ELIMU: Mikopo Elimu ya Juu kaa la moto

ELIMU: Mikopo Elimu ya Juu kaa la moto

Kwa nchi hii mjadala mzito kama huu utaishia kwenye social media kama hivi na ukifika bungeni kidogo utasomwa ILA sasa kwenye kupitishwa ndo shiiida, walio wengi watauponda na utakufa kifo chake.

Kwa wale waliopevuka (mabeberu) issue kama hii pale inapoingizwa ndani ya jumba la kutungia sheria huku nje wasomi kutoka familia masikini na wananchi wanaripuka Nje ya mjengo mpaka kieleweke.
 
Uzi una mwendo Wa kinyonga, ujinga tulikuwa nao tunaojiita watetezi wasikini nyuzi kama hizi hatuzioni, ila kutetea ujinga wa wanasiasa na wanaharakati wanaotetea matumbo yao, nyuzi kama hizi zinazo ongelea masrahi mapana ya jamii za wanachi masikini hata hatuwaoni. Kutwa kumuongelea pascal mayala kama kweli ni watetezi Wa wanyonge, ila kwenye nyuzi kama hizi zinazohusu na kugusa maslai mapana ya jamii yanaojidai kuwaongelea hata hatuwaoni.
 
Well said, hata cost za kukodi majengo ielekezwe kwenye mikopo
Majitu yalisomeshwa bure enzi za Nyerere leo yanataka kuwakamua wajukuu wa wenzao, na hakunajitihada zozote za kulinda ajira za ndani kwa kucontrol bidhaa toka China, ili basi walau viwanda vya ndani viweze kuchipuka, watu wapate ajira za kueleweka na kulipa hilo deni.., damn it.

Kama HESLB inataka kujiendesha kama benki na sio taasisi ya kudumia watoto wa masikini basi wakasajiliwe BOT na wapewe leseni ya kufanya biashara hiyo na walipe kodi stahiki TRA kwa biashara hiyo, otjerwise hili jukumu la kutoa hii mikopo ya kibiashara waachiwe NMB, CRDB na wengine wenye uwezo, hizo pesa serikali inazotenga kulipa mishahara ya watumishi HESLB ziende kutumika kwingine penye uhitaji, hakuna sababu ya kuwa na taasisi ya serikali inayofanya kazi ambazo ni duplicate ya zinazoweza kufanywa na mabenki.., watu hawakatai kufanyika kwa hayo marejesho, shida ni hizo 6% na 1% za kuongezaka eti kila mwaka?!!!!
 
Nilisaini kukatwa 8% but now nakatwa 15% bila taarifa, kila mwaka wanatoa 6% na 1%. Kwa hali hii mpaka unastaafu bado unakatwa tu na bodi
ONLY IN TANZANIA
Shida yenu mmeamua kukubaliana hiyo hali. Hakuna hata mmoja aliyeenda mahakamani kuomba tafsiri za makubaliano mliyokuwa nayo hapo awali.

Hata kwenye mabenki si dhani kama haya mambo yapo,leo unakopa kwa asilimia 9,ghafla kesho wanakwambia 15.

Kila mtu angepeleka malalamiko kwenye vyombo vya usuruhishi/ mahakamani leo pengine msingekuwa mnalia lia.
 
Shida yenu mmeamua kukubaliana hiyo hali. Hakuna hata mmoja aliyeenda mahakamani kuomba tafsiri za makubaliano mliyokuwa nayo hapo awali.

Hata kwenye mabenki si dhani kama haya mambo yapo,leo unakopa kwa asilimia 9,ghafla kesho wanakwambia 15.

Kila mtu angepeleka malalamiko kwenye vyombo vya usuruhishi/ mahakamani leo pengine msingekuwa mnalia lia.
Hata hapa ni mahakamani pia, hebu imagine huu uzi ungekuwa walau na views 50k na comments walau page 20, we unafikiri ingekuwaje? Tatizo wengi wetu ni mafunza yamejaa kichwani, wakiona nyuzi za Diamond kutuhumiwa ushoga na unakuta views 200k ndani ya nusu saa, mambo ya msingi kama haya hata page 3 hatufiki, siku nzima, lazima tuburuzwe tu, kwa akili za kijinga kama hizi..!!
 
Tukiwa tunaongea kuhusu tanzania tunayo ijua wanatuita majina mengi. Tukiambiwa elimu yetu haina msaada kwa jamii tunarusha ngumi. Wasomi wetu kutwa kulalamikia serikali mala serikali haija tuajiri, na walio ajiliwa kutwa kulalamika mishahara imechelewa, yaani wasomi ndiyo wamekuwa watu wakulalamika mitandaoni nyuzi zisizo kuwa na kichwa wala miguu, kwenye nyuzi kama hizi ambazo zinaongelea mustabari wao hawaonekani. Kwa staili hii kweli we can pay back to our community!!
Tusiruhusu mavampire kama haya ya HESLB. Sio mnufaika Wa mkopo ila naona kama hili jini lipo kwa ajili ya kuwamaliza wanainchi wanyonge.
 
Hii ndio faida ya kuwa na upinzani sio maccm wanaunga mkono kila kitu hata mauaji kwa Watanzania wenzao. Majinga kabisa haya majitu.
Sijui tumelogwa na nani!! Mida mingine ushabiki wenu Wa kisiasa muwe munauweka pembeni, wanufaika Wa hii mikopo, wapo Wa ccm, ukawa na wasiokuwa na mlengo wowote. Kumbuka asilimia kubwa ya wanufaika wazazi wao ni masikini. Sasa unapoleta siasa kwenye maswala kama haya tunashindwa kukuelewa mkuu.
 
Hii ndio faida ya kuwa na upinzani sio maccm wanaunga mkono kila kitu hata mauaji kwa Watanzania wenzao. Majinga kabisa haya majitu.
Tuone nini kitatokea huko bungeni, huu unyonyaji wa mtoto wa masikini kwa kiwango cha SGR haukubaliki kwamwe..!!
 
Mkuu Retired, sio hawaoni, bali kuna macho ya aina 3, yaani tuna makundi matatu ya watu with three types of visions
  1. The Blind- hawa hawaoni kitu, they don't see anything, hawa please lets leave them alone.
  2. The Myopic and Unidirectional- hawa macho yao ni myopia, wanauwezo wa kuona hadi mwisho tuu wa pua zao, na vision yao ni upande mmoja tuu, wakiwa ndani ya box wao wanaona humu walimo ndio mwisho, hawa wanaona mazuri tuu, wakiwa nje wanaishia kuona kwa nje wanaona mabaya tuu, haoni upande mwingine wowote.
  3. The Objective, observers and multi-directional, hawa hawako ndani ya box, they are watching from a distance lakini macho yao yanaonda ndani ya box, nje ya box na difference sides na directions, hawa wako very objective kwa kuona both sides of the coin, wakiona mabaya, wanakosoa, wakiona mazuri wanapongeza, haiwezi uwe unana mabaya tuu mazuri huoni, au unaona mazuri tuu na kusifia tuu yaani praise team, kukifanyika mabaya wewe huoni. This is where I belong!. Mimi sio praise team but objective observer, Magufuli na serikali yake nawaangalia with objective eye, wakifanya mazuri, napongeza, wakifanya mabaya nakosoa.
P.
Brother mayala hilo suala la bodi ya mkopo ni janga hususani watumishi wa umma kinachonishangaza watumishi wapo kimya they don't speak na ukifutilia asilimia 50 ya watumiaji wa hii mitandao ya jamii wengi wao ni wanafuika wa hii mikopo but wapo kimya wanategemea mwanasiasa awatete mtu kama msukuma au lusinde hii kitu hawajui kabisa so wataongelea nini

Kiukweli bodi ya mkopo inaumiza graduated wengi waliopo serikalini mshahara yao mikubwa but take home yao 😀😀😀😀 kituko mwisho wa siku wanaishi kama mashetani madeni kila kona alafu hayalipiki maana akipatacho hakikizi mahitaji at the end tamaa za rushwa zinaingia
 
Mimi ni mmoja wa wanufaika waliogoma kulipa kwa sababu ya kukiukwa kwa mkataba tuliosaini, nimekuwa nikifanya kila namna inayowezesha kuniepusha na hilo.... sasa naanza kupata tumaini kwa kusikia wengi wanapaza sauti.
Nilishajiandaa kisheria endapo ingetokea namna yoyote kuniwajibisha, tungekutana kwa pilato na hizo 6% zingepata tafsiri kisheria na uhalali wake kula kwa nyuma.... yaani ni kinyume na maumbile kupitisha sheria uchwara leo kisha ikaathiri makubaliano ya miaka 10 nyuma.
 
Sijui tumelogwa na nani!! Mida mingine ushabiki wenu Wa kisiasa muwe munauweka pembeni, wanufaika Wa hii mikopo, wapo Wa ccm, ukawa na wasiokuwa na mlengo wowote. Kumbuka asilimia kubwa ya wanufaika wazazi wao ni masikini. Sasa unapoleta siasa kwenye maswala kama haya tunashindwa kukuelewa mkuu.
sasa unashindwa kunielewa nini ndugu yangu wakati hili suala limeathiriwa na siasa, Kumbuka sheria ya kukandamiza wanufaika wa bodi ya mikopo kutoka asilimia 8 hadi 15 imeletwa na Jiwe na kupitishwa na Wabunge wengi ambao ni CCM, sasa hujaelewa nini hapo kuwa hilo limesababishwa na wanaccm bila kujali hata wanachama wao wanaathirika?
 
Hii nchi ishajifia.
Hao ccm hawawezi kukuelewa kwa sababu wao watoto wao wanasoma nje
 
sasa unashindwa kunielewa nini ndugu yangu wakati hili suala limeathiriwa na siasa, Kumbuka sheria ya kukandamiza wanufaika wa bodi ya mikopo kutoka asilimia 8 hadi 15 imeletwa na Jiwe na kupitishwa na Wabunge wengi ambao ni CCM, sasa hujaelewa nini hapo kuwa hilo limesababishwa na wanaccm bila kujali hata wanachama wao wanaathirika?
Unaonyesha upande mwingine wa sasa hata kama haupo ccm, tumeona hata zile halmashauri zinazoongoza na upinzani zimeshindwa Kudeliver, na kwavile tushaathiliwa na siasa, basi wanasiasa wanatuendesha wanavyotaka. Na ndiyo maana hata wanaharakati huru baadae wanageuka kuwa wanasiasa, wangebaki huru nadhani wangesaidia kusemea manyonge.
 
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imesema itawasilisha hoja mahsusi bungeni wakati wa mkutano ujao wa Bunge kupinga ongezeko la asilimia sita kila mwaka katika deni la wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Mkutano ujao wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza Septemba 3, mwaka huu ukitanguliwa na vikao vya kamati za kudumu za chombo hicho cha kutunga sheria.

Vilevile, kambi hiyo imesema katika hoja yake hiyo, pia itapinga makato ya asilimia moja yanayofanywa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) dhidi ya wanufaika wa mikopo hiyo kwa ajili ya ada ya uendeshaji kwa kuwa serikali kila mwaka imekuwa ikitenga fungu maalum kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za bodi hiyo.

Kifungu 7.2.1.1 cha Mwongozo wa HESLB wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa Wanafunzi kinabainisha kuwa mnufaika wa mkopo wa bodi hiyo atalipa tozo ya kulinda thamani ya fedha ambayo itakatwa asilimia sita kwa mwaka tangu tarehe mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.

Pia, katika kifungu 7.2.1.2 cha mwongozo wake huo, HESLB inaeleza kuwa itakata asilimia moja ya ada ya uendeshaji kwa mwanafunzi mnufaika.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Susan Lyimo, alisema kambi yao imeamua kuwasilisha hoja bungeni kupinga makato hayo.

Alisema kuwa kabla hoja hiyo haijatua kwa Spika, ataiwasilisha kwanza kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ili kamati hiyo ambayo yeye ni mjumbe, iitake serikali kupeleka bungeni muswada wa kurekebisha Sheria Na. 9 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Mwaka 2004 ili vifungu vyenye makato hayo vifutwe.

"Serikali itambue kwamba HESLB na haifanyi biashara, bali inatoa huduma ya kuhakikisha watoto wanaotoka familia maskini wanapata elimu ya juu, lakini kwa hali ya sasa ya kuwaongeza deni wanufaika wa mikopo, hakuna haja ya kuwa bodi hiyo," Lyimo alisema na kueleza zaidi:

"Kama wanataka kufanya biashara, basi jukumu hili lisifanywe na HESLB, liachwe kwa benki. Kumtoza mnufaika wa mkopo wa elimu penalti ya asilimia 10 ya mkopo kisha tozo ya asilimia sita ya mkopo kila mwaka na asilimia moja kwa ajili ya uendeshaji si haki.

"Inakuwa ngumu kwa wanufaika kumaliza kulipa deni kwa sababu linaongezeka kila mwaka hata kama wanalilipa, vinginevyo ndugu waungane na mnufaika kulipa deni lote kwa siku moja.

"Kitafika kipindi vijana wetu hawa itakuwa shida hata kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa sababu watahofu kuoa au kuolewa na mtu mwenye deni la HESLB ambalo hata ukianza kulilipa haliishi.

"Makato yenyewe ya marejesho ni asilimia 15 ya mshahara wa kila mwezi, huyo anayekatwa ana makato mengine ya bima ya afya, kodi ya serikali, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii... yaani karibu asilimia 50 ya mshahara wake unaishia kwenye makato ya taasisi za serikali, huyu mtoto wa maskini ataishije?"

Mbunge huyo wa Viti Maalum (Chadema) kwa kutambua uzito wa suala hilo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeona njia nzuri ya kutatua changamoto zilizojitokeza ni kuwasilisha hoja maalum bungeni kuitaka serikali kufanya marekebisho tena katika sheria iliyoanzisha HESLB.

"Hizi penalti za asilimia 10 na tozo ya asilimia moja nazo ni tatizo. Hakuna nchi nyingine inayofanya hivi. HESLB inatengewa fedha na serikali kwa ajili ya uendeshaji na watumishi wake wanalipwa mshahara na serikali.

"Pia tunaona hakuna haja kupiga penalti mnufaika kwa sababu hali halisi ya ajira nchini inajulikana. Kikubwa, bodi iwe na mfumo mzuri wa kuwatambua wanufaika," alishauri.

KAULI YA WIZARA

Akizungumza na Nipashe jana kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Willian Ole Nasha, alikiri kupokea malalamiko ya wanufaika kuhusu kuwapo kwa uonevu katika urejeshaji wa mikopo hiyo na kwamba wizara yake inaendelea kuyafanyia kazi.

Hata hivyo, Ole Nasha alisema baadhi ya changamoto zilizoibuka kuhusu urejeshaji wa mikopo hiyo, utatuzi wake unahitaji kurejea bungeni kufanya marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Mwaka 2004.

"Tumesikia malalamiko na siyo kwamba hatujayapata, tumeyapata na tunayatolea ufafanuzi na kusambaza taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari," alisema.

Ole Nasha alisema serikali ni sikivu na kwamba kwa sasa inafanya mapitio ya mfumo mzima wa mikopo hiyo ili kuangalia njia bora ya kutatua changamoto zote zilizopo.

“Tunahitaji kuendelea kutoa elimu ingawa inafahamika kwa sababu mkataba wa mikopo umeeleza kila kitu, tunaendelea kutoa elimu ili watu wafahamu zaidi na kila mwaka tunafanyia marekebisho mwongozo wa mikopo.

"Kuna mambo ya kisheria ambayo hatuwezi kuyafanyia marekebisho mpaka sheria ikabadilishwe bungeni, lakini yale ambayo yapo chini ya kanuni zetu tunafanyia marekebisho kila wakati tunapoona kuna haja kufanya hivyo," alisema.

Naibu waziri huyo alisema tozo ya asilimia sita imewekwa kwa lengo la kulinda thamani ya fedha ili kusaidia wanafunzi wengine wanaotaka kusoma kwa kupewa mkopo na Serikali.

“Tozo ya kutunza thamani inafanya ile thamani ya mkopo wako isipotee, yaani usiwe umekukopesha Sh. milioni moja na wewe uje urudishe milioni moja baada ya miaka saba, haitakuja kutusaidia, lengo la serikali siyo kukusanya fedha, bali kutunza thamani ya fedha," alisema.

Ole Nasha alibainisha kuwa uzoefu wa wizara yake unaonesha kuwa ukiacha miezi 24 iliyotolewa na HESLB kwa wanufaika kuanza kuhesabiwa muda wa kulipa deni, mdaiwa anaweza kumaliza deni lake ndani ya miaka 10 kama hatapigwa penalti.

“Utafiti unaonyesha kuwa inachukua miaka minne hadi 10 mnufaika kumaliza kulipa deni lake endapo ataanza kulipa kwa wakati," Ole Nasha alisema.

Hata hivyo, utafiti huo unakinzana na takwimu za urejeshaji mkopo za HESLB ambazo zinaonesha kuwa kati ya wanufaika 479,779 waliopatiwa mikopo hiyo tangu serikali ilipoanza kuitoa mwaka 1994, ni wanufaika 11,214 (asilimia 2.3) waliofanikiwa kumaliza kulipa madeni yao.

Pia, wanufaika wa mikopo hiyo waliozungumza na Nipashe wiki iliyopita, walidai wanufaika wengi wa mikopo hiyo walioanza kuilipa, wameshindwa kumaliza urejeshaji kutokana na deni kuongezeka kwa asilimia sita kila mwaka.

“Wito wetu ni kwamba ukichukua ule mkopo , tukijenga ustaarabu wa kulipa, inawezekana wanafunzi wote wanaoenda chuo kikuu, wanaohitaji mikopo wapate kwa sababu ni hela ambayo ipo kwenye mzunguko.

“Haimaanishi kwamba sisi kama wizara hatufanyii kazi changamoto zinazojitokeza, tukipata changamoto tunatoa elimu kuhusu hali ilivyo sasa na tukiona kuna haja ya kurekebisha, pale tunapoona tunaweza tunafanya,a Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kufanyiwa marekebisho ilikuwa Novemba 2016, serikali ilipowasilisha bungeni muswada ambao pamoja na mambo mengine, ulipendekeza mnufaika wa mkopo arejeshe mkopo kwa makato si chini ya asilimia 15 ya mshahara wake wa kila mwezi badala ya asilimia nane iliyokuwa awali.

Kumbe hii 15% inayontesa ilipitishwa na Bunge letu tukufu?!!!!!!
Nilijuwa Mr stone aliamua Tu!!!!
 
Haya mambo yanaanzaga kama utani mwisho wa Siku unasikia makato yameanza.. Naikumbuka asilimia 15%

Hii ilikuwa sababu tosha ya wanazuoni kupinga katika kila forum mbalimbali kwa kuandika hashtag ya uonevu huo sambamba na kuwasilisha malalamiko kwa wakikilishi wetu bungeni
 
Unaonyesha upande mwingine wa sasa hata kama haupo ccm, tumeona hata zile halmashauri zinazoongoza na upinzani zimeshindwa Kudeliver, na kwavile tushaathiliwa na siasa, basi wanasiasa wanatuendesha wanavyotaka. Na ndiyo maana hata wanaharakati huru baadae wanageuka kuwa wanasiasa, wangebaki huru nadhani wangesaidia kusemea manyonge.
Hapo na wewe umeonyesha upande wake halisi.
 
Back
Top Bottom