Elimu imenishinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu imenishinda

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by tizo1, Apr 28, 2011.

 1. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Naomba ushauri jaman!nimemaliza kidato cha sita HKL na nimepata DIV 4 YA 19 .je nifanye nini sasa?naomba mnisaidie.
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Email me at mtoboasiri@yahoo.com
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,121
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Pole mzaz..jaribu kusoma vyuo vya ufundi kama veta.
   
 4. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  Usiwe na hofu huo siyo mwisho wa maisha..tulia mwombe Mungu, He always has a plan 4u, Jeremiah 29:11...
  Kuna stori nyingi sana za watu waliofeli form 6 na sasa wamefanikiwa academically and in life...wala usiwe na hofu mdogo wangu!!!
  * one of the options ni kutumia vyeti vyako vya form four uanze certificate uendelee na life..
  * au, kama unaona, unajua, na una uhakika kuwa imetokea kwa bahati mbaya, labda hukuwa tayari kimaandalizi, as in u r very sure...then i suggest u resit the examinations..lakini hii ni kama una uhakika wa sababu iliyokufanya upate matokeo hayo!!!
  Ulikuwa shule gani mdogo wangu!??
   
 5. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  nilikuwa kwiro high school
   
 6. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole Tizo1. Ukweli ni kuwa bado una nafsi kubwa sana ya mafanikio katika maisha. A-level huwa ina suprises zake na mazingira ya usomaji mara nyingi ni magumu. Miongoni mwa mambo ambayo huwa yanatatiza ni kuulizwa maswali na watu wa mtaani kuhusu matokeo yako na pia inauma pale unapoona wenzako wanaenda vyuo vya elimu ya juu na kukuacha. Hili ni jambo la kawaida.

  USHAURI:

  1. Usijaribu kuzuia maumivu ya kufeli. Kwa kipindi fulani ni lazima na ni halali pia kupata maumivu. Usifanye kazi kubwa sana kujaribu kuzuia maumivu, yataisha yenyewe. Maumivu huisha kama utakuwa na altenatives. Ukishapata jibu juu ya hatua za kuchukua utashangaa ghafla maumivu yanaanza kuisha.
  2. Soma kwa hatua. Kwa kutumia cheti chako cha Form 4 unaweza kuapply vyuo vinavyotoa certificates then diploma then degree n.k. Ni sawa tulikuwa tunataka kwenda chuo kikuu, lakini matokeo hayaturuhusu. Katika mazingira kama haya tufe? Hapana maisha ni lazima yaendelee, hata kama watu watakucheka, vumilia. Katika kuchagua certificates angalia courses za mambo unayoyaweza au kuyapenda, pia ni vizuri kuangalia soko la ajira la courses hizo Tz (kama unawaza kuajiriwa).
  3. Kama unadhani umefeli kwa bahati mbaya unaweza ku-resit, japo ku-resit na kufaulu ni kitu kigumu sana. Angalia uhalisia wa uwezo wako.
  Jipe moyo, maumivu ni lazima yawepo kwa muda fulani na ni lazima yaishe. Ila ni rahisi maumivu kuisha kama utajua nini hatua ya kuchukua baada ya matokeo haya. Tuko pamoja na Mungu akubariki.

  NB. Kama utakuwa unahitaji ushauri wa ziada au ushauri private waweza kunitumia private message.
   
 7. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hakuna haja ya pole na wala usikubali yeyote akupe POLE. Panga stratergy yako upya, naamini ulikuwa una ndote, malengo, you wanted to be(come) somebody. Hebu fanya assessment kama umeharibu sana au kuna uwezekano wa ku-make up.
  There's still a life for you.
  Nilikuwepo ile Kwiro ya Makunja, sisi ndo tulianzisha combi za arts mahali hapo. Natumaini Mama Ngapo bado atakuwepo!
   
 8. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  nashukuru kwa ushauri mzuri,nitaufanyia kazi.pia nta ku pm ili unijuze zaid.nimekata tamaa kabisa.ki ukwel nlikuwa fit sana'
   
 9. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  asante kwa ushauri.
   
 10. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  A level ndivyo ilivyo, cha msingi uangalie nini unafanya kuanzia hapa, hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa mdogo wangu. Mungu akutie nguvu
   
 11. c

  corleone Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we mbona hujafeli! kufeli ni kupata division 0.. kuna vyuo vingi unaweza kuapply usome remedial course then unaunga degree mwaka huu huu. fuatilia st. augustine university mdogo wangu, usikate tamaa.
   
 12. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Asante sana kwa ushaur mzuri.UMENITIA MOYO na kunipa mwanga!nilikuwa na uwezo mzuri sana!hakuna wasi ntajitahd kufanya hivyo!
   
 13. Mani H

  Mani H Senior Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mdogo kwanza naomba kukuambia kuwa ujaanguka bali umeteleza na "kuteleza si kuanguka" si nafasi kibao za kuendelea na elimu ya juu tafuta pre degree me najua hii iko zanzibar sijui ni chuo gani hasa,ambayo unasoma one year ukipass unaendelea na masomo yko, vile vile unaweza ukaanza ngazi ya cheti ,diploma na kufikia advance diploma. nakushauri kw wakati huu usiwe na haraka katika maamuzi yako , kuwa makini na tumia mda wako kwa kuuliza watu na kuomba ushauri, i hope utafanikiwa
   
 14. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  mimi ushauri wangu usirudie mtihani... utapoteza muda, jipange tafuta mradi ... kama ni biashara usifanye ya kuuza na kununuwa, fikiria biashara ambayo ita provide service "even though inategemea na sehemu uliyopo" ..

  kufeli kitu cha kawaida sana kwa elimu yetu ya bongo.

  Jipange
   
 15. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  asante sana TIZO1...asanteni wadau wote mliotoa ushauri wa kujenga.....hapa sasa napata faraja na maana ya kukaa JF....it is a building block, nikiwa mdau mkubwa wa elimu nashawaishika kusema dogo TIZO1 kujgundua tatizo au kushirikisha watu tatizo lako tayari umeshalitatua 50%... yaani umeshafika nusu ya jibu la tatizo lako
  Shule zipo nyingi kufikia malengo yako ..japo ile njia uliyokuwa unaiona haikidhi haja!
  rejea ibada kwa kasi mpya
   
 16. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,957
  Likes Received: 20,288
  Trophy Points: 280
  Huna haja ya kujilaumu kivile, ni kweli unaokosa kufikia malengo yako unaumia, lazima kila kitu kiende mbele, Naunga mkono wote wanaosema kuwa tumia cheti chako cha fom4 (kama unahitaji kuendelkea na elimu ya juu) unaweza kuanza na dip na kama inashindikana kabisa anzia cheti. Vyuo vilivyo chini ya Nacte vinasaidia sana katika hili, vipo vingi mfano ni IFM, CBE, Mwalimu Nyerere na TIA, USTAWI,
  Ningekushauri tembelea USTAWI MNMA utapata zaaidi

  Halafu (SIRI YAKO) unaweza kucope na stress ulizonazo kwa kuangalia mifano ya watu walioanzia na elimu za UPE lakini leo ni madaktari, mfano mmoja ni Dr Kadeghe Maiko:A S 39:
   
 17. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Asante sana nazid kufarijika na wana JF nilipo wengi si wasomi na wanafikiri kufel nh uzembe!kwel hiki ni jukwaa la elimu tayari naanza kupata mwanga na kuona si mimi pekee niliyefeli maisha
   
 18. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  asante sana angalau nimepata mwanga fulani hivi!JF ni msaada tosha jamani
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kufeli shule sio kufeli maisha mdogo wangu.
  Unaposhindwa upande mmoja geukia upande wa pili. Tafuta shule za ufundi ujiendeleze inawezekana hiyo ndio channel ya kutokea mungu aliyokupangia.
   
 20. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu kwa maneno yako hapo juu. Kaka TIZO1 usikate tamaa kama wadau hapo juu walivyosema kufeli pepa sio kufeli maisha. Nakuomba jipange na kusonga mbele hata mm nakushauri usirudie pepa kwan unaweza songambele na hizo point zako cheki vyuo hapo tz, nakupiga masomo ya jioni unaunga degree kabisa.

  Sasa naona bongo vijana tunabadilika kwan nilikuwa nachukia kumwambia mtu heti umefeli na walio faulu wakawa wanajiona wapo fiti kiakili lakini sio hivyo katika ulimwengu huu.

  pamoja tutajenga taifa, hila vijana tubadilishe mawazo yetu. Wana JF pamoja tutapeleka taifa la tz kwenye ukurasa mpya.
   
Loading...