maendeleo gani, wafanyakazi na wafanya biashara makato ni makubwa ni kama kukomoana. Angalia hata thamani ya shilingi huporomoka, makusanyo ya kodi kwa maana ya vyanzo vipya vya mapato hakuna which seems kubana kupitia ukusanyaji tu ndo solution, itatuchukua miaka mia kwa mtazamo wa inchi ya viwanda kuwa the reality case!!!
 
Aisee kama kuna kipindi Boing imefanya biashara ni kipindi hichi cha Trump
 
Njemba zilizotumwa na nanihii bado ziko kwenye mazungumzo lakini mazungumzo yanaelekea hayatakuwa na manufaa bila njuluku za kulipa angalau $12.5 million papo hapo na balance kulipwa haraka iwezekanavyo katika kipindi cha miaka miwili au mitatu na riba juu. Kuna tetesi kwamba mazungumzo yameongezwa muda.

bombadear yetu itakuja lini?
 
Humu ndani kama kila moja wetu angekuwa kama wewe, basi IQ yetu ingekuwa ni triple digit. Big up Comrade and keep it up..
 
Ukisoma history ya Emirates walianza na kukodishia tu ndege toka Pakistan 1986 leo hii wote tunaona. Shekh Mohd alikuwa na vision tu nataka hivi basi wakaja mzee tupe mtaji million 10 ndio mwanzo wao na walichofanya kujenga uwanja mkubwa na sio uwanja tu lazima kuwe na Hotel za kutosha kukuwa pamoja na wingi wa watu yaani mipango yote inaenda sambamba. Kila mtu kafanya kwa upande wake kuelekea one vision. idara za serikali zinashindana kiutendaji wa goals na targets. wakati sisi tuna Air Tanzania wao walikuwa hawana hata ndege. tumebaki uchama tu ohh sijui barabara sijui michango ya shule. kwao ni aibu mtu kusema barabara ni achievement maana ni wajibu wa serikali kuboresha miundo mbinu sio kupigia kampeni. leo hii airport yao huna haja ya kupitia immigration officer ukitaka unatumia smart gate yote kuwafanya watu wavutiwe kupitia Dubai na ukipita Dubai lazima uta spend airport au utatoka kuchukuwa hotel na ukitoka utanunua zawadi tu kwa hiyo ndege ina link na kila kitu katika maisha ya Dubai. we have long way to go lakini sio impossible. ukiwa unatembea kati ya Terminal C na B utaona wameweka history yao starting 1986 mpaka leo kweli utafungua mdomo tu hakuna maajabu ni vision na hard work.
 
Hawa waarabu kama si vitavita wangekuwa mbali mno,
ndo maana kila baada ya miaka kadhaa lazima wapunguzwe speed kwa miji yao kuharibiwa,bila hivyo wanafanya kufuru mno,
mshindani wao mkuu eneo hilo ni iran ,ila wakiungana wote hawana mshindani kiuchumi hapo hata Turkey anakaa
 
Duuh jamani hivi kindege chetu kimoja tu ndo huko Canada wamekatalia kabisa?

Kweli tuko tofauti aisee
Mijitu ina sifa kinoma inaagiza mindege kibao wakati sisi kindege kimoja tu kimeshindikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…