Elimu kuhusu "Kuua bila ya kukusudia" S.195(1) penal code

mwandishi A. hajui B. hajui kueleza maana nimesoma sijaona jambo geni au la maana ambalo ameandika. amesikia sikia sehemu akanukuu vifungu ndo kaja kuandika badala ya kuelezea kwa kina. hawa wasomi wenu wa siku hizi ni hopeless kabisa. miaka yetu haya mambo ya kipuuzi hayakuwepo .
Asante GuDume ...tutajitahidi kuwa wasomi wazuri zaidi mpaka tufikie level zenu ...
 
DEFINITION(MAANA)
Kuua bila kukusudia "BLACK LAW DICTIONARY 8TH EDITION 2004,P.3056
Limetoa maana kua "ni kitendo cha kuua binaadam bila ya nia ya kufanya hivyo" .....ni kwamba , bila ya kua na nia ovu mtu anaweza kusababisha kifo kwa mtu mwengine na akajikuta anawajibika katika mlolongo wa kisheria....mfano katika kesi ya "REPUBLIC V/S ELIZABETH MICHAEL" (UN REPORTED)
ambapo accused ameshukiwa kumuua "B" bila ya kukusudia na kukubali kosa hilo mbele ya mahkama.

VIINI VYA KOSA
A.kitendo kinyume ya sheria au kuacha kutenda.
Mfano "A" amewajibika kumsaidia "B" lkn akaacha kw makusudi au uzembe kumsaidia ...ikatokea "B" amefariki ..."A" atakua na kesi ya kujibu juu ya kwa nn ameacha jambo baya limtokee mwenzake ....au "B" sio kwa makusudi imetokea kamuua "Q" bila ya kukusudia "B" atawajibika .

B.kusababisha kifo kwa mtu mwengine.

AINA ZA KUUA BILA KUKUSUDIA.
1.kuua bila kukusudia.
2.kuua kwa kukusudia.
mfano :"S" amemuua "G" kwa hasira. Refer case of "BENJAMIN MWASI V. REPUBLIC(1992) TLR 86 (CA).
ambapo mshtakiwa alikubali kosa la kumuua mchumba wake ..katika rufaa alitaja defence ya hasira kutokana na maneno alioongea mpenziwe ambayo ni ya kashfa ...mahakama ya ya rufani ikakubaliana na dai lake na kosa lake likawa ni kuua bila ya kukusudia.

Mfano(2) : self defence(kujihami)
Ref. case of "MOSES MUNGASIANI LAIZER ALIAS CHICHI V. REPUBLIC (1994) TLR 222 (CA) .
Ambapo mshtakiwa alikata rufaa kutoka hukumu ya kuua kwa kukusudia kutokana na kusababisha kifo cha alieuliwa "deceased" ikiwa sababu ni kupigana ...mahakama ya rufani ikaamua kua mshtakiwa aliua bila ya kukusudia....


By Yunus (DIL 2nd Year )
Safii mwanzo mzuri, ukifika LL.B utakuwa vyema zaidi kwenye Legal method(case analysis) hata mbuyu ulianza kama mchicha, as long as una practise law everywhere utakuwa nondo anywhere.
 
Kesi kusikilizwa upande mmoja ( ex-parte) hutokana na:
A.Upande wa pili kutohudhuria shaurini.
B.Kupuuza wito n.a. kutotoa/wasilisha ushahidi au utetezi.Inaweza kuwa hata kati kati ya shauri.

Endapo hukumu itatoka ya upande mmoja, upande uliokosa nafasi ya kusikilizwa unaweza kupeleka maombi ya kusitishwa hukumu hiyo (set aside) n.a. kupewa nafasi ya kusikilizwa ( baada ya kutoa sababu kwa nini haukusikilizwa/haukuhudhuria shaurini-sababu za msingi. Maombi yapelekwe mahakama hiyo hiyo n.a. hakimu huyo aliyesikiliza mwanzo shauri Hilo.
Je ikiwa huyu judge,aliyesikiliza kesi amefariki,ndio kusema haiwezekani tena kufungua hilo shauri?Kwa kumaanisha kesi imesikizwa na judge sio hakimu.
 
Je ikiwa huyu judge,aliyesikiliza kesi amefariki,ndio kusema haiwezekani tena kufungua hilo shauri?Kwa kumaanisha kesi imesikizwa na judge sio hakimu.
Mwingine anasikiliza,ila kama aliyesikiliza yupo ni vyema aisikilize
 
Mimi sheria ilipita kushoto napenda kujua kazi za watu wafuatao
1. Hakimu
2. Judge
3. Wakiri

Pia nijue hizi mahakama kiundani zaidi
1. Mahakama ya mwanzo na inauwezo gani.
2. Mahakama ya wilaya na uwezo wake
3.mahakama ya rufaa na uwezo wake
4. Mahakama ya aridhi na si mahakama zingine
5. Mahakama ya watoto

Mwisho
Nn sababu ya kesi kusikilizwa muda mrefu?

Nawezaje kufungua jarada LA kesi

Nawezaje kuondoa kesi mahakamani/ kuifuta

Simu inapogika nikiwa mahakamani sheria inasemaje. Maana huwa nasikia ni makosa. Maswali ni mengi tuanze na haya.
 
Back
Top Bottom