ukweli ni kwamba Elimu imeshuka sana Tanzania tena sio Vyuo vikuu tu zaidi mno hata kwa mashule ya secondary na A'LEVEL's .
Nakumbuka wakati tunamaliza sisi mtu ilikuwa kuingia MHIMBILI lazima uwe na div 1 ,ukikosa basi walau uwe na div 2 nzuri esp kwa males.
Lakini leo nenda pale mhimbili ukawaulize watakwambia kuwa hadi div 3 ya mwisho wanachukuliwa sababu watu wenye div One kwa masomo hayo wamezidi kuwa wachache sana. Na juzi juzi tu nilikuwa naongea na jamaa yangu aliyepale akawa ananipasha na kusema mmmhh yaani hapa siku hizi Criteria sio za mhimu sana.
Sasa unategemea nini? kama huwezi kuwa strict on academic credibility? je hao unaandaa madaktari wa kiasi gani? si maanishi kuwa wakiwa na div 3 au 4 hawawezi kuwa madaktari, la hasha ila nataka kuweka hali halisi ilivyobadilika , na hili liko karibu vyuo vyote ambavyo vilikuwa na sifa kubwa kwa sasa vinazidi kuporomoka.