Elimu Haipaswi kuwa Chanzo cha Matabaka


mzamifu

mzamifu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2010
Messages
4,254
Points
2,000
mzamifu

mzamifu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2010
4,254 2,000
Elimu ya tanzania ina ishara ya kujenga matabaka. Siku hizi shule za serikali zimebatizwa jina la Kayumba. Kuna tofauti kubwa sana ya kimtazamo na kisaikolojia kati ya wanafuzi wanaosoma English Medium na wale wa shule za Kayumba. shule nyingine ada mpaka milioni tano kwa mwaka. elimu gani inatolewa huko kuzidi hata ada ya Chuo kikuu.
pendekezo langu ni kuwa zichukuliwe hatua za makusudi kuunganisha shule zetu kwa programu mbalimbli ka ma mashindano ya michezo. taaluma na life skills. watoto wa shule za kayumba wako inferior mbele ya watoto wa English Medium kwa misngi ya kwamba wanapata huduma kwa shida sana mfano usafiri, chakula na kufundishwa na walimu wanye manung'uniko. ni vyema pia walimu wakalipwa vizuri.
katka Elimu ya juu kumeanza hii tabia ya kuita vyuo vingine vyuo vya Kata huu ni ubaguzi na dharau. Tume Ya vyuo vikuu ichunguze kama kweli kuna vyuo inaoparate chini ya viwango vipewe maelekezo.
Eimu haipaswi kujenga taswira ya matabaka na ubaguzi.
 
Ruge Opinion

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2006
Messages
1,774
Points
1,500
Age
65
Ruge Opinion

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2006
1,774 1,500
Sekta ya elimu ina-reflect jamii ya sasa ilivyo. Ni jamii yenye matabaka. TCU au serikali haiwezi kufuta matabaka kwa amri au miongozo. Tuko kwenye soko huria na mlaji anachagua anachokitaka na anachoweza kumudu gharama zake. Kuna wanaoendesha magari ya Hammer wakati wengine hawawezi kununua hata baisikeli. Inaumiza lakini ndiyo hali halisi.
 
mzamifu

mzamifu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2010
Messages
4,254
Points
2,000
mzamifu

mzamifu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2010
4,254 2,000
Asante kwa kweli umesema vizuri. hii ina maana tumeacha ile misingi ya usawa. baada ya kutoa hii thread nimemsikia Pengo naye akikemea hali hii. amefikia hata kukemea tabia ya makanisa kutoza ada kubwa.
 
mtzedi

mtzedi

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2011
Messages
2,715
Points
2,000
mtzedi

mtzedi

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2011
2,715 2,000
Matabaka lazima yawepo kwani mambo mengi Tanzania yanafanyika kwa maneno na si vitendo.Utasikia ooh shule haina walimu,vifaa kwa maneno tuu.Usawa katika elimu Tanzania ni sawa na kusubiri muujiza. Mtoto wa familia za hali ya chini anasoma shule za kayumba kwa bidii ili afaulu vizuri walau apate mkopo wa elimu ya juu,mwishowe anaambulia patupu.Wakati watoto wa wanaojiita vigogo,mafisadi chekechea tuu analipa kama milioni moja kwa mwaka akifika chuo anachakachua mkopo anapata asilimia mia moja.
 

Forum statistics

Threads 1,283,843
Members 493,850
Posts 30,802,759
Top