mcndomba maprosoo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 225
- 94
Kwa sasa vituo vingi vya kuuzia mafuta nchini vimefungwa mashine zinazotoa risiti automatically.
Changamoto niliyoiona ni uwepo wa elimu ndogo inayohusu kumpa risiti mteja ama mteja kuomba risiti baada ya kupata huduma.
Hii imekuwa ikijitokeza mara nyingi baada ya mteja kupata huduma, muuzaji mafuta hakati risiti ambayo tayari inakuwa imetoka kwenye mashine na kumpa mteja.
aidha, kuna baadhi ya wateja pia ambao hawaoni ulazima wa kuomba ama kuchukua risiti hata kama zinakuwa tayari; na mara nyingine karatasi za kuchapishia risiti zinakuwa zimeisha kwenye mashine pasipo kurudishia zingine.
Ni muhimu mamlaka husika zikaongeza elimu ya kutoa/kuomba/kuchukua risiti baada ya kutoa/kupata huduma. Kwa kufanya hivyo kutaongeza hamasa ya kuona kuwa kodi ni kwa maendeleo ya taifa.
Asante
Ni mimi mlipa kodi