Elimu yangu darasa la saba, naomba ushauri

Mdau Makin

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
767
207
Habari wana jf wenzangu,
Natumai mu wazima wa afya...

Mimi ni binti mwenye elimu ya darasa la 7, Dhumuni langu ni kujiendeleza kielimu hasa kwa kujikita kusomea kozi yenye maket sokoni..

Je kwa uzoefu wako ktka soko la ajira unanishauri nisome kozi gani itakayo nifanikisha(mafanikio).?

Binafsi ninawazo la kujiendeleza chuo cha ufundi Veta...
Je wewe unanishauri ni fanye nini au kama ni kusoma unanishauri nisome kozi gani...?

mshana jr, Michael Mkwanzania
Watu8,
 
Inategemea na unapenda kuwa nani maishani. Ziko fani ambazo tayari zimekwisha wekewa vigezo tayari hivyo inakubidi uufuate utaratibu na utafute kwa kusoma sifa wanazozitaka. Fani hizo ni kama uhasibu.uhandisi.ugavi na manunuzi.nk
Ziko fani ambazo bado unaweza ingia na ukapata kazi ndani ya muda mfupi. Fani hizo ni kama hotel management.ufundi ngazi ya kati.kilimo. nk.
Hotel management mara nyingi ukianza na cheti haichukui muda utakuwa na diploma ndani ya muda ambao hata form 4 ungekuwa hujafika.
VETA nayo inategemea uelewa wako na utayari wa kujiajiri.
Vyote ni pumzi yako.mahali ulipo kama fursa zipo na uwezo wa kugharamia.
Dunia hii ina nafasi kwa kila mtu na sio kama wengi wanavyofikiri ni lazma uwe na degree !!
 
Habari wana jf wenzangu,
Natumai mu wazima wa afya...

Mimi ni binti mwenye elimu ya darasa la 7, Dhumuni langu ni kujiendeleza kielimu hasa kwa kujikita kusomea kozi yenye maket sokoni..

Je kwa uzoefu wako ktka soko la ajira unanishauri nisome kozi gani itakayo nifanikisha(mafanikio).?

Binafsi ninawazo la kujiendeleza chuo cha ufundi Veta...
Je wewe unanishauri ni fanye nini au kama ni kusoma unanishauri nisome kozi gani...?

mshana jr, Michael Mkwanzania
Watu8,
Dada nenda usome elimu ya sekondari kwa miaka miwili yaan kidato cha kwanza had I kile cha NNE na ukimaliza hapo soma kwa mwaka mmoja kidato cha tano na cta ,,,,,,,,baada ya hapo fikiria kwenda chuo
 
Back
Top Bottom