Uchaguzi 2020 Elimu ya uendeshaji mashauri ya uchaguzi ilete tija- Jaji Benhajj

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Benhajj Shaaban Masoud amewataka Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani kutumia vyema elimu ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya sheria na haki nchini.

1603084936467.png

Akifunga rasmi Mafunzo hayo hivi karibuni yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt Masoud aliwaeleza washiriki kwamba, imani ya wananchi ni kuwa, Mahakama ni mahali pa kupata haki, hivyo basi Maafisa wa Mahakama wanatakiwa kutambua muhimu walionao kwa wananchi wanaowahudumia.

“Ninawasihi sana kujiepusha na rushwa, kataeni rushwa, kemeeni rushwa na toeni elimu pale mnapopata nafasi na uwezo wa kufanya hivyo juu ya madhara ya rushwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi”

Aidha, aliendelea kwa kuwaomba Maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu anayopewa Jaji husika kwa wakati na pia kwa viwango bora.

Kwa upande mwingine, Mhe. Dkt Masoud aliwapongeza wawezeshaji wa mafunzo kwa jinsi walivyoendesha mafunzo hayo kwa umahiri mkubwa.
 
Hapo kwenye suala la kukataa rushwa hapo, hususani kwa hao aliokuwa akiwaasa...

Ngoja tuendelee tu na uchaguzi.
 
Back
Top Bottom