Elimu kufaidisha wanasiasa ni sawa?

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
Leo asubuhi wakati najiandaa kuelekea kunakoshughuli nikabahatika kuona taarifa ya habari ITV ambapo Mzee Makamba alikuwa anazindua kitabu chake ambacho kimechapwa na Nyambari Nyangwine. Uzinduzi wa kitabu haukuwa tatizo kwangu bali hotuba fupi aliyoitoa mzee makamba kwamba aliandika barua kwa Rais, Waziri Mkuu na waziri wa Elimu kuwaomba wanunue kitabu chake ili ajikomboe na ufukara na sasa kimenunuliwa na serikali na kinatumika kufundishia darasa la tano nala sita. Maswali yakaja, je vitabu vya kufundishia nchi hii vinapitishwa na rais au waziri mkuu au waziri wa elimu? Na kama utaratibu utakuwa ni mtu kuandika kitabu kwa vile ana-influence ya kuishawishi serikali kununa kitabu chake je ikiwa hakikidhi mahitaji na kikapitishwa kwa sababu aliyeomba ni mwenzao kiitikadi itakuwaje? Je mzee makamba alikuwa anaandika kitabu ili aiuzie serikali au ulikuwa ni utashi wake tu tena kwa gharama zake? Ni kweli mzee makamba ni maskini? Suala kama hili wanalichukuliaje waandishi mahiri wa vitabu nchini ikiwa wao hawana access wala kufahamiana na viongozi waliopo juu? Utaratibu wa kupitisha kitabu kwa ajiri ya shule zetu ukoje?

TAFAKARI
 
Back
Top Bottom