Elimu, Elimu, Elimu kwanza mengine yafuate

BEDECCA

Member
Oct 27, 2016
10
4
Ndg wapendwa, Uongozi wa BEDECCA umepanga mkutano wa kuelimisha jamii umuhimu wa Elimu, athari za utoro mashuleni kwa watoto, pia na athari za mimba katika umri mdogo.
Mkutano huo utafanyika katika mkoa wa Mbeya, halmashauri ya wilaya ya Busokelo, kata ya Kandete katika kijiji cha Mwela, Kitongoji cha Kisiba, maeneo ya Kisiba na Mbozi mnamo tarehe 10/12/2016, katika eneo la Kisiba na tarehe 17/12/2016, katika eneo la Mbozi siku ya Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne asubuhi.(08:00 hadi 10:00 asubuhi) sehemu zote hizo mbili ni muda mmoja. Wadau wa Elimu tunahitaji mchango wenu wa mawazo,
Ahsanteni.
 
Nawakumbusha: Msisahau kuweka vikolezo kama ngonjera,mashairi,nyimbo nk toka kwa watoto wetu. Mkiwaandaa mapema ni vizuri. Vikolezo hivyo huwa kivutio na hufikisha ujumbe kwa haraka.
 
Kweli kabisa
Nawakumbusha: Msisahau kuweka vikolezo kama ngonjera,mashairi,nyimbo nk toka kwa watoto wetu. Mkiwaandaa mapema ni vizuri. Vikolezo hivyo huwa kivutio na hufikisha ujumbe kwa haraka.
 
Back
Top Bottom