Elimu sio Siasa, Nyuma ya pazia Sekondari ya Mt. Francis Mbeya

Umenikumbusha mbali teacher Rand kanifundisha tuition hapo Meta huyu teacher hata kama huipendi chemistry atafanya uipende na kuielewa ni comedy sana harafu anjua mbinu za ufundishaji. Anatembelea gongo lakini anakwambia disco anaenda kama kama kawaida atakuonyesha mbwembwe za kucheza hapo mtabaki vicheko tu, kwa kifupi huwezi kudoji kipindi chake
Mi mwalimu Mageta (Second master) alinifundisha Commerce na Mwasalanga alinifundisha Accountancy hapohapo kitaa cha Meta Secondary miaka hiyo niko Advance
 
Nakubaliana wewe kabisa. Tuache kulalamika ,tujipange. Bahati mbaya sana waislam ni wataalam wa kulalamika badala ya kujua ni wapi waliteleza na wajipange. Wao wanadhani kuna mtu atawasikia
Niujinga tu wakufikiri ambao wanao ... hata ulaya wa roman nao kuna kipindi walitawaliwa sana na jamii ya watu wa kiislam toka ottoman empire .... so wajipange

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eee man sahivi niko kitaa napambana na life....Mzee Mng'ong'o pale getini alikuwa ananiboa sana na vile vikadi vya kuingilia
Unawakumbuka wengi aise hadi huyu mzee, alishawahi nichomesha kwa Mageta nilipokuwa namuomba nipite mana gatepass ilikua ishaisha muda nilichezea stiki na kufyatua tofari mia
 
Unawakumbuka wengi aise hadi huyu mzee, alishawahi nichomesha kwa Mageta nilipokuwa namuomba nipite mana gatepass ilikua ishaisha muda nilichezea stiki na kufyatua tofari mia
Hahahaha ni noma mzee...Mageta alizoea kusema ''nakukong'oli'' akikumaindi class anakwambia uweke miguu ukutani alafu mikono chini...hapo lazima uombe poo
 
Wakati wamiliki wa St.Francis wanatumia pesa nyingi kuwekeza kwenye Elimu bora, Jiwe yeye anatumia pesa nyingi kununua mandege yanayodaiwa kuwa mabovu, kununua wapinzani, kujenga Kiwanja cha ndege Chato nk. Sasa kila mtu anavuna alichokipanda.
Brother u said all....unanikumbusha usemi mmoja unasema " ukitaka kujua potential ya nchi fulani kimaendeleo huko mbeleni angalia serikali ya nchi husika kwa kiasi gani inawekeza kwa watoto wake". So far elimu yetu ipo kwenye hali mbaya sana lakini si magufuli wala ccm wanaojali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa alivyokuwa na roho mbaya ya kimasikini anakwambia waliosoma private schools mkopo haupati hata na single digit yako
 
Shule za private kwa Watoto wasio na nidhamu Fimbo yao NI kufukuza, Shule za Serikali zilikuwa zinatumika Fimbo kuchapa wasio na nizamu ambazo Sasa ZIMEPIGWA MARUFUKU. Unategemea huyu mwanafunzi atanyookaje?
Hapa una hoja.
===
Signature yako nayo matata, Unasema:
  • USITOE MACHOZI TOA VYETI KAMA SISI TULIVYOHAKIKIWA .HAKI SAWA KWA WOTE
 
Wewe umedandia gari kwa mbele.

Huyu niliye mkwoti amedai wanafunzi wa ST FRANSIS huwa wanafeli sana mitihani ya kidato cha sita sasa nikamuuliza kwa nini wanafeli mitihani ya kidato cha sita? Sijauliza kuhusu hiyo Iyunga yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
swali lako lilikuwa lina direction mbili (kwa st.francis and Iyunga) but pale St.fancis hakuna A-level,that is why it has been directed to Iyunga.
but OK just splash it den kp on moving ahead.
 
Mkuu labda tu nikwambie jambo moja lakukusaidia " Tangia dunia hii ianze kuishi watu ..mfumo wa maisha unalazimisha jamii ya watu fulani kuwatawala watu wengine ... (haswaa jamii ya wasomi wengi kuwatawala wasio soma), hawa watawala wanaweza kuwa ni Wakabila fulani .nchi/taifa .Dini .. ..na nikwambie tu kila (dini .kabila .nchi .) yoyote ile unayoijua wewe duniani lengo lake kuu ni kuhakikisha inakuwa na utawala .. na inapoupata utawala huo haiwezi kuwa neutral ni lazima itakuwa na mfumo kandamizi kwa watu wa nchi .kabila dini fulani " ili wao waweze kutawala " .... hivyo basi kama mimi .wewe.na mwingine/wengine tunaona kwamba RC ndio wanaotawala mfumo mzima wa maisha hatupaswi kulia lia we must admit that" wenzetu walijipanga vyema ili waweze kuwa watawala " wakati sisi tukiwa bado tumelala ..na huo ndio mfumo wa maisha ulivyo najinsi ambavyo unapaswa kuwa (mtawala +mtawaliwa = maendeleo mengi kwa watawala /maendeleo kiasi au hafifu kabisa kwa watawaliwa )"...............

Hivyo basi ninini kifanyike ili watu wa dini " makabila .nchi .nyingine ziweze kuwa na watawala " Wanapaswa kujipanga na wao ili waweze kuwa na mikakati itakayoweza kuwatoa katika shimo la kutawaliwa ambalo wanaishi kwa sasa ili na wao waweze kuwa watawala. Na hakuna mbinu nyingine ya wao kuweza kufika hapo zaidi ya kuzihimiza jamii za watu wao ziweze kuwa na wito mkubwa wa elimu .. wahakikishe jamii yao inaipenda elimu kuliko hata kula Jamii yao ikisha elimika itaanza kuchukia kutawaliwa .. na taratibu itaanza kuutafuta ukombozi wakuwafanya wawe watawala " sio safari rahisi kuweza kuifikia hiyo hatima lakini inawezekana ...





Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema vyema boss kila kitu kinaitaji gharama hadi kukifikia... mara nying wanasemwa wachagga wametawala kona zote ni kweli kabisa elimu na usatarabu wakusoma ulitangulia kufika kwao..me ni mtu wa mbeya sina interest kwa lolote katika hili..ivyo ivyo kila dini inatakiwa kuhimizawa watu wake kusoma kwa bidii sana ili waweze kutawala bila ivo tutaishia kulalamika
 
Mimi nimelelewa na kukulia kwenye mazingira ya uislam ijapo kuwa now sifungamani na dini yoyote ... lakini huo niliokwambia ndio ukweli ... sometimes yatupasa kuongea ukweli hata kama utakuwa hauna maslahi na sisi/ hata kama utakuwa unauma'' unapo utambua udhaifu wako ndio hatua ya mwanzo kabisa itakayo weza kukufanya uanze kujifunza/kubadilika"..........., mfumo wa dunia unamtaka mtawala na mtawaliwa. So kazi nikwetu sisi Binaadamu kuchagua kuwa sehemu moja wapo katika hayo makundi mawili
Umesema vyema boss kila kitu kinaitaji gharama hadi kukifikia... mara nying wanasemwa wachagga wametawala kona zote ni kweli kabisa elimu na usatarabu wakusoma ulitangulia kufika kwao..me ni mtu wa mbeya si interest kwa lolote katika hili..ivyo ivyo kila dini inatakiwa kuzawa watu wake kusoma kwa bidii sana ili waweze kutawala bila ivo tutaishia kulalamika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KIBURI CHA KUSHUGHULIKIA MATATIZO NA MALALAMIKO YA WAALIMU NDO CHANZO CHA TATIZO.

Maafisa Utumishi wangi NI miungu watu, Hawashughuriki na matatizo ya mwalimu kwa wakati. Matokeo Yake mwalimu anashinda barabarani kiguu na njia ,Jua lake, Mvua Yake kumfuatilia stahiki zake Halmashauri.Na akifika anaambiwa Njoo kesho Leo siyo siku ya kusikiliza madai ya waalimu Leo NI siku ya wansotaka kwenda kulipa benki. Na siku uliyoambiwa uende ,UKIENDA utaambiwa Afsa Utumishi hawapo wote, Mmoja likizo, Mmoja kasafiri mmoja katika tu au hajafika. Mwalimu anakaa kwenye benchi wee mwisho Anaamua Kaondoka huku akiwa na huzuni kubwa. Anaamua kwenda wiki inayofuata akifika anaambiwa Afsa Utumishi kaenda kunywa chai, Anaamua kumsubiria akifika Afsa Utumishi anamwambia subiria kidogo naingia kwenye kikao. Akitoka kwenye kikao ooh samahani mtandao haupo Njoo wiki ijayo, Anaamua kupanga wiki ijayo , Wiki ijayo anapokuja Tena ooh swala lako lipo makao makuu Basi.Afsa Utumishi hawezi hata kunyanyua Simu kuwapinga wenzake huko makao makuu ili kujua suala la huyu mwalimu limefikia wapi Wala. kwa sababu halimhusu. Mwalimu anaondoka kwa matumaini labda mwezi ujao litashughurikiwa Lakini atakaporudi Tena jibu NI Hilo Hilo atapewa suala lako tulidhakwambia lipo makao makuu. NA NENO MAKAO MAKUU LIMEKUWA NI CHAKA LA KUJIFICHIA MAAFISA UTUMISHI KUWAJIBU WAALIMU MASUALA YAO YAPO MAKAO MAKUU. UNAJIULIZA KWANINI HAWAPIGI HATA SIMU ILI MWALIMU APEWE MAJIBU MOJA KWA MOJA NA HUYO ALIYEKO MAKAO MAKUU?

KWANINI KUMZUNGUSHA MWALIMU BILA SABABU ZA MSINGI KIASI HIKI? UNAPOMZUNGUSHA MWALIMU BILA KUMPA HUDUMA KUMBUKA VIPINDI VYAKE WATOTO HAWASOMI HILO PIA MLIJUE WANAOASIRIKA ZAIDI NI WATOTO KUKOSA VIPINDI VYA MWALIMU NA KWA MWALIMU ANAPOTEZA PESA ZA NAURI NA UNAMWACHIA MAUMIVU YA KISAIKOLOJIA KITU AMBACHO KITAMFANYA ASIFUNDISHE VIZURI DARASANI.

Serikali imekalia kuunda tume ili Hali matatizo yanajulikana yapo wapi.Bora hizo pesa za tume zingekuwa zinatumika kutatua matatizo ya waalimu.

Mfano, Vitambulisho waalimu wananunua kwa sh 10000. NI jukumu la mwajiri kumpa kitambulisho. Lakini hawatoi. Mwalimu anataka kwenda kuchukua mkopo anaambiwa leta kitambulisho Cha kazi ambacho Hana . Akienda kwa mwajiri anaambiwa labda ajitengenezee na Kuna mtu huwa anatengeneza Vitambulisho kwa sh 10000 nenda akakutengenezee ulete tukugongee muhuri.

Wakati haya anafanyiwa mwalimu wa Serikali kwa upande wa mwalimu wa shule binafsi Yeye katulia tulii kwenye shule Yake ,Hana madai yoyote anayomdai mwajiri wake, Anachojua Yeye NI ratiba ya kuamka na kwenda Darasani Hana ratiba ya kuzunguka na bahasha kumsaka mwajiri wake et anampelekea MALALAMIKO ya madai.
Halafu mtu anataka matokeo ya Shule binafsi na ya Serikali yawe sawa.

Mishahara midogo

Madai ya pesa za Nauri.

Kutokuwapandisha madaraja kwa wakati.

Kutokutolewa posho za mazingira magumu.

Waalimu Kutokujengewa makazi na Hivyo wanasafiri KUTOKA mbali Hadi kuifikia shule.

Mrundikano wa wanafunzi katika Darasa moja.

Kupunguzwa kwa marks za ufaulu DARASA LA SABA.NA HIVYO WENGI WAMEKUWA WANASUKUMIZWA TU KWENDA SEKONDARI BILA KUANGALIA VIWANGO BORA VYA UFAULU WAO.IMEFIKIA SASA WANAPELEKWA HATA WASIOJUA KUSOMA FORM 1. SASA MWALIMU WA SEKONDARI ATAFANYA MIUJIZA GANI ILI HUYU MTOTO AFAULU IKIWA KUSOMA NA KUANDIKA JINA LAKE TU NI SHIDA UNATEGEMEA ATAFAULU HUYU?

Kutokuwepo kwa mitihani ya kuwachuja wanafunzi pindi anapotoka Darasa moja kwenda jingine Kama zifanyavyo shule za private.

Shule za private kwa Watoto wasio na nidhamu Fimbo yao NI kufukuza, Shule za Serikali zilikuwa zinatumika Fimbo kuchapa wasio na nizamu ambazo Sasa ZIMEPIGWA MARUFUKU. Unategemea huyu mwanafunzi atanyookaje?

Mlundikano wa wanafunzi Darasa moja kuwa na wanafunzi zaidi ya 60 ... kwa shule za Serikali ili Hali za private Darasa moja wanafunzi 35.

Bila jitihada za kutosha kuyatatua hayo na kukifanya hayaonwi , Halafu tunasubiria matokeo ya Shule binafsi yatakuja kuwa sawa na ya Serikali NI SAWA na kusema ipo siku maji yatapanda Mlimani.
Labda kwa MIUJIZA ya MUNGU.
Mkuu hii comment ilibidi iwe na uzi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom