Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,623
- 8,427
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imesema itawasilisha hoja mahsusi bungeni wakati wa mkutano ujao wa Bunge kupinga ongezeko la asilimia sita kila mwaka katika deni la wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.
Mkutano ujao wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza Septemba 3, mwaka huu ukitanguliwa na vikao vya kamati za kudumu za chombo hicho cha kutunga sheria.
Vilevile, kambi hiyo imesema katika hoja yake hiyo, pia itapinga makato ya asilimia moja yanayofanywa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) dhidi ya wanufaika wa mikopo hiyo kwa ajili ya ada ya uendeshaji kwa kuwa serikali kila mwaka imekuwa ikitenga fungu maalum kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za bodi hiyo.
Kifungu 7.2.1.1 cha Mwongozo wa HESLB wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa Wanafunzi kinabainisha kuwa mnufaika wa mkopo wa bodi hiyo atalipa tozo ya kulinda thamani ya fedha ambayo itakatwa asilimia sita kwa mwaka tangu tarehe mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.
Pia, katika kifungu 7.2.1.2 cha mwongozo wake huo, HESLB inaeleza kuwa itakata asilimia moja ya ada ya uendeshaji kwa mwanafunzi mnufaika.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Susan Lyimo, alisema kambi yao imeamua kuwasilisha hoja bungeni kupinga makato hayo.
Alisema kuwa kabla hoja hiyo haijatua kwa Spika, ataiwasilisha kwanza kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ili kamati hiyo ambayo yeye ni mjumbe, iitake serikali kupeleka bungeni muswada wa kurekebisha Sheria Na. 9 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Mwaka 2004 ili vifungu vyenye makato hayo vifutwe.
"Serikali itambue kwamba HESLB na haifanyi biashara, bali inatoa huduma ya kuhakikisha watoto wanaotoka familia maskini wanapata elimu ya juu, lakini kwa hali ya sasa ya kuwaongeza deni wanufaika wa mikopo, hakuna haja ya kuwa bodi hiyo," Lyimo alisema na kueleza zaidi:
"Kama wanataka kufanya biashara, basi jukumu hili lisifanywe na HESLB, liachwe kwa benki. Kumtoza mnufaika wa mkopo wa elimu penalti ya asilimia 10 ya mkopo kisha tozo ya asilimia sita ya mkopo kila mwaka na asilimia moja kwa ajili ya uendeshaji si haki.
"Inakuwa ngumu kwa wanufaika kumaliza kulipa deni kwa sababu linaongezeka kila mwaka hata kama wanalilipa, vinginevyo ndugu waungane na mnufaika kulipa deni lote kwa siku moja.
"Kitafika kipindi vijana wetu hawa itakuwa shida hata kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa sababu watahofu kuoa au kuolewa na mtu mwenye deni la HESLB ambalo hata ukianza kulilipa haliishi.
"Makato yenyewe ya marejesho ni asilimia 15 ya mshahara wa kila mwezi, huyo anayekatwa ana makato mengine ya bima ya afya, kodi ya serikali, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii... yaani karibu asilimia 50 ya mshahara wake unaishia kwenye makato ya taasisi za serikali, huyu mtoto wa maskini ataishije?"
Mbunge huyo wa Viti Maalum (Chadema) kwa kutambua uzito wa suala hilo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeona njia nzuri ya kutatua changamoto zilizojitokeza ni kuwasilisha hoja maalum bungeni kuitaka serikali kufanya marekebisho tena katika sheria iliyoanzisha HESLB.
"Hizi penalti za asilimia 10 na tozo ya asilimia moja nazo ni tatizo. Hakuna nchi nyingine inayofanya hivi. HESLB inatengewa fedha na serikali kwa ajili ya uendeshaji na watumishi wake wanalipwa mshahara na serikali.
"Pia tunaona hakuna haja kupiga penalti mnufaika kwa sababu hali halisi ya ajira nchini inajulikana. Kikubwa, bodi iwe na mfumo mzuri wa kuwatambua wanufaika," alishauri.
KAULI YA WIZARA
Akizungumza na Nipashe jana kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Willian Ole Nasha, alikiri kupokea malalamiko ya wanufaika kuhusu kuwapo kwa uonevu katika urejeshaji wa mikopo hiyo na kwamba wizara yake inaendelea kuyafanyia kazi.
Hata hivyo, Ole Nasha alisema baadhi ya changamoto zilizoibuka kuhusu urejeshaji wa mikopo hiyo, utatuzi wake unahitaji kurejea bungeni kufanya marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Mwaka 2004.
"Tumesikia malalamiko na siyo kwamba hatujayapata, tumeyapata na tunayatolea ufafanuzi na kusambaza taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari," alisema.
Ole Nasha alisema serikali ni sikivu na kwamba kwa sasa inafanya mapitio ya mfumo mzima wa mikopo hiyo ili kuangalia njia bora ya kutatua changamoto zote zilizopo.
“Tunahitaji kuendelea kutoa elimu ingawa inafahamika kwa sababu mkataba wa mikopo umeeleza kila kitu, tunaendelea kutoa elimu ili watu wafahamu zaidi na kila mwaka tunafanyia marekebisho mwongozo wa mikopo.
"Kuna mambo ya kisheria ambayo hatuwezi kuyafanyia marekebisho mpaka sheria ikabadilishwe bungeni, lakini yale ambayo yapo chini ya kanuni zetu tunafanyia marekebisho kila wakati tunapoona kuna haja kufanya hivyo," alisema.
Naibu waziri huyo alisema tozo ya asilimia sita imewekwa kwa lengo la kulinda thamani ya fedha ili kusaidia wanafunzi wengine wanaotaka kusoma kwa kupewa mkopo na Serikali.
“Tozo ya kutunza thamani inafanya ile thamani ya mkopo wako isipotee, yaani usiwe umekukopesha Sh. milioni moja na wewe uje urudishe milioni moja baada ya miaka saba, haitakuja kutusaidia, lengo la serikali siyo kukusanya fedha, bali kutunza thamani ya fedha," alisema.
Ole Nasha alibainisha kuwa uzoefu wa wizara yake unaonesha kuwa ukiacha miezi 24 iliyotolewa na HESLB kwa wanufaika kuanza kuhesabiwa muda wa kulipa deni, mdaiwa anaweza kumaliza deni lake ndani ya miaka 10 kama hatapigwa penalti.
“Utafiti unaonyesha kuwa inachukua miaka minne hadi 10 mnufaika kumaliza kulipa deni lake endapo ataanza kulipa kwa wakati," Ole Nasha alisema.
Hata hivyo, utafiti huo unakinzana na takwimu za urejeshaji mkopo za HESLB ambazo zinaonesha kuwa kati ya wanufaika 479,779 waliopatiwa mikopo hiyo tangu serikali ilipoanza kuitoa mwaka 1994, ni wanufaika 11,214 (asilimia 2.3) waliofanikiwa kumaliza kulipa madeni yao.
Pia, wanufaika wa mikopo hiyo waliozungumza na Nipashe wiki iliyopita, walidai wanufaika wengi wa mikopo hiyo walioanza kuilipa, wameshindwa kumaliza urejeshaji kutokana na deni kuongezeka kwa asilimia sita kila mwaka.
“Wito wetu ni kwamba ukichukua ule mkopo , tukijenga ustaarabu wa kulipa, inawezekana wanafunzi wote wanaoenda chuo kikuu, wanaohitaji mikopo wapate kwa sababu ni hela ambayo ipo kwenye mzunguko.
“Haimaanishi kwamba sisi kama wizara hatufanyii kazi changamoto zinazojitokeza, tukipata changamoto tunatoa elimu kuhusu hali ilivyo sasa na tukiona kuna haja ya kurekebisha, pale tunapoona tunaweza tunafanya, na mengine kama haya (malalamiko ya uonevu katika urejeshaji mkopo), inabidi turudi bungeni," Ole Nasha alisema.
Mara ya mwisho Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kufanyiwa marekebisho ilikuwa Novemba 2016, serikali ilipowasilisha bungeni muswada ambao pamoja na mambo mengine, ulipendekeza mnufaika wa mkopo arejeshe mkopo kwa makato si chini ya asilimia 15 ya mshahara wake wa kila mwezi badala ya asilimia nane iliyokuwa awali.