Huyu jamaa inaonekana ana fikra ndogo sana tena ndogo kupita kiasi na zilizo mgando... hivi nikuulize labda ukisikia anasema elimu bure wew unaelewa vip? Inavoonekana hujui nini maana ya sera na jinsi inavyofanya kazi na haya mambo wala huyaelewi kabsa kwakuwa kufikiria kwako ndo kumekomea hapo kwamba haiwezekani eti kwa mfano/sababu uliyotoa wew..hivi wew hata unaelewa ni jinsi gan vyombo na tawala mbalimbali za serikali zinavyoendeshwa... hao unaosema wataondoka DUCE kuja mlimani kusoma uhasibu umeshafikiria kwa kina huko DUCE walifikaje. Au unadhani kila anaeenda kusoma medicine, uengineer,ualimu, uhasibu, na kwengineko wanajiamulia tu kwamba wanaenda kusoma huko. Kama ni hivo basi naomba nkushauri hivi kama wewe uko form 6 au mwanao mfano combination HKL afu akimaliza shule baada ya matokeo uende ukaombe form ya enrollment pale COET mlimani ili ukasome hyo engineering unayoitaka, au pale ardh unvsty ukasome urban economics, au nenda mzumbe unvst ukasome ICT. Wewe kwa fikra zako Ukisikia anasema elimu bure mpaka chuo kikuu unaelewa nin? Labda tuanzie hapo. Najua utafikiria kwamba hiyo huwa inaitwaga ni sera. Ila hujui sera maana yake ni nin. Zimeweza nchi ngap hiyo kitu tena na mengine mengi ya bure na ukiangalia nyingine ni nchi ambazo hata sisi tunazipita kwa resources tulizonazo. Swala la elimu bure mpaka chuo kikuu haliihitaji mjadala na tena limecheleweshwa lilitakiwa lianze kitambo sana sema hawa minyooo ccm walokuandikia huu uzi uje kupaste huku ndo wamefanya tusifike huko.
Swala hili linawezekana tena bila kupingwa provided that kuna means,plans na strategies za kulifikisha pale tunapotaka. Nahiyo ndo maana ya sera. Wala halihitaji kutumia nguvu za tembo kufikiri muda mwingi kama ulivofanya wew na kuja na conclusion ya kishamba sana. Swala ambalo hata mmachinga ambae hajaenda shule ila ni mwenye kupenda kujifunza mengi kutoka kwa watu kwa kusikia au kuona anaelewa kwamba hilo linawezekana sembuse wewe.
Kama wew rika lako ni kijana bas pole sana kwakuwa ulishalemazwa kifikra na ccm kama wale wazee wa tabora kwa kununuliwa katika kila general election.
Na unasafari ndefu sana ya kupoteza muda mwingi mno katika maisha yako ya kifikra na mpaka uje kujua what's going on in this country and what's wrong with this shit ccm ni pale upinzani utakaposhika hii nchi.
Hukuwa na haja ya kusema et kesho ukumbushwe kurudia uzi na atakaekukumbusha bas ni kilaza plus tena kuliko hata wew nadhan.
na inaonekana maisha yako ni mafupi saana kama sisimizi au nzi kwa fikra ulizonazo.
Kwasabu utakujafanya maamuzi hasi yatakayokucost kutokana na kiwango cha fikra ulichonacho.
kimsingi hukuwa na hoja yoyote kama alivosema bwana More Tiz nashukuru kwa kulitambua hilo.
Kitu kingine familia yako kama unayo au unaitarajia bas itajuta sana kupata kiongoz wa familia kama wew simply because of your brain limit capacity.
Nyie ndo malofa na wapumbavu alowasema mkapa japo wewe kwa fikra zako finyu sana isiyoweza kuchambua hata neno bure na ccm wenzio kwa fikra zenu mgando hamkumwelewa yule mzee mkapa alikuwa anamaanisha nini.
Mkahisi alikuwa anawatukana akina lowassa. kumbe lilikuwa ni tusi kwa watu kama wewe na ccm yenyewe. Kama ulikuwa hujui hilo ulijue.
Sina cha kukushauri na Sijui nkushaur nin kwasabu ushauri wangu utahitaji fikra hata ile ya kawaida ambayo wew huna kwasababu tu ulishaharibiwa na fikra za manjano/kijani.
siwez kukwambia kaa chini ufikirie upya hilo hutaliweza sababu unaijua wewe. Ila inasikitisha sana kuona mtu kama wewe mwenye fikra kama hizo na huwezi badilika kamwe kwakuwa laana ya wengi wanaoumia kwa maovu ya ccm na wale wawaungao mkono bado imewashika mpaka pale mtakapotembelea futi 6. Kwenda chini.
Kama ni umaskini utakufa nao, kama ujinga utabak nao milele ili viendelee kukutafuna.
Kiujumla hujielewi na hujitambui ndiko kunakopelekea kuwa na fikra fupi kias hicho.
Pole sana mkuu "vikao vya harusi"
Jina tu peke yake linaonesha kuwa wew si mzima kabsa, na yaweza kuwa ni grade one ya milembe!
Leo ngoja niwasaidie jamaa zangu wa CCM ambao wengi wao hawajui Hesabu. Tangu Mgombea Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa atangaze Elimu bure, kuna watu wamekuwa wakiona huo kama muujiza.
Kwa kifupi zipo njia nyingi sana zinazoweza kufanya Elimu kuwa bure kuanzia Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Leo ngoja niongelee 'alternative' moja.
Kwa mujibu wa TAMISEMI Tanzania ina jumla ya shule za msingi 16,343 zenye wanafunzi 8.3 mil. Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka kutoka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka huu.
Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 54 kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, wanafunzi wa shule za msingi wanakadiriwa kugharamia kiasi cha Sh.10,000/= hadi 15,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi Tanzania wanahitaji Bilioni 80 waweze kusoma BURE.
Shule za Sekondari za Serikali zinakadiriwa kuwa 2,446 zikiwa na jumla ya wanafunzi 1,004,071. Kati yao wanafunzi 185,652 ni wa Shule za Kulala (Boarding), na wanafunzi 818,419 ni wa shule za kutwa (Day).
Wanafunzi wa Shule za kutwa wanalipa ada TZS 20,000 kwa mwaka. So ukichukua 20,000 × 818,000 utapata Bilioni 16.3. Wanafunzi wa shule za Bweni wanalipa ada TZS 70,000/= kwa mwaka. So ukichukua 70,000 × 185,652 utapata Bilioni 11.2.
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu wa vyuo vya Serikal na vya binafsi wapo 200,986. Kati yao wanafunzi 162,987 wanasoma Course za 'Social Science, Law, Humanities, Education etc' ambao ada zao hazizidi Mil.2 kwa mwaka. So chukua 162,989 × 2000,000/= utapata Bilioni 325.
Wanafunzi 37,997 wanasoma course za "Science" kama Engineering, Udaktari etc na ada zao ni zaidi ya Mil.3 kwa mwaka. So hawa watahitaji Bil 113.5 kulipa ada ya mwaka mzima.
Fedha ya kujikimu pamoja na chakula (Meals & Accomodation) inayotolewa kwa sasa ni TZS 7,000 kwa siku kwa mwanafunzi mmoja. Hivyo basi mwanafunzi mmoja anapata Jumla ya Shilingi 1,680,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu ambao ni 200,986 wanahitaji Bil 337.
Fedha ya Utafiti (Research), Mafunzo kwa njia ya vitendo (Field) na vitabu (Stationeries) hutolewa jumla ya Shilingi 735,000/= kwa mwaka ambayo hugawanywa kulingana na asilimia ya mkopo ya mwanafunzi. Hivyo basi wanafunzi wote wanahitaji Bil 147 kwa mwaka.
Ukijumlisha gharama zote hapo juu utapata jumla ya Shilingi Bilioni 934 tu. Kwa lugha rahisi ni kuwa ili kila mwanafunzi nchini asome bure kuanzia Elimu ya msingi, sekondari na akifika Chuo Kikuu alipiwe gharama zote bure kwa asilimia 100%, serikali inahitaji kutoa Shilingi Bilioni 934 tu kila mwaka.
Swali, Je hizi Bilioni 934 zinapatikanaje?
Ukisoma hotuba ya Bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2014 utagundua kuwa Mlima Kilimanjaro peke yake unachangia karibu Bil.800 kwenye pato la Taifa (Gross National Income of $350 Milion).
Kwa lugha Rahisi ni kuwa tunahitaji Mlima Kilimanjaro mmoja tu ili watoto wetu wasome bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Yani tukiamua mapato yote ya Mlima Kilimanjaro tuyapeleke kwenye sekta ya Elimu bila kuchakachua, tutakua na uhakika wa kusoma bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu. Je hatuwezi??
Hapo hatujagusa Mbuga za wanyama, hatujagusa Bandari, Madini, Gesi, Mazao ya misitu, Uvuvi, Kilimo, Viwanda, etc. Tumegusa mlima Kilimanjaro peke yake. Kama CCM wanaona hawawezi wakae pembeni wanaoweza wafanye.!