Elimu ni ufunguo wa maisha

Elimu ni ufunguo wa maisha

Mema Tanzania

Member
Joined
Feb 23, 2020
Posts
66
Reaction score
65
"Elimu ni ufunguo wa maisha". Moja ya msemo ambao tumekuwa tukiusikia tangu awali. Ni kiasi gani msemo huu umeakisi maisha yako baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu?
 
Unazungumzia Elimu au Elimu iliyo rasimishwa.

maana naona chuo, darasa la tatu.
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha". Moja ya msemo ambao tumekuwa tukiusikia tangu awali. Ni kiasi gani msemo huu umeakisi maisha yako baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu?
Elimu ni ufunguo wa maisha.

Watu wanatafsiri "shule na vyuo ni ufunguo wa maisha"

Shule ama vyuo sio ufunguo wa maisha,bali elimu,kile unachokipata ndio ufunguo wa maisha.

Mfano sisi tunasoma leo kuhusu umeme shuleni hiyo ni elimu,Tukisoma kuhusu afya ya mwanadamu hiyo ni elimu.

Umeme ni kweli umeleta ufunguo wa maisha kwa kuwezesha urahisi wa mambo mbalimbali.

Afya kusomea udaktari wa fani mbalimbali kweli imeleta ufunguo wa maisha kwa kurahisisha kuyatibu magonjwa mbalimbali na kuokoa uhai wa watu.

Elimu ni ufunguo wa maisha.
 
Acha hao, wachaga wengi walio na mafanikio makubwa sahv wengi waliishia la 4 au hawakusoma kabisa
Ipo tofauti Kati ya kusoma darasani kisha unapewa vyeti na kusoma maisha kisha unapata uzoefu wa maisha
 
Ipo tofauti Kati ya kusoma darasani kisha unapewa vyeti na kusoma maisha kisha unapata uzoefu wa maisha

Kwahiyo tu-focus wapi? Watoto kusoma ili kupata vyeti wakati hamna ajira au tuwape elimu ya maisha?
 
We upo darasani miaka 20 mwenzake yupo kwenye biashara miaka 20 huwezi mkuta ktk maisha labda umalize chuo upite bila kupingwa au upate nafasi ya kufanya ufisadi
 
Kwahiyo tu-focus wapi? Watoto kusoma ili kupata vyeti wakati hamna ajira au tuwape elimu ya maisha?
Balance vyote,ila muhimu elimu ya awali amalize angalau sekondari Kisha akasomee fani iendanayo na kile akipendacho.

Kuna fani zingine ufanya vizuri zaidi ukipita darasani zingine si lzm mfano fundi garage,vyuma, ujenzi.
Ila ukichanganya elimu ya darasani na elimu ya mtaani unapata collabo matata ya kusonga mbele.
 
We upo darasani miaka 20 mwenzake yupo kwenye biashara miaka 20 huwezi mkuta ktk maisha labda umalize chuo upite bila kupingwa au upate nafasi ya kufanya ufisadi
Mbona wapo kibao mitaani tumekaa darasani miaka 20 tumerudi tumewakuta wako choka mbaya kitaa wameshazeeka na sasa tunapiga pesa wanakuja kuomba omba. Kwa maisha ya Mtanzania bado elimu ni ufunguo wa maisha kwa kiasi kikubwa sana.
 
Pana tajiri mmoja Mkubwa sana Nigeria ni motivation pia kuhusu ujasiliamali na mafanikio.Baada ya kumaliza masters ya uchumi UK akarudi nigeria amesaka ajira kwa miaka 10 bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa kabisa ikampelekea kwenye ulevi wa pombe chafu akiwa kapoteza kabisa matumaini.Pombe uunganisha urafiki hasa mkikutana vilabuni,akapata rafiki ambae ni mlevi mwenzake wakawa wanaishi wote maana hata uwezo wa kodi hakuwa nao.Yule mlevi aliishi kwa kutegemea kusukuma torori mjini lagosi kubebea watu mizigo uhakika wa kipato utegemea na wingi wa Kazi akipata utumia yote kesho atapata zingine,yule mlevi akawa akimshwishi mchumi waende wakasukume wote mkokotoni kuliko kukaa ndani bila Kazi,kwa shingo upande na hana jinsi mchumi ikabidi aweke masters pembeni akashika torori aibu pembeni asife njaa ajira zimegoma.Wakawa wanaenda wote aibu ikamtoka Kazi ikaingia damuni maana hel ya kula na kulewa sio shida tena uhakika upo, baada ya uzoefu na kuijua Kazi mchumi akaamua kusave akipata utumia robo zingine anasave bank alifanya Kazi ya torori na kusave ndani ya mwaka kwenda kuchungulia akaunti bank hakuamini pesa aliyoikuta ndo akafanya mtaji wa kuanzia kufungua biashara sababu uzoefu wa kuwabebea wafanyabiashara mizigo akafungua duka lake likafanya vizuri plus uchungu na nidhamu ya Kazi na hofu ya kurudi chini kwenye ulevi akafanya vizuri biashara ikakua akafungua maduka mengine na mengine mtaji ukakua akaanza biashara za kuchukua vitu nje ya nchi vinapotoka na kuuza kwenye maduka yake akajenga magodauni ya mizigo akawa ajenti Mkubwa na kuzidi kufungua biashara tele tele zikampa utajiri Mkubwa saana Nigeria.
Funzo hapa tunaona Masters holder amechanganya elimu mbili ya darasani kujua umuhimu wa saving na hofu ya kesho akiwa mgonjwa au mzee je ataendelea kusukuma torori?
Point kubwa hapa ni kwamba wengi waliokwenye hizi shughuli ndogo ndogo hawazioni Kama ni fursa wanazoweza zikuza Ili waje wawe wafanyabiashara wakubwa kupitia savings.
Hizi shughuli zenye kudharauliwa na wengi ukizifanya kwa malengo ni rahisi kufikia malengo yako.
 
Mbona wapo kibao mitaani tumekaa darasani miaka 20 tumerudi tumewakuta wako choka mbaya kitaa wameshazeeka na sasa tunapiga pesa wanakuja kuomba omba. Kwa maisha ya Mtanzania bado elimu ni ufunguo wa maisha kwa kiasi kikubwa sana.
True wamekalia almas bila kujua sababu ya elimu thus mwenye elimu uona fursa hizo
 
Fanya hivi peleka mtoto shule ..wakati yuko shule mchana live kuwa hakuna ajira. ..tumia mfumo wa wahindi

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

Mimi nampeleka shule akatoe ujinga + kujua lugha. Then namwandalia mazingira ya kuja ku-run shughuli zangu au kama anatalent yoyote nampa support kwa 100%. Mambo ya kusoma mpaka Chuo ni uoga wa maisha.
 
Acha hao, wachaga wengi walio na mafanikio makubwa sahv wengi waliishia la 4 au hawakusoma kabisa
Hio ya darasa la 4 ni elimu sio sawa na ambaye hajasoma kabisa.Elimu sio lazima itolewe darasani hata nje ya darasa.Watanzania wengi wana elimu ya nje ya darasa kama ufundi nyumba,ususi,kinyozi,uselemala nk.
Tuache kutafsiri sec,veta, University ndio elimu.Hizo ni elimu ya upili,juu nk.
katika zama za mtandao elimu sio kitu kigumu kama zamani, kila mtu anaweza kuipata tu bila hata kuhudhuria chuo ola cheti ndio kigumu kukipata mpaka taasisi zithibitishe.
nyumbani tunaishi na binti ambaye hajapitia shule, tulivyogundua hajui kusoma tumemfundisha kusoma na kuhesabu mpaka kajua, sasa tunataka kumfundisha kingereza.
Je Huyo ana elimu au hana?
 
Kujua kusoma na kuandika hatua kubwa sana hii
 
Back
Top Bottom