Elimu itolewe Tamisemi haraka, wizara imelemewa majukumu

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
871
1,000
Nimekuwa naifuatilia Tamisemi na jinsi inavyofanya kazi, ni dhahili wizara hii imelemewa na majukumu.

Haiwezekani Tamisemi ichuje ajira za walimu, afya, kilimo n. k wakati Kuna tume ya ajira. Hiyohiyo wizara ihusike na uhamisho wa watumishi, iratibu mitihani na ulipaji posho, ishughulikie madeni ya watumishi, ishughulikie ufaulu wa wanafunzi.

Matokeo kidato cha nne 2020, yalitangazwa mapema kabisa na NECTA, cha kushangaza mpaka leo Tamisemi haijawahi kuwapangia shule wanafunzi, wengine wameshasahau kama kuna kusoma, wengine hasa watoto wa kike wamejazwa mimba.

Hiyo hiyo Tamisemi inaratibu ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, afya n. k

Hiyo hiyoTamisemi inahusika na mchakato ya upandishaj vyeo kada mbalimbali ikiwemo watumishi wa kada za elimu.

Hiyo hiyo Tamisemi inahusika na kuratibu mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA.

Tamisemi imelemewa na kazi, itaporomosha ubora wa elimu, elimu irudishwe wizara ya elimu.
 

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,114
2,000
Ni kweli lakini mengine uliyoyataja yapo chini ya wizara ya utumishi na utawala Bora.
 

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
1,356
2,000
Kwani Wizara ya elimu inasimamia nini?

Kwani selection za kidato cha tano na chuo huwa zinatoka muda gani?

Au ni kujisahaulisha na kupenda kulaumu kila kitu, kwa sababu vya kulaumu vimekwisha.
Wizara ya elimu imebaki kwenye vyuo na kutunga Sera za elimu na mitaala kwa ngazi zote za elimu.
Ila huku sekondari kwenye uendeshaji ni Tamisemi kila kitu.
Selection kidato cha tano mwezi wa 6
 

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,759
2,000
Serikali yetu sio wabunifu walipaswa kuivunja vunja tamisemi na kutoka hata taasisi tatu au nne na teyari serikali itakuwa imetengeneza Ajira na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii.
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,977
2,000
Serikali yetu sio wabunifu walipaswa kuivunja vunja tamisemi na kutoka hata taasisi tatu au nne na teyari serikali itakuwa imetengeneza Ajira na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii..
1. Taasisi inayoratibu Elimu na miundombinu yake
2. Taasisi inayoratibu Afya na miundombinu yake
3. Taasisi inayoratibu ajira na vyeo au madaraja
4. Taasisi ya supervisors waziri,manaibu na katibu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom