Embu tuzijadili benki zetu kulingana na ufanisi wao

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,413
3,904
Nisaidieni, ni Benki gani ambayo ukiingia tu wahudumu wanakukimbilia kama mpira wa kona na vilevile wana huduma za kuingiza na kutoa hela kwenye account kupitia MPESA? Juzi nimetoka kurenew kadi yangu ya CRDB, huduma mbovu kabisa. Niko tayari kuhamisha sh 5,000 yangu!

Kwa kweli hapa Tanzania, Benki ni moja ya sehemu nisizopenda kwenda kabisa. Wafanyakazi wamelala, wanajivuta na hawana energy kabisa.

Sijali kulipa account fee kubwa, nahitaji huduma fasta na waonyeshe kunijali. Kawaida huwa sijali kulipa zaidi kwa huduma nzuri. Niliachana na TIGO baada ya kupiga mara mbili kwa tatizo dogo la kwenye TIGO-Pesa na nilijibiwa vibaya. Baada ya hapo Vodacom wamefaidika sana na hela yangu.
 
Niongee tu ukweli ukitegemea kwenda kwenye huduma yeyote Kwa mawazo ya kutegemea kujaliwa au kupokelewa vizuri subiria ukaipate mbinguni, taasisi,makampuni yote hayana shida na kuna binadamu wema na wabaya pia kuisema taasisi unakosea hapo imetegemea ulikutana na MTU mwenye tabia ipi, kwetu tz customer care industry bado ni Kwa watu wachache tu sababu customers care huanzia nyumbani kwenye malezi.Hata km MTU akipewa PhD ya customers care km si wa kubadilika ni ngumu. Ili usiumie kuwa flexible ktk maisha usiyabebe mambo na tegemea yote ukihudumiwa vizuri sawa usipo sawa uwe MTU wa kupotezea stress free man.Huwezi kuwabadilisha watu jibadili mwenyewe kuwa positive ili laws of nature ikikutanishe na watu wema kwenye sehemu za huduma. Ktk bank bora CRDB still inaongoza.
 
Brick and mortar banks sio k
wa sa hvi , kuongeza branches ni kujiongezea mzigo utahitaji more staff running cost ya branch moja sh ngapi kwa mwezi? Mambo sa hvi ni digital wawekeze zaidi mobile banking.
Wajifunze na Vodacom wamekuwa wabunifu matokeo yake benki zote sa hvi lazima transaction za mobile wapitie voda hpo napo voda sa hvi wanatoa mikopo kwenye simu.
Sasa voda watakapofika kutoa mikopo tuseme 5m, hamna kupanga foleni paper work hakuna mkopo ukiomba dk 1 umeingia kwenye simu yako benki zisome alama za nyakati.
Kuna rafiki yangu kutoka nchi jirani alinieleza benki huko wanafunga matawi wanawekeza kwenye mobile banking mikopo wanatoa hadi 70m kwenye simu hapo credit officer, meneja hamjuani cha kushangaza marejesho ni 95% defaults ni kidogo sana.
 
Niongee tu ukweli ukitegemea kwenda kwenye huduma yeyote Kwa mawazo ya.....

Ushauri mzuri. Mimi ni mtu positive sana. Pamoja na yote yanayokera huwa nakuwaga mpole na hata huwa nawashukuru kwa huduma yao.

Ni kweli malezi ni muhimu sana katika kujenga tabia ya mtu ila nadhani wana fikra potofu kuhusu huduma wanayotoa. Kuna dhana potofu iliyojengeka kichwani mwao ambayo ni nje ya malezi inayowafanya wanyate vile.
 
mimi natumia equity bank hizi nmb na crdb nilizibwaga zamani sanaaaa...

hata nikiwa mikoani ambapo equity hana branch huwa na withdrawal kwa sim banking tu.. nahamishia mpesa.. maisha yanaendelea
 
Brick and mortar banks sio k
wa sa hvi , kuongeza branches ni kujiongezea mzigo utahitaji more staff..........

Ni kweli. Mobile banking ndiyo suluhisho. Hakuna mantiki yoyote mtu unaenda kuweka hela benki unakaa kwenye benchi masaa. Kwa watu tusiopenda kukaakaa tu, hilo huwa ni mtihani.
 
mimi natumia equity bank hizi nmb na crdb nilizibwaga zamani sanaaaa...

hata nikiwa mikoani ambapo equity hana branch huwa na withdrawal kwa sim banking tu.. nahamishia mpesa.. maisha yanaendelea

Yes. Na mimi kwa kiasi kikubwa natumia mtindo huo ila adha inakuja unapotaka kuweka au kutoa hela kubwa au kudeposit cheque. Hapo kunakuwa hamna jinsi.
 
Wazo zuri ila kwa mtu mwenye fikra pana sio kitu cha kirahisi, si cha kukurupuka. Hiyo ni long term plan.. Benki zikikurupuka kutoka ktk mfumo zilionao na kuinvest ktk huo mfumo huenda ni hasara kubwa zikapata. So kujiconect na voda kwa hiyo huduma sio kitu cha ajabu zishafanyika tathmini sana na hasara inaonekana itakuwa cost
 
Mimi bado sijashawishika gharama za mobile banking za mitandao ya simu hasa kwenye kutoa, zinaendana na thamani ya huduma. Mentally huwa nachukulia gharama za kuwithdraw ATM au tawini (kama sh 1000) kama benchmark.
 
Benki za nchi jirani zimeungana wamekuja na pesa link, kuhamisha pesa toka benki moja kwenda nyingine ni dakika na inagharimu 1000tsh kuhamisha 20m.
Benki zetu jamani kuweni wabunifu biashara ipo kubwa tu.
 
Brick and mortar banks sio k
wa sa hvi , kuongeza branches ni kujiongezea mzigo utahitaji more staff running cost ya branch moja sh ngapi kwa mwezi? Mambo sa hvi ni digital wawekeze zaidi mobile banking.
Wajifunze na Vodacom wamekuwa wabunifu matokeo yake benki zote sa hvi lazima transaction za mobile wapitie voda hpo napo voda sa hvi wanatoa mikopo kwenye simu.
Sasa voda watakapofika kutoa mikopo tuseme 5m, hamna kupanga foleni paper work hakuna mkopo ukiomba dk 1 umeingia kwenye simu yako benki zisome alama za nyakati.
Kuna rafiki yangu kutoka nchi jirani alinieleza benki huko wanafunga matawi wanawekeza kwenye mobile banking mikopo wanatoa hadi 70m kwenye simu hapo credit officer, meneja hamjuani cha kushangaza marejesho ni 95% defaults ni kidogo sana.
hakuna sheria inayosimamia kikamilifu taasisi za fedha dunia inayoruhusu makampuni ya simu kutoa mikopo mikubwa kama ivyo so huo ni uwongo pia izo kampuni za simu iyo shughuli ya utoaji mikopo sio kazi yao kuu thats why wametakiwa kufungua mabenki kwa ajili ya huduma za kifedha
 
Back
Top Bottom