Elimu bure bila kuboresha maslahi ya walimu

Elimu bure bila kuboresha maslahi ya walimu

Hasa miwalimu ya shule ya msingi, ni mioga sana, tatizo nadhan ni vyeti vyao

Walimu wa shule za msingi wengi Wao ni mazezeta na waog sana....

Hakuna sheria wala waraka unaompa Afisa elimu nguvu ya kukushurutisha we mwalim ufundishe kipind cha likizo...otherwise kuna posho wanakulipa

Walimu zinduka....tutaonewa mpaka lini
 
Bora nikalime karanga kulko kufanya kazi ya ualimu

Jitu kama hili linaongea utafikiri halina mtoto au Kizazi!! Sijui kusipokuwepo na walimu taifa litakuwaje!! Badala ya kujadili changamoto linajadili upuuuzi any way wewe ni mpuuzi!!!!
 
UBORESHAJI WA ELIMU UENDE SAMBAMBA NA UBORESHAJI WA MASLAHI YA WALIMU.

Serikali inatakiwa kujielekeza katika ujenzi wa nyumba za walimu na kuboresha pia maslahi yao, maana kwa sasa suala la madawati sio tatizo tena. Walimu wanamchango mkubwa katika kuboresha elimu ya nchi yetu, hivyo basi serikali inatakiwa ione thamani yao kwa kuboresha maslahi yao.Ninachokiona kwa sasa kwa serikali yetu ni kujikita zaidi upande mmoja tu wa wanafunzi na sio walimu.

Shule nyingi za sekondari na msingi hazina nyumba za walimu za kutosha, walimu wanaishi kwa kuhangaika sana, baada ya serikali kutangaza elimu bure idadi ya wanafunzi imeongezeka lakini idadi ya walimu imebaki kuwa ileile.

Suala la Upungufu wa walimu hususan wa masomo ya sayansi ni tatizo kubwa katika nchi yetu, serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka ili kuajiri mapema na sio kuanza kupiga danadana jambo hili. Binafsi nimefanya utafiti zipo shule nyingi za sekondari hakuna hata Mwalimu mmoja wa physics, chemistry, Biology na Basic Mathematics. Ukosefu wa walimu wa sayansi unaathiri sana wanafunzi kitaalamu. Walimu wapo mtaani wamehitimu vyuoni wengine mwaka jana na wengine mwaka huu lakini chakusikitisha ni kuona serikali suala hili hiichukulii kama ni kipaumbele badala yake suala la madawati ndio limekuwa ni kipaumbele. Hivi mwanafunzi anapokwenda darasani na kukaa tu kwenye madawati huku baadhi ya masomo hayafundishwi kabsa maana yake ni nini hapa? . Kuna athari kubwa za mwanafunzi kwenda darasani tu halafu akaishia kusoma masomo ya sanaa (arts) tu huku baadhi ya masomo ya sayansi hakuna walimu kabsa. Pesa zinazotolewa na serikali kwa kila shule hazitoshi kuajiri hata walimu wa parttime kwa ajiri wa kushughulikia pengo hilo la walimu. Serikali inatakiwa ilitafutie ufumbuzi wa haraka jambo hili.

Namuomba sana Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli kufikiria upya suala la elimu na kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya walimu. Kwani bila kumjali mwalimu elimu bora ni ndoto ya mchana. Tukiwa tunaelekea katika nchi ya viwanda serikali yetu inatakiwa kutenga angalau 30% ya Bajeti yote kila mwaka na kuwekeza katika sekta ya elimu.

Mwisho, naiomba serikali isikilize na itatue kero za watumishi wa umma. Watumishi wa umma walio wengi mpaka sasa wameanza kukata tamaa maana wanaona serikali yao kama haiwajali vile.

Wako,
Abel Magembe Lugimba
Kada wa CCM Kalambo, Rukwa.
 
Suala la kufikiriwa mwalimu itakuwa lini serikali inadhani itafanya mapinduzi ktk elimu kwa kumtelekeza mwalimu hata kama ikifanya yote hayo?

Ukweli ni kwamba walimu wanakimbia fani sio kwa sababu nyingine bali kutafuta malisho mazuri hasa walimu wa sayansi wanabadili fani.

Habari ndio hiyo serikali ibadilike la sivyo viwanda ni ndoto.
 
Wataleta siasa za BRN, MMEM & MEMKWA. Mwisho wa siku waulize watoto wao kama wanasoma shule hizo ?!.
 
BONGO MOVIE............unatumia mabavu ili walimu wafanye kazi unayoitaka,wakati unaishi ikulu,akibolonga utajuaje
 
Back
Top Bottom