Elimu juu maambukizi ya Ukimwi itolewe kuanzia ngazi ya chekechea

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Kundi hili limekuwa likisahaulika sana kupewa elimu juu ya maambukizi yanavyoweza kuambukiza kwa njia ya kushirikiana vitu vyenye ncha kali huko mashuleni kama vile viwembe, pini nk.

Watoto hawa wadogo wapo wengine wana maambukizi waliyoyapata kutoka kwa wazazi wao na hawajui lolote kutokana na umri waliokuwa nao,hivyo basi katika michezo yao huko mashuleni na mitaani wamekuwa wakishirikiana vitu vingi hata vile ambavyo ni hatarishi.

Juzi mtoto wa jirani yangu hapa mwenye umri wa miaka mitano ambae ni muathirika kutoka kwa wazazi wake na pia Baba yake alishatangulia mbele za haki kutokana na tatizo hilo hilo, nimemkuta akiwa anakata kucha huku akiwa tayari amejikata damu zinamtoka huku mtoto mwingine ambae walikuwa wanacheza wote pale akiwa anatumia wembe ule ule kukatia kucha zake.

Hapo tunaona kabisa kuwa wote hao hawajawahi kukatazwa au kupewa elimu kuhusu kushirikiana vitu kama hivo. Kwamba mmoja akitumia basi mwingine hairuhusiwi kukitumia tena kifaa hicho.

Hayo ni machache katika mengi ambayo wanafunzi wetu au watoto wetu wamekuwa wakikutana nayo huko mashuleni na mitaani.

Serikali kupitia Taasisi husika zinapaswa kutoa elimu ya ukimwi kuanzia ngazi ya chekechea hii itafanya watoto wetu kuwa na uelewa tangu wakiwa wadogo
 
Wapo kwenye risk sana. Michezo yao ni hatari tupu. Wanaokota tu vifaa na kuchangia pamoja.
Ni kumkataza mtoto kuanzia nyumbani, wengine unakuta wanashika shika vidonda vya wenzao au sehemu zenye majerahae
 
Back
Top Bottom