Elimu ya bongo

Yuda

Member
Sep 20, 2011
6
1
ndugu wadau wa Elimu Tz, hii sasa inatisha mno kwani pamoja nakuwa na bodi mpya ya elimu lakini hamna ambacho kitaenda kufanyika kwani mwaka huu wanasema kuwa mkopo haitatolewa kwa waombaji wa sifa linganishi (Equivalent Qualification) ni bora wangetuambia tusiombe kwa kupitia ile System yao kuliko sasa hivi tunaambiwa kuwa hakuna mkopo kwa watu hawa, hivi hizi sheria wanazitoa wapi hawa wanaobuni mambo ambayo yanaleta kwa Taifa.

mimi ninachotaka kuwataarifu kuwa warekebishe huoo utaratibu ambao hauna tija kwa kizazi hiki kigumu, tumepiga simu bodi ya mkopo na wengine wameenda kuuliza wamepewa majibu hayohayo ya kutopewa mkopo. je, hawa watu waende wapi? kama mpango wenu kwa Sayansi na Walimu na Manesi wanataka wasome ili wawe kwenye Level nzuri katika taifa hili, kwani hawa watu wanauzoefu tayari wa vitu vingi kwa hiyo wakiwezeshwa wataleta tija kubwa sana katika Nchi hii. Hebu tujaribu kuwaangalia watu hawa wasionekane wameachwa na Nchi ambayo inategemea kuazimisha Miaka 50 ya uhuru.

bodi ya Mikopo, Mhe. Waziri wa dhamana hiyo, waziri mkuu anaglieni hilo suala hilo kwa ukaribu zaidi.

Ni Mimi mwanachi,
IRINGA
 
Kweli hii inasikitisha na inadidimiza juhudi za wananchi katika kujiendeleza kitaaluma.Nadhani kuna haja ya kuvunja bodi hii kwani inafanya mambo kisiasa bila kujua adhari zake kwa taifa letu.
Mungu Ibariki Tz
 
Back
Top Bottom