Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 253
- 893
RIWAYA; ELIZABETH NEVILLE
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
Sehemu Ya Kwanza
Ni asubuhi na mapema ndani ya mji wa Mafinga uliopo mkoani Iringa, Tanzania. Baridi likiwa kali sana. Watu walikuwa wanatembea mitaani huku wakiwa wamevaa makoti makubwa kupambana na baridi hiyo.
Katika hoteli moja iliyopo katika mtaa wa Pipeline ndani ya mji huo kulikuwa na kikao cha siri cha watu wawili. Saa tatu sasa walikuwa wanapanga mikakati yao.
"Sasa Martin fanya juu chini umpate Elizabeth Neville, ni yeye pekee ndio anajua kila kitu kuhusu mimi, na nina hakika endapo atathubutu tu kusema basi nimeangamia na ndoto yangu ya kuja kuwa rais wa Tanzania itakuwa imefikia kikomo." Lucas alisema kwa sauti ya upole na kusisitiza.
"Usiwe na hofu yoyote Mheshimiwa Lucas. Mimi ndiye Martin, sijawahi kushindwa kazi yoyote ile. Ukiwa na tatizo lolote lile jua lifikapo kwa Martin limekwisha. Nipe siku tatu tu nitakuletea Elizabeth Neville mikononi mwako na utaamua mwenyewe nini cha kumfanya. Nakuhakikishia siri yako haitotoka katika mdomo wa Elizabeth Neville kwenda katika sikio lolote lile lingine hapa duniani." Martin alisema kwa kujiamini.
"Nakuamini Martin Hisia. Sasa nakupa hizi milioni kumi za awali, na nitakupa milioni kumi na tano baada ya kukamilisha kazi hii. So milioni ishirini na tano ulizozihitaji zitakuwa zimekamilika" Lucas alisema huku akimkabidhi Martin bahasha yenye milioni kumi. Martin alizipokea, wakaagana.
"Huyo Elizabeth Neville atakuwa anaijua siri gani ya waziri?. Maana kumpeleka kwake hiko kiumbe dhaifu tu katoa milioni ishirini na tano. Nitaifanya kazi hii siku mbili tu ili animalizie milioni zangu kumi na tano nilale mbele." Martin aliwaza akiwa ndani ya gari yake.
"Namwamini sana Martin atakamilisha hili kwa ufanisi mkubwa. Jamaa anaonesha yupo makini sana kazini. Huu ndio utakuwa mwisho wa Elizabeth Neville na marecord yake, na safari ya kuelekea ikulu itakuwa nyeupee" Lucas alikuwa anawaza.
Martin alirejea katika nyumba yake iliyokuwa katika mtaa wa Pareto. Alipiga honi na mlinzi wake alifungua geti. Baada ya kushuka garini alimsalimia mlinzi wake na moja kwa moja aliingia ndani. Alienda katika chumba chake anachotunza zana zake za kazi, akachukua bastola yake pekee na kuiweka kiunoni vizuri akiifunikia na shati.
"Sihitaji kubeba zana nyingi, hii ni kazi ndogo ingawa malipo yake ni makubwa sana" Martin aliwaza.
Alitoka nje na kuondoka na gari yake ndogo aina ya Toyota vitz. Naenda kumchukua Elizabeth Neville, akijifanya mjuaji naitoa roho yake mara moja. "
Dakika ishirini baadae ilimkuta Martin mbele ya nyumba akiyoishi Elizabeth Neville. Nyumba kubwa na nzuri iliyokuwa katika mtaa wa Kinyanambo.
"Bila shaka hii ndio nyumba ya Elizabeth Neville" Martin alisema wakati akishuka garini.
Alifika getini na kugonga hodi. Alisikia kishindo cha mtu akielekea getini. Martin alikaa tayari kwa lolote. Mara alisikia kelele za mlango ukifungulia. Geti likafunguliwa. Alikuwa anatazamana na mama wa makamo.
"Bila shaka atakuwa mama yake Elizabeth Neville" Aliwaza.
"Shikamoo mama" Martin alisalimia.
"Marhaba mwanangu sijui nikusaidie nini?"
"Nimekuja kumuulizia Elizabeth Neville. Ni rafiki yangu tulisoma shule moja, ila tumepotezana siku nyingi sana kwakuwa mimi nilienda kusoma nje ya nchi" Martin alidanganya.
"Kwani hujasikia yaliyompata Elizabeth Neville? Labda kwa kuwa ulikuwa nje ya nchi muda mrefu."
"Kimempata kitu gani Elizabeth Neville?" Martin aliuliza akiwa na wasiwasi.
Yule mama alianza kulia. Aliivuta kanga yake na kufutia machozi.
"Mwanangu Elizabeth Neville ametekwa mwezi wa pili sasa?"
"Ametekwa? Ilikuaje? Ametekwa na nani?" Martin aliporomosha maswali mfululizo.
"Ingia ndani mwanangu nikuelezee, si vyema kuongelea haya mambo hapa getini"
Martin na yule mama waliingia ndani. Walikaa katika sofa zilizoruhusu waangaliane.
"Elizabeth Neville alitekwa hapo nje. Ilikuwa mida ya saa moja hivi. Elizabeth alikuwa anaenda katika sherehe ya harusi ya rafiki yake, nilimsindikiza hadi pale getini, wakati tunaagana ghafla zilitokea gari mbili nyeusi na kufunga breki miguuni mwetu, walimvuta kwa nguvu Elizabeth na kumtia ndani ya gari na kuondoka nae. Ni mwezi wa mbili sasa tangu tukio lile baya kutokea" Yule mama alisema huku machozi yakimtoka.
"Daah pole sana mama, kwani ulikuwa na mahusiano gani na Eliza?" Akauliza.
"Eliza ni mwanangu wa mwisho. Katika maisha yangu nimejaaliwa kupata watoto wawili tu, Elizabeth na kaka yake Moses" Mama Elizabeth alijibu.
"Huyo Moses anaishi hapa naye?" Martin akauliza.
"Hapana. Moses anafanya kazi Mbeya. Ameoa na anaishi na familia yake huko."
"Je tukio la kutekwa rafiki yangu mliripoti polisi, na walisemaje? " Martin aliuliza.
"Tuliripoti, na kila siku wanasema bado wanaendelea na uchunguzi. Mwezi wa pili huu sasa"
Daah pole sana mama. Kama nilivyokueleza naitwa Peter. Ni rafiki mkubwa wa Elizabeth Neville. Na nakuahidi nitakusaidia katika msako wa kumsaka hadi apatikane. Naomba sana ushirikiano wako mama" Martin alidanganya.
"Karibu hapa muda wowote ule, nitakusaidia chochote kile kuhakisha Elizabeth anarudi na waliofanya huo mchezo mchafu wanakamatwa na kuozea jela" mama Elizabeth alisema kwa uchungu.
Walibadilishana namba za simu kwa ajili ya mawasiliano. Martin alitoka nje akisindikizwa na mama Elizabeth. Aliingia katika gari yake na kuondoka.
"It can't be serious!!! Elizabeth Neville was kidnapped? Nani aliyetuwahi huyo?"
Martin alitoa simu yake na kumpigia Lucas.
"Haloo Martin, vipi umefanikiwa kumpata Elizabeth Neville?"
"Hapana Mheshimiwa, Elizabeth ametekwa!"
"Whaaaat!!!" Lucas aling'aka simuni.
"Ndo hivyo Mheshimiwa. Nimeenda nyumbani kwake Kinyanambo na kukutana na mama yake mzazi Elizabeth. Amenambia tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita. Elizabeth ametekwa mbele ya macho yake akimsindikiza kwenda katika harusi ya rafiki yake. Gari mbili nyeusi ndizo zilizombeba Eliza"
"Oooh my God, this is very dangerous to me. Ni nani hao waliomteka Elizabeth Neville? Kwa lengo gani?"
"Tutajua Mheshimiwa. Kwakuwa hii kazi umenipa mimi hakuna litakaloshindana. Elizabeth atarudi mikononi mwako, ingawa sio kwa malipo yake tuliyokubaliana awali"
"Pesa kwangu si tatizo. Nitakupa kiasi chochote kile cha pesa ilimradi tumpate Elizabeth. Yeye ndio kikwazo pekee katika safari yangu ya kuelekea ikulu. Lazima tumpate Elizabeth" Lucas alisema.
"Nitakupigia Mheshimiwa...." Martin alisema huku akikata simu baada ya kuona taa nyekundu katika saa yake aliyoivaa katika mkono wake wa kushoto inawaka. Akanyoosha mkono na kuupeleka sikioni kwake. Aliisikiliza ile saa.
"....kama nilivyokwambia Felix. Kuna jamaa amekuja hapa leo kumuulizia Elizabeth. Amesema ni rafiki yake walisoma shule moja zamani na baadaye yeye akaenda nje ya nchi..." Kukawa kimya. Baadaye mama Elizabeth akaongea tena.
"He is lying. Elizabeth amesoma shule ya wanawake watupu tangu nursery. Yeye kasoma nae wapi?, na ilihal Elizabeth hajafika chuo"
Kukawa kimya tena. Mama Elizabeth akaongea tena.
"Nimeweza kumpiga picha nitakutumia baada ya muda mfupi" Kisha saa ya Martin ikazima ile taa nyekundu.
"Kuna mchezo nachezewa. Mama Elizabeth anawajua waliomteka mwanae. Hanijui mimi ni nani? Kile kifaa nilichoweka pale kwenye sofa kitanisaidia sana kujua watu atakaongea nao akiwa pale ukumbini. Nitarudi tena usiku katika ile nyumba" Martin alijisemea.
Kwanini Mheshimiwa Lucas anamtafuta Elizabeth Neville? Mama Elizabeth anaongea na Felix, Felix ni nani? Elizabeth Neville katekwa na kina nani? Je Martin Hisia atafanikisha kupatikana kwa Elizabeth Neville? Maswali ni mengi majibu yapo katika simulizi hii..Elizabeth Nevvile