Elimu ya open university na soko la ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya open university na soko la ajira

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by CONSULT, May 8, 2011.

 1. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Wana jamii forum naomba ushauri wenu, kutaka kujua hadhi ya elimu huria kama inayotolewa na OPEN UNIVERSITY katika jamii yetu ya kitanzania aidha kwenye soko la ajira au mtazamo wa jamii kwa kulinganisha na elimu ya vyuo vingine kama vile UDSM, MZUNBE, UDOM.
   
 2. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Usipoteze muda na elimu kwa njia ya posta. Soma thread zilizotangulia utapata majibu kwa vile imejadiliwa katikahttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-
   
 3. R

  Rangi 2 Senior Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Elimu ya chuo kikuu huria ina viwango sawa tu na vyuo vingine. Siku zijazo elimu ya vyuo vikuu itachukua sura ya Open and distance learning (ODL).

  Ni ngumu kidogo kufanya Engineering pamoja na udaktari (watu na wanyama) lakini mengine yanawezekana kabisa...
   
 4. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Rangi unajidanganya kulinganisha distance learning na elimu ya full time vyuoni. Baada ya huu tandawazi hata ma PHD yameongezeka nchini ukiuliza wamesoma lini wanakuambia kwa internet.
   
 5. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli hapa ni jamvini mbona kuna watu wengi tu wamesoma open na wanafanya sehemu za maana tu na mbona pia kuna vyuo fulani watu wamesoma full time na wameshindwa kuthibitisha first class zao katika soko la ajira? Mimi nadhani kikubwa ni wewe ubongo wako unavyoufanya upokee vitu unavyosoma maana kama ni ulipuaji kila sehemu kuna ulipuaji wakuu. wakuu tujifunze kuelimika sio kupata vyeti na kuanza kulalamika chuo gani kinafaa kwa soko lipi, Hata hao wa internet nao wamejipenyeza kuleta ushindani na ndio maanabadala ya kushindana tumebaki kulalamika kila kukicha ukizingatia sasa tunaelekea soko la ajira la afrika mashariki. Tafakari na chukua hatua
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,032
  Likes Received: 3,056
  Trophy Points: 280
  Kaka L'mour kajibu vzuri sana...usianze kudanganywa na majina ya vyuo na kama ingelikuwa miaka5 iliyopita ningelikwambia usiende OUT lakn kwa sahv,imeadvance sana kuna kozi kama CL haikuwa inafundishwa,sahv ipo,hawakuwa na class tests/exams,sahv wanazo,bnafsi mie UD nilifundishwa psycology na mwenye bachera ya OUT ...nenda kasome
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Usidanganye watu bwana kuna wengine tuliwahi kuwa pale kwa capacity fulani hivi, ni upuuzi mtupu. Wastage of time unless unabiashara yako au mwanasiasa unataka uwe unataka qualification bila kuwaza kichwani unanini? Mie mwenyewe nilivyopitia tundiko lako nikabaini kwanini ilibidi ufundishwe na mwanafunzi wa OUT badala ya kukamata vitabu na kusoma.
   
 8. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kwa kila learning mode ina methodologies zake na objectives zake. Kwa out, hakuna tatizo. Kila kitu katika mfumo wa vyuo vyote hapa nchini kinaongozwa na kusimamiwa na tz commission of universities, tcu. Namaanisha wanapitia course outlines, study materials, na uwezo wa chuo chenyewe.
  Kwahili out haina tofauti na vyuo vingine.
  Suala la kuvilinganisha vyuo lina mitazamo tofauti inayojengwa na experience ya mtu husika.
  Uwezo wa mwanafunzi hutofautiana kulingana na chuo alichosoma but mara nyingi juhudi/initiatives za kukabiliana na changamoto za kujijengea uwezo/competency ni za mwanafunzi.
  Ninatakwimu za idadi kubwa ya wanafunzi waliosoma out na kufanikiwa katika nyanja na kazi mbalimbali hapa nchini.

  Tutachagua sana bucha lakini nyama ni ileile na mpishi ni wewe!!
  I submit
   
 9. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kama tayari upo kwenye system soma lkn kama bado hapana, mimi nimewaona watu wazima wengi sana waliosoma OUT ukweli walikuwa wanafanyiwa kazi za chuo na vijana, na ndio maana unaona kina kilango nao sasa hivi wana nondo
   
 10. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Nawashukuru sana kwa mawazo yenu.
   
 11. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kusoma chuo si kwamba you only absorb the materials that are delivered by instructors. unatakiwa kutazama mijadala, kusoma courses mbalimbali ambazo zitakuongezea skills, kujua vitu muhimu kama english, presentations etc. kuna mdogo wangu alikuwa anasoma pale OUT, kwasababu anamuda mchana akaenda chuo cha kodi akasoma certificate ya clearing and forwarding, akaomba kazi bandari akapata fasta na akapiga sana hela huku akiwa anajisomea sana night na week end....he is graduating this year. ulimwengu wa kukaa chuo bwenini na kula kantini unaisha. kazi na shule..... kikubwa nikuwa na tabia ya kusoma vitabu maana kuna libraries nyingi sana kwa dsm kama maktaba ya taifa, udsm, soma book shop victoria, palepale OUT wanayo...plenty of them.
  jijue wewe upoje ndo uamue usome wapi.
  i submit
   
 12. M

  Mr Mayunga JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tuna TCU sasa,sio kabla ya 1995 ndiyo tulikua tunahoji hivyo.
   
 13. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  umenikosha mkuu.
   
 14. m

  master gland Senior Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  OUT ni chuo kama vyuo vingine tena kama una mishe zingine unazifanya na kitabu kinaenda na wale wanaomaliza undergraduates OUT MTELEMKO kwa POSTGRADUATES msipoteshe kwa msioijua OUT ila kwa wavivu wa kusearch information wataona ni mzigo pale OUT unapata guidlines tu hivyo kama uta graduate kwa efforts zako unakuwa nondo mbaya hata kwenye masters unapewa first priority ukicompare na wa convetion NJIA NI TFAUTI ILA SAFARI NI MOJA KINACHOMATA NI GPA TU WANA JF ELIMU
   
Loading...